Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Mara nilipoona zile picha nilisikitika sana. Niliona huruma, yule mzee sinfa akashindwa kuchuchumaa akaliga magoti. Huu ni udhalilishaji. Haukubaliki. Sielewi ni kwa nini polisi wanadhalilisha sana watu. Au wao wapo juu ya sheria? Nina uhakika kwa nchi zinazojali sheria hii haipaswi kutendeka.. Ila in Tz, unaweza uliwa hata ukiwa polisi
Mshaanz kuhamisha magoli
 
Mayalla, ombi lako ni zuri lakini bahati mbaya limeangakia kwenye jamii ambayo haikupata elimu ya uraia ambayo humfundisha mtu kumpenda, kumheshimu na kumjali mwezake haya kama hamfahamu; lugha unayoisikia ndani ya bunge inatokana na ukoseu was elimu hiyo. Askari hutumia vitendo kutokaa na hisia za viongozi wao na jamii kwamba wakiona watafurahi! Na ndivyo inavyotokea, hivyo basi watoa hoja usione ajabu wakakukejeli na kukubeza kwani kwao wengine wanapofanyiwa kejeli kwao huwa ni furaha na wanapata simulizi ya siku. Ndani ya mada hii wamo watakaoanza kuwabeza watu ambao wewe haujawataja, watakuja na ukabila, udini, muonekano wa mtu na mangine mengi tu sijui wanayapata wapi, lakini kwa kuwa ndivyo walivyo basi wanajua na mungu wao.
 
Mbona kassim Hanga alipigishwa magoti mnazi1miaka ya 70 je K Hanga alikuwa na mpango wa kukimbia? Tuiache Serikali ifanye kazi na sisi WaTZ tupige kazi Tuache maneno
 
Paskali,

Tuache unafiki. Hebu niambie ni waTanzania wangapi wanaodharirishwa tena zaidi ya hao walioambiwa kuchuchumaa and no body cares?

Tuache huu unafiki. watu wamepiga kelele jinsi wafungwa/mahabusu wanavyokuwa treated, jinsi magereza yalivyo machafu but no body cares. hata sidhani kwenye bajeti kuna mbunge anasimama kuhoji magereza yanaendeshwa vipi. Leo singa singa ameambiwa achuchumae chini unaandika thread ndeefu kwamba amedharirishwa? Human rights zinakuwa human rights for the rich and stronger but not for the poor and the wretched of the earth? Si ndiyo?

Ngoja tusubiri tuambiwe kwamba inabidi wajengewe gereza lao maana yaliyopo ni machafu.

Kaka yangu Paskali, wazungu wanasema: If the society cannot protect the weak in its midst, what makes you think that they will protect the stronger when times come?

All I can say: Tupige kelele wee..lakini Magufuli anatufundishia watoto kitu kimoja muhimu sana (it may be late for me and you) kwamba CRIME DOESNT PAY! Tufanye kazi kwa bidii tule na kuridhika na tunachopata kwa halali. Mengine ni porojo.

Masanja
Paskali ameshitushwa n.a. role model wake wa biashara kupigishwa magoti
 
As much as siwakubali hao jamaa kutokana na tuhuma zao, ila hilo la kudhalilishwa sijalipenda, na huwa haitokei kwao tu, ni kila mtu anachuchumaa kisha waandishi wanawapiga picha, sijaelewa mantiki yake mpaka leo

Nakuunga mkono ulichokileta ila nimeshangaa kuleta baada ya hao watu ambao una kitu nao wamefanyiwa hivyo ndio unaileta, wale waliotajwa na Makonda walifanyiwa pia hivyo hivyo, ila hilo halikuzungumziwa

unafanana na mke wa pili!! nongwa tu!!

binadamu anafanya kitu, kukumbuka kitu kama ana ukaribu nacho na akili kaiwea hapo!! ndio anafanya kitu fulani!!!
 
I felt heart sick nilivyoona Mzee Rugemalila akipiga magoti na rozari yake.

Hakuna asiye mdhambi, hakuna apendaye kudharirishwa. Hakuna mkamilifu.

Wakipatikana na makosa wahukumiwe ila si busara kuwadharirisha.

Mtu akiwa na pesa lazima mumuabudu.

Huyo mzee ndio mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo?

Wangapi wamefanyiwa hivyo mkakaa kimya.

Muda mwingine askari wetu ni wapole sana hao ilitakiwa wanyanyuliwe kwa mitama kabisa

Waswahili wanasema "pesa sabuni ya roho"
 
Pascal umechelewa Manji, wapinzani wamefanyiwa hivyo sana. Polis wa tz wamefundishwa hasira.
 
Paskali, tatizo sio Mahakama bali ninyi wanahabari. Ktk Journalism ethics suala unalolalamikia linafundishwa na wanahabari waliosoma taaluma ya habari wanafundishwa, sasa iweje uiingize Mahakama hapa? Hata MCT wenyewe wametoa kijitabu kuhusu court reporting ili kuwaepusha wanahabari na matatizo wanayoweza kujikuta matatani, sasa

Binafsi siamini kama Mahakama waliruhusu hili, labda polisi maana jambo kama hilo haliwezi kutokea ndani ya Mahakama.
 
Hiv mwizi anatakiwa afanyiwe nn?? Ina maana hata magazeti yafungiwe kumwandika!!?? Hata kwenye taalifa ya habari watolewe.na ile kesi iendeshwe usiku!!!?? .Ni afrika tu mwizi anapewa heshima na utukufu km mfalme.
Mkuu siyo kwamba mwizi anapewa heshima na utukufu, la hasha, isipokuwa mwizi ana haki yake kisheria. Anakuwa ni mtuhumiwa tu hadi hapo ushahidi wa kumtia hatiani utakapokamilika. Na ushahidi wenyewe usiwe na shaka yeyote.( beyond any reasonable doubt)
 

Wanabodi,

Tanzania ni nchi yenye katiba inayoendeshwa kwa misingi ya haki, the rule of law kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni. Kwenye kila jambo linatekelezwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, mahakamani ni mahali pa kutoa haki, tunaomba usiruhusu vyumba na maeneo ya mahakama kutumika kuwa ni sehemu ya udhalilishaji wa watuhumiwa!. Status ya Watuhumiwa wowote mbele ya sheria ni innocent until proven guilt!. Kwa nini watuhumiwa wadhalilishwe tena mbele ya kamera huku wakipigwa picha na video?!.

Tanzania inafuata mfumo wa sheria wa ya Uingereza, common law, ambapo mtuhumiwa huhesabiwa not guilt until proven guilt. Mfumo huu hauruhusu kuwapiga picha watuhumiwa wowote wakiwa mikononi mwa polisi au ndani ya vyumba vya mahakama. Lengo la kuzuia ni ili kuwaepushia watuhumiwa kuhukumiwa na media, "media trial".

Kitendo walichofanyiwa watuhumiwa hawa wawili, Rugemalila na Sing kuchuchumalishwa chini mbele ya camera za waandishi, ni udhalilishaji wa hali ya juu ya haki za watuhumiwa na ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni!.

Lengo la watuhumiwa kuchuchumalishwa, ni wale watuhumiwa wanaoshikwa kwa kufanya fujo, hivyo huchuchumalishwa ili kuwazuia wasitoroke chini ya ulinzi, hivi kweli Rugemalila na umri ule, na Singasinga na unene ule, walikuwa na tishio lolote la kutoroka chini ya ulinzi hadi kuwa chuchumalisha?!.

Sio mara moja au mbili, watuhumiwa wanafolenishwa na kupigwa picha mikononi mwa polisi. Watuhumiwa wanapigwa picha ndani ya vyumba vya mahakama!. Huu ni ukiukwaji wa haki za watuhumiwa!.

Tanzania – Code of Ethical Practice for media photographers and ...

"Contravene laws or lawful orders prohibiting the taking for pictures in the precincts for courts. The law prohibits the taking of pictures of any person (Judges, jurors and witnesses) involved in a proceeding before the court, whether civil or criminal; or to publish any photograph taken in contravention of the order. It could be in the courtroom, in the precincts of the building in which the court is held, or the persons leaving or entering the precincts".

Kwa msio fahamu, hata watuhumiwa nao ni binadamu na haijalishi wamefanya kosa gani, nao wanastahili heshima na utu wa ubinaadamu wao na sio kudhalilishwa. Watuhumiwa wana haki zao ambao zinapaswa ziheshimiwe.

Hata wahalifu wanaohukumiwa kunyongwa, pia wana haki zao zinazopaswa kuheshimiwa. Mfano mtu aliyehukumiwa kunyongwa mpaka kufa, japo lengo ni afe, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa kwanza daktari ataitwa na kumpima akikutwa na ugonjwa wowote, adhabu ile haitekelezwi hadi atibiwe apone kabisa akiwa fit ndipo anyongwe hadi kufa. Kumnyonga mtu mgojwa ni kumuonea!. Kabla ya kunyongwa viongozi wa dini huitwa kumsalisha sala ya toba, kumuungamisha na kumuombea dua na kama ni Muislamu hutazamishwa kibla ndipo hunyongwa!. Lengo la kueleza haya ni kuonyesha kuwa hata wahalifu wana haki.

Hivyo ni ombi maalum kwa Kaimu Jaji Mkuu wetu, Dr. Ibrahim Juma, tunakuomba please usiruhusu maeneo ya mahakama na vyumba vya mahakama kutumika kama sehemu ya udhalilishaji utu wa watuhumiwa huu unaofanywa wanapokuwa mikononi kwa polisi na ndani ya vyumba vya mahakama zetu!.

Ndani ya vyumba vya mahakama za Uingereza, India na Afrika Kusini, watuhumiwa hawaruhusiwi kupigwa picha wakiwa ndani ya vyumba vya mahakama, au mikononi mwa polisi. Kama sisi tumerithi sheria za Uingereza, kwa nini tuende kinyume cha wenzetu, unless kwa kufanya hivyo, ndio maendeleo yenyewe!.

Kitendo cha kuwapiga picha watuhumiwa ndani ya vyumba vya mahakama, huku kamera za video zikiwamulika, ni kama kuwahukumu kupitia kitu kinachoitwa "media trial", mtu akiishaonyeshwa kwenye TV ni jambazi, hata akijakukutwa hana hatia, mtaani kila apitapo, watu watanyoosheana vidole, "jambazi yule!"

Naamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni, kwa nini haya yanafanyika na tunayanyamazia wakati sheria, taratibu na kanuni zipo wazi?!.

Wanasheria mliopo jf mtatusaidia kwa hili kama tulibadilishwa kutoka kufuata the common law or English Law into American law.

Nimetokea kumfahamu Prof. Ibrahim Juma kwa karibu na sina mashaka kabisa na uadilifu wake katika kutenda haki na kutoa haki ili tuu sio haki itendeke bali pia haki kuonekana imetendeka, "Justice must not only be done but must be seen to be done".

Paskali.
Rejea
Utetezi wa kutetea haki za binaadamu humu jf, sikuanza leo, na wala siwatetei hawa kwa sababu ni matajiri, nimepigia kelele siku nyingi na haya chini ni mabandiko yangu kutetea haki
1. Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji ...

2. Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani ...

3. Huu ni udhalilishaji wa Polisi kuwavisha mabango watuhumiwa ...

4. Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

5. Tukio zima la wachawi wawili waliodondoka na ungo huko kahama ...

6. ITV na "Morbid Curiosity", Very Unprofessional! | JamiiForums ...

7. Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo | JamiiForums | The Home of Great ...

8. Nini hasa maana ya utu? | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great ...

9. Swali kuhusu ma-fumanizi, na reaction za wafumaniaji ...

10. Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo ...

11. IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...

12. Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

13. Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? | Page 2 ...

14. TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali ...

15. Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...

16. Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..

17. Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...

18. Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .

19. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

20. Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .

21. Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .

22. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

23. Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |

24. Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...

25. Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..

26. Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .

27. Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J

28. Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...

29. Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...

30. Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...


Respect bro, wewe ni moja ya waandishi wa habari, walionifanya niwaheshimu baadhi yenu hapa Tanzania, mko wachache
 
Leo nakuunga mkono 100%.

Hiyo ni hukumu na adhabu kabla ya kuhukumiwa.

Ni udhalilishaji wa kibinadamu wa hali ya juu.

Fikiria hapo ni mahakamani na mbele ya kadamnasi, jee huko mahabusu watuhumiwa wanakuwa katika hali gani?

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Wote tumejazwa ujinga wa hali ya juu na mpaka sasa humu nchini hakuna wakututowa huo ujinga.

Au ni ujinga wa asili?
Hapana, hakuna ujinga wa asili, huu tulionao ni wa kusomea. Kuna swali huwa unauliza mara kwa mara. "Hivi huko shule mlienda kusomea ujinga"?Leo ndio jibu limepatikana.
 
Pascal umechelewa Manji, wapinzani wamefanyiwa hivyo sana. Polis wa tz wamefundishwa hasira.
FB_IMG_1497948497085.jpg
 
Masanja, kusema kweli watu wengi tulidhani kuchuchumalisha ni aina ya 'restraint' hadi jana nilipomwona JR! Maadam sasa tumeona mtu mzima akifanyiwa hivyo sasa tunaona kumbe ni udhalilishaji tu wa watuhumiwa na siyo unafiki kulalamikia. Kwa bahati mbaya wewe inaelekea umeshawahukumu watuhumiwa hao kuwa ni wahalifu na wanastahili kudhalilishwa!
 
Waliopiga picha siyo Polisi
Nawakizuiwa hao lazima mrudi hapa kuropoka
Kuna watu huwa mnatumia makalio kufikiri sio bure. Ni wao wenyewe tu waliamua kuchuchumaa?

Issue sio kupigwa picha, issue ni walichoambiwa wafanye ili wapigwe picha. Waandishi wao wako sahihi, kutuletea taarifa kama ilivyo. Ni kwa msaada wa camera zao ndio sasa tunajua kuwa walichuchumazwa. Je ni sheria gani inatumika kuwachuchumaza as if labda walikuwa wanaleta ubishi ndio ikabidi wadhibitiwe?
 
Back
Top Bottom