Maajabu haya!! Usichokijua ni kwamba kwa nchi isiyofuata mipango ya kitaifa basi kila rais anakuwa na priority zake!!Si hayo ya ooh rais aje wa uchumi wa gas ,mara ooh kahama sijui nini wakati nothing on ground
Kwa mfano, kila mmoja anafahamu jinsi Mkapa alivyofanya ubinafsishaji kama ndiyo kipaumbele chake!! Na baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, kila mtu aliona jinsi ambavyo JK alivyofanya Gas Economy kama kipaumbele, na ndio maana hata huo mradi wa gas processing plant na ugunduzi wa cubic feet trillion 57 ulifanyika wakati wa JK na Muhongo wake!!
Alipoingia Magu, habari za gas akaziweka kando akajikita kwenye madini, hususani dhahabu!!!
Ni kutokana na hilo, ndio maana nikasema akija rais ambae priority yake itakuwa ni gas economy! Gas ya Songosongo kwa mfano, iligundulika tangia wakati wa Nyerere lakini hakuwa na time nayo hadi Mkapa alipoingia!
Hata Kahama, kabla ya uchimbaji mkubwa wa dhahabu haujaanza enzi za Mkapa, there's no way mtu angeweza kuilinganisha Kahama na Shinyanga lakini baada ya uchimbaji wa madini huku Almasi ikiwa ya kutafutwa kwa tochi Shinyanga, ghafla Kahama ikaanza kula sahani moja na Shinyanga!!
Sasa kinachokushangaza hapo nini?! Au hujui miradi mikubwa ndiyo ina-stimulate uchumi wa sehemu mbalimbali?!Au unaweza kulinganisha uchumi wa gas na uchumi wa kilimo uliopo Njombe?!