Mimi si Mbena wala Msukuma ila niko objective..
Kahama kwa Data ni Mji wa nane kwa wingi wa watu nchini.. na lazima uko kati ya miji 10 mikubwa nchini.
Kwenye drone footage naona mazingira... Ukitumia kigezo chakuwa na miti na maji yanatitirika basi Dubai na Dar haziwezi kuifikia Njombe..
Ukitaka kujua eneo ni potential.. angalia wangapi wanaamka bila kuwa na ndugu wanaamua kwenda kuanza maisha eneo hilo kila mwaka.. Kahama nchini ni kati ya miji mitano inayovutia vijana kuzamia..
Watoto wanatoka mikoa ya mbali wanaunga kwenye malori hata wasiokuwa na fedha wananing'inia chini huko ili wafike Kahama... Hii nimeoniona. Wanachokimbilia ni opportunities...
Wengi hapa wanaperception isiyo sawa kwa mji huu wa Kahama.. mji huu ulianza na madini.. ukakua na Mpunga na sasa unajiendesha na Biashara na Huduma.. hiyo ni natural progression ya mji wowote kukua..
River Thames lilikuwa bonde la kilimo.. ila leo london hakuna anayelima watu wameshatoka huko.. na wamejikita kwenye sehemu ya pili.. Biashara na huduma na hapo ndio mahala wanaanza kuwa true Urban Center.
Ukisikia Buzwagi na Bulyanhulu kila mtu anadhani Kahama inajiendesha na madini .. wachimba madini ni sehemu ndogo tu ya Uchumi mkubwa wa Kahama.. Kahama primarily today.. ukiulizwa ni Mji gani.. unasema mji wa kibiashara..
Na biashara ndiyo inaupa mji huu uhai. Hakuna mashamba na mbuga nyingi za mpunga hazizalishi tena kama zamani.. hivyo watu wamegeukia sekta nyingine.. kama manufacturing na Huduma.
Kahama wengi wamehamia kwenye Rice Processing and Exportation... Maize Milling and Exportation, Viwanda vya vinywaji, Mafuta, Mabati, Nguo, Samani za Ndani, Gold Ellussion (Kusafisha Dhahabu), Transportation, Ujenzi na Huduma kama Elimu na Hotels.
.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app