Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kuna tatizo kwenye mtaala wa mafunzo ya upolisi Kule Moshi na sijui Kurasini. Assessment na evaluation inatakiwa iwe carried out to review mtaala huo ili polisi wetu wawe na akili angalau kadogo maana kwa sasa they are not rational. Vinginevyo Siku nitakayoingia madarakani nchi hii na vunja jeshi lote naanza upya
 
Tuko kwenye kick mode. Bila kudhalilisha hatuonekani tunatetea wanyonge. Sio mbaya wacha walioko madarakani wafanye watakavyo lakini mlango umeshafunguliwa kwamba ukiwa madarakani fanya upendavyo lakini ukitoka utakutano na ulichowafanyia wenzio, kama ni kinyume utaisoma namba. Mfano halisi muone Sumaye saa hii analimia meno. Lakini enzi zake alikuwa anawachukulia wapinzani ni kama mashetani.
Well said
 
Dah! Nilifikiri ni mimi tu nimeliona, kutokana na muhemuko wa hili Jambo nikaona ngoja nikae kimya, ni kweli hao jamaa wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi lakini sikuona sababu yoyote ile ya kuwadharirisha, sasa walipiga magoti ili iweje??
Hii nchi kuna uonevu mkubwa sn
 
Mkuu siyo kwamba mwizi anapewa heshima na utukufu, la hasha, isipokuwa mwizi ana haki yake kisheria. Anakuwa ni mtuhumiwa tu hadi hapo ushahidi wa kumtia hatiani utakapokamilika. Na ushahidi wenyewe usiwe na shaka yeyote.( beyond any reasonable doubt)
Mr danny.kw hiyo kupigwa picha ni KUHUKUMIWA!!!???naamini hata wewe hukuwepo mahakamani lkn umejuaje km sio kupiga picha!!??WATANZANIA TUACHE U BUSH LAWYER.
 
Huku ni kudhalilisha watu kabisa... Kitendo hiki ni cha kulaaniwa...

Hao ni washitakiwa, bado si wahalifu....
 
Arusha kuna wanachama wa chadema walipigwa kwenye kesi ya lema mpaka wakashona nyuzi za kutosha,lkn mlikaa
Kimya apandacho mtu ndicho avunacho
 
Paskali unasema unaamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni. Jee, unawaongelea hawahawa polisi wa Tanzania au wa nchi nyingine? The last time I checked, mtu akipata division zero au division bashite ndio hua anaenda kujiunga na jeshi la polisi na wengi wao hata kuandika maelezo tu vituoni ni shida, sasa je watajuaje sheria kama hizo? Paskali tafadhali kuwa serious kidogo!
Mmhhh hio chukI haisaidii bt pia sio polisi walio wapiga picha.
BADALA YA KULALAMIKA KUHUSU UKOSEFU WA ELIMU WA POLISI WASOMI MUENDE MKAJIUNGE NA POLISI ILI MBADILISHE MUUNDO WAKE HII ITASAIDIA KULETA UFANISI KATIKA KAZI ZA POLISI KINYUME NA HAPO UTAENDELEA KUONYOOSHWA NA HAO UNAOWAITA DIVISION BASHITE MPK MWISHO WA DUNIA
 
Acha kujipendekeza kwa hiyo hawa jama wa escrow wakipigwa picha ndo mnaona kosa ila wengine wa kawaida walipokuwa wanapigwa picha ilikuwa sawa kwa nn iwe wakat wa watuhumiwa wa escrow
 
Mmhhh hio chukI haisaidii bt pia sio polisi walio wapiga picha.
BADALA YA KULALAMIKA KUHUSU UKOSEFU WA ELIMU WA POLISI WASOMI MUENDE MKAJIUNGE NA POLISI ILI MBADILISHE MUUNDO WAKE HII ITASAIDIA KULETA UFANISI KATIKA KAZI ZA POLISI KINYUME NA HAPO UTAENDELEA KUONYOOSHWA NA HAO UNAOWAITA DIVISION BASHITE MPK MWISHO WA DUNIA
Wanipata wapi mimi hao vilaza zaidi ya kunisimamisha kwenye gari na kuniandikia faini ya TZS 30,000? Tena siku hizi hata siongei nao nawaambia tu andika nikalipe! Halafu mimi nilianza kufaulu shule ya msingi mpaka chuo kikuu kwa hiyo sikuwa na nafasi ya kujiunga polisi kwa sababu sikuwa na sifa yao kuu ambayo ni kufeli.
 
Kuna kitu naona hakipo sawa labda mimi sijui hivi wenzetu mlio soma na kufaulu kwanini msitumie usomi wenu kubadilisha sheria iliyounda jeshi la polisi na kubadilisha vigezo vya kujiunga na polisi mpo bungeni na ma PHD yenu mnakula posho na kugonga meza mambo ya msingi hamuyaangalii kazi kulaumu na kudharau nyie wasomi ndo mnaruhusu kina Ally Kesi wanatukana watu mnawasifia nyie wasomi mliofaulu ndo mnaongoza kutumia wasio soma kwa maslahi yenu na kwa kua hata wewe uliepass kuanzia vidudu mpaka chuo kikuu umeshindwa kufata sheria ndogo za usalama barabarani zilizowekwa na wasomi wenzako hii inaonesha hata wasomi hamuheshimiani acha mnyooshwe na MABASHITE
 
Mr danny.kw hiyo kupigwa picha ni KUHUKUMIWA!!!???naamini hata wewe hukuwepo mahakamani lkn umejuaje km sio kupiga picha!!??WATANZANIA TUACHE U BUSH LAWYER.
Sina uhakika kama umenielewa. Na pia mimi siyo bush lawyer mkuu.
 
Ni wazo zuri lakini kwa kuwa Mheshimiwa anakaimu atapata ukakasi.
 
huo sio udhalalishwaji bali ni utaratibu wa kawaida kabisa wa kumdhibiti mtuhumiwa yeyote yule akiwa chini ya askari haijalisha mtuhumiwa anafahamika sana au hafahamiki lazima akamatwe na awekwe chini ya ulinzi,
jambo hilo halifikii viwango vya kusema kuna ukiukwaji wa haki za binaadamu au sheria yoyote ile ya nchi.

watuhumiwa kama hao wana mtandao mkubwa unaojulikana na wengine hawafahamiki hivyo bila kuwadhibiti kwa style hiyo ni hatari sana. kuwekwa chini ya ulinzi kama huo huwezi kusema au kuita kuwa tayari wamehukumiwa ndio maana watuhumiwa huwekwa rumande hiyo haimaanishi kuwa tayari wamehukumiwa bali ni utaratibu ulio wekwa.

katika ulimwengu wa uhuru wa habari huwezi kuwazuia wanahabari kuwapiga picha watuhumiwa.
 
Udhalilishaji gani nihii mijizi???mbona mna leta ujinga... Hawa hawana uchungu wowote na wananchi
 
kwa tuhuma walizonazo na raia tulichukia sana walipoachwa pale mwanzo nawapongeza Polisi na Magereza kwa kuwafanya walichokifanya....
 
Malipo hapa hapa duniani
Za mwizi arobaini
Mwisho wa ubaya ni aibu na fedheha so wacha wafedheheshwe kidogo .... Den after kesi kuisha fedheha iendelee zaid
 
Back
Top Bottom