Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Hata mimi naamini uliyoyasema ni kweli, lakini nikushukuru kwa kitendo ulichokifanya baada ya kumaliza hoja yako cha kuturejesha kwenye maandiko uliyowahi kuyatoa katika mazingira ya namna hii, maana kuna uzi humu ndani unauliza kama wewe ulikuwa kwenye payroll ya Rugemarila. Sasa na tamka bila shaka yeyote kuwa wewe ni mtetezi wa haki za msingi za binadamu. Hongera sana.
 
I agree with you on this Pascal: "A person is innocent until proven guilty". Hawa watuhumiwa wawili hawana hatia mpaka mahakama itakaposema kuwa wana hatia na kuwapa hukumu stahiki.
 
Pascal upo sahihi 100%. Mahakama ni lazima ikemee na izuie uholela katika mazingira ya mahakama. Lakini pia hata huko mahabusu na magerezani wahusika wafuatilie kuona kama mahabusu na wqfungwa kama wanatendewa haki.

Lazima tupige vita Taifa kuwa na taratibu za hovyo na holela.
 
Dah! Nilifikiri ni mimi tu nimeliona, kutokana na muhemuko wa hili Jambo nikaona ngoja nikae kimya, ni kweli hao jamaa wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi lakini sikuona sababu yoyote ile ya kuwadharirisha, sasa walipiga magoti ili iweje??

Hivi hakuna kweli aliyejisaidia Haja Big pale?
 
Naona kuna Watu mmeamua kujitoa mhanga 100% katika awamu hii. Haya jamani kila la kheri na yangu macho tu.
 
Mayala ni gt mno humu jf na tunakutegemea.
Mada inayostahili kuanzishwa na wewe humu, inatakiwa "ichote" hadhira sawasawa. Hii ya kutetea mibaka uchumi unatugawa mashabiki wako.
Hiyo common law unayoitetea ina upande mmoja tu wa shilingi, haina upande wa pili.
Ninamaanisha kuwa sheria hiyo ni mahsusi kwa kutetea wahalifu tu, ama tuseme ipo ki haki za binadamu.
Unavyodai kuwa mwizi hawezi kuitwa mwizi hadi hapo mahakama itakapomtia hatiani. Msemo huo unajenga swali, je mwizi akiishatiwa hatiani, ulishawahi hata siku moja kusikia ameitwa mwizi? Baada ya kutiwa hatiani huwekewa "kava" tena na kuitwa mfungwa kwa tuhuma ya wizi a,b,c. Lakini kwa kutiwa kwake hatiani hairuhusiwi kumuita mwizi. Hakuna wakati wowote ambao mwizi anastahili kuitwa mwizi.
Vyombo vya habari kuwaita hao watuhumiwa wezi viko sahihi, kwa kuwa hapa Tanzania matendo maovu yanayofanywa na jamii huwa hairuhusiwi mahali popote kutumia hicho kiambishi katika uhuru wa kujieleza ama kutoa habari ya matendo ya watu hao.
Kwa nyie wasomi mgetunga kiswahili cha kuweza kutumia kutofautisha maneno.
Pia hili la kuchuchumalishwa nalo umelichambua kiubaguzi na kiutetezi zaidi. Kwani 'pozi' hilo hajawahi kufanyiwa mtuhumiwa mwingine ama sheria za ulinzi za askari jela wakiwa na mtuhumiwa "muhimu" hapo mahakamani zinasemaje?
Tunapokuwa kwenye kadhia kubwa za namna hii kitaifa nyie gt's tusaidieni kutudadavulia ili twende sote. Maana wengine tunaona lakini hatuelewi kinachoendelea. Sasa inapofika sehemu gt tegemeo unaanza kupanua ubawa ili kukinga hao mibaka, kwa kauli yoyote ile, sisi wepesi wa kubandika watu vyeo, moja kwa moja tunakuweka upande wa kina TL. Au unabishi?
 
Mkuu Paskali sijawahi kuthubutu kuipita "post" yako bila kuisoma thoroughly,this is yet another quality post, haina chembe ya unafiki.
 
This how GT deserve, Hongera mkuu Paskali wewe ni mmoja wa watu waliobaki humu ndani uliosababisha niwe mlevi wa JF.
Sio mafake wengine waliovamia humu either kupinga au kusifia kila kitu, they are nonsense at all.
 
Ujue uzuri mmoja wa kukamatwa vibopa utazijua haki nyingine ambazo hata hazisemwi kila siku wanavyokamatwa makapuku.
 
Hiyo ni sawa tu na perp walk.

Dominic Strauss-Kahn alitembezwa mbele ya waandishi akiwa amefungwa pingu.

Wengine wakiwa booked mug shots zao huwekwa public.

Sioni kabisa tatizo la hao wawili kupigwa picha kwenye hali hiyo.
 
wewe ni mpumbavu sana,

umeona hee! you sound like the one! sasa ungekuwa wa tatu ndio ungekoma!!

kwa kifupi ulichoongea ni poor thinking!!! eti mbona haukulalamika kipindi kile kwa watu wale!!! aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…