"O trade & logistics | Tanzania's National Development Corporation (NDC) signed a deal for $77 million with Fujian Hexingwang Industry Tanzania to facilitate iron... | Instagram" View: https://www.instagram.com/otl.trade/p/C_x1HCjidzG/
Diwani wa kata ya Kitandililo katika Halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe Imani Fute ameliomba taifa la china kuisaidia Tanzani kupata soko la parachichi, chai,korosho na ufuta.
Fute ametoa ombi hilo akiwa nchini china kwenye semina ya diplomasia ya uchumi wakati akizungumza katika semina hiyo yenye wawakilishi 42 kutoka mataifa 11 duniani, ambapo ameiomba china iisaidie Tanzania kwenye soko la mazao hayo huku akitaka ije iwekeze kwenye soko la kimataifa Makambako ambalo eneo limetengwa.
Fute amesema ombi hilo ni kutokana na jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hasan katika kukuza uchumi wa wananchi na Taifa letu.