Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Nakumbuka kipindi Mbowe ameomba maridhiano akiwa Mwanza niliandika humu kuwa haki haiombwi, inachukuliwa.Ndiyo , kwa sababu CCM wanajua utamu wa madaraka . Utajiri wote unaoonekana Tanzania una mikono ya makada wa CCM.
Ukiona mashule ya Private ,mahospitali ya Private, Mabasi ,Malori, Mahoteli,viwanda, mashamba makubwa, Majengo kule Kisutu na Upanga ,matenda makubwa , Ajira kule Hazina n.k.
Watawala ndani ya Serali zote za CCM ndio wanaonufaika na kodi zote za watanzania. Kwao suala la pesa sio tatizo tena wanataka sasa kurithisha vizazi vyao Mali na madaraka milele na milele.
Ni jukumu la wagombea wa upinzani kujua kuwa Ubunge,udiwani na hata urais ni ajira muhimu inayopaswa kupiganiwa mana walioishika wanajua utamu wake na hawapo tayari kupokonywa.
CCM watawahonga mawakala na kuwatisha sana.
Na kwa sababu wapinzani wengi hawajawahi kushika madaraka wakihongwa hata mil. 10 wanaachia nafasi kumbe ni vijisenti wenzao wanavyovipata kama Chenji kwenye madaraka.
Haki inalindwa mana wanazulumu huwa wananufaika na dhulma zao na familia zao zinaishi maisha ya raha mustarehe mana mbaya zaidi kuna MTU mmoja mwenye madaraka makubwa kuliko Mungu hapa duniani anaweza kumlinda MTU yeyote popote na hakuna wa kumzuia wala kumhoji alimradi tu anakalia madaraka .
Ni jambo jema sana mwaka huu CCM itolewe au wabunge wake watolewe kwa namna ambayo haijawahi kutokea ili nchi hii iwe na watu wenye usawa na wenye kuheshimiana kuthaminiana bila kubaguana .