Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Acha ujinga bhn rugemalila ye kama nani asipige magoti je angelambwa na makofi ungesemaje acha kulinganisha haki na mambo ya kijinga mkuu
 
Paskali unasema unaamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni. Jee, unawaongelea hawahawa polisi wa Tanzania au wa nchi nyingine? The last time I checked, mtu akipata division zero au division bashite ndio hua anaenda kujiunga na jeshi la polisi na wengi wao hata kuandika maelezo tu vituoni ni shida, sasa je watajuaje sheria kama hizo? Paskali tafadhali kuwa serious kidogo!
asant mkuu
 
Paskali unasema unaamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni. Jee, unawaongelea hawahawa polisi wa Tanzania au wa nchi nyingine? The last time I checked, mtu akipata division zero au division bashite ndio hua anaenda kujiunga na jeshi la polisi na wengi wao hata kuandika maelezo tu vituoni ni shida, sasa je watajuaje sheria kama hizo? Paskali tafadhali kuwa serious kidogo!
Angeanzia na kupigia kelele mfumo mzima wa ajira kwenye jeshi letu la Polisi.Wengi wanadai kwamba elimu sio muhimu kwenye utendaji wa jeshi la Polisi.How naive.
 
Hiv mwizi anatakiwa afanyiwe nn?? Ina maana hata magazeti yafungiwe kumwandika!!?? Hata kwenye taalifa ya habari watolewe.na ile kesi iendeshwe usiku!!!?? .Ni afrika tu mwizi anapewa heshima na utukufu km mfalme.
 
Leo nakuunga mkono 100%.

Hiyo ni hukumu na adhabu kabla ya kuhukumiwa.

Ni udhalilishaji wa kibinadamu wa hali ya juu.

Fikiria hapo ni mahakamani na mbele ya kadamnasi, jee huko mahabusu watuhumiwa wanakuwa katika hali gani?

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Wote tumejazwa ujinga wa hali ya juu na mpaka sasa humu nchini hakuna wakututowa huo ujinga.

Au ni ujinga wa asili?
 
south africa ipi unayoisema we paskal mayalla hukumbuk kesi ya oscar pistorious iliendeshwa live luningani mpaka vyombo vya BBC
 
Hakuna jambo baya kama kuishi bila kuzingatia sheria na utaratibu. Kuishi vyovyote tu ni jambo baya zaidi kwa mwanadamu.
Hili ni tatizo la Serikali na raia wa Tanzania kwa ujumla wake.
Mara ngapi tumeshiriki kupiga na kuchoma moto vibaka kwa kisingizio cha wananchi wenye hasira?
Mara ngapi watu wamebambikiwa kesi na vyombo vya ulinzi na Usalama?
Mara ngapi watuhumiwa wameteswa na kudhalilishwa mikononi mwa vyombo vya ulinzi?

Kilichotokea kwa hao watuhumiwa kinatokea kila siku na tumeamua kuwa kimya.
Kuna msemo "justice for all or justice for none "
Ukiona mtu anaonewa usifurahi maana uonevu ni kama mnyororo utakufikia tu.
Note : sitetei uhalifu lakini tuna utaratibu tuliojiwekea wa kushughulikia wahalifu. Utaratibu ufuatwe.
 

Wanabodi,

Tanzania ni nchi yenye katiba inayoendeshwa kwa misingi ya haki, the rule of law kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni. Kwenye kila jambo linatekelezwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, mahakamani ni mahali pa kutoa haki, tunaomba usiruhusu vyumba na maeneo ya mahakama kutumika kuwa ni sehemu ya udhalilishaji wa watuhumiwa!. Status ya Watuhumiwa wowote mbele ya sheria ni innocent until proven guilt!. Kwa nini watuhumiwa wadhalilishwe tena mbele ya kamera huku wakipigwa picha na video?!.

Tanzania inafuata mfumo wa sheria wa ya Uingereza, common law, ambapo mtuhumiwa huhesabiwa not guilt until proven guilt. Mfumo huu hauruhusu kuwapiga picha watuhumiwa wowote wakiwa mikononi mwa polisi au ndani ya vyumba vya mahakama. Lengo la kuzuia ni ili kuwaepushia watuhumiwa kuhukumiwa na media, "media trial".

Kitendo walichofanyiwa watuhumiwa hawa wawili, Rugemalila na Sing kuchuchumalishwa chini mbele ya camera za waandishi, ni udhalilishaji wa hali ya juu ya haki za watuhumiwa na ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni!.

Lengo la watuhumiwa kuchuchumalishwa, ni wale watuhumiwa wanaoshikwa kwa kufanya fujo, hivyo huchuchumalishwa ili kuwazuia wasitoroke chini ya ulinzi, hivi kweli Rugemalila na umri ule, na Singasinga na unene ule, walikuwa na tishio lolote la kutoroka chini ya ulinzi hadi kuwa chuchumalisha?!.

Sio mara moja au mbili, watuhumiwa wanafolenishwa na kupigwa picha mikononi mwa polisi. Watuhumiwa wanapigwa picha ndani ya vyumba vya mahakama!. Huu ni ukiukwaji wa haki za watuhumiwa!.

Tanzania – Code of Ethical Practice for media photographers and ...

"Contravene laws or lawful orders prohibiting the taking for pictures in the precincts for courts. The law prohibits the taking of pictures of any person (Judges, jurors and witnesses) involved in a proceeding before the court, whether civil or criminal; or to publish any photograph taken in contravention of the order. It could be in the courtroom, in the precincts of the building in which the court is held, or the persons leaving or entering the precincts".

Kwa msio fahamu, hata watuhumiwa nao ni binadamu na haijalishi wamefanya kosa gani, nao wanastahili heshima na utu wa ubinaadamu wao na sio kudhalilishwa. Watuhumiwa wana haki zao ambao zinapaswa ziheshimiwe.

Hata wahalifu wanaohukumiwa kunyongwa, pia wana haki zao zinazopaswa kuheshimiwa. Mfano mtu aliyehukumiwa kunyongwa mpaka kufa, japo lengo ni afe, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa kwanza daktari ataitwa na kumpima akikutwa na ugonjwa wowote, adhabu ile haitekelezwi hadi atibiwe apone kabisa akiwa fit ndipo anyongwe hadi kufa. Kumnyonga mtu mgojwa ni kumuonea!. Kabla ya kunyongwa viongozi wa dini huitwa kumsalisha sala ya toba, kumuungamisha na kumuombea dua na kama ni Muislamu hutazamishwa kibla ndipo hunyongwa!. Lengo la kueleza haya ni kuonyesha kuwa hata wahalifu wana haki.

Hivyo ni ombi maalum kwa Kaimu Jaji Mkuu wetu, Dr. Ibrahim Juma, tunakuomba please usiruhusu maeneo ya mahakama na vyumba vya mahakama kutumika kama sehemu ya udhalilishaji utu wa watuhumiwa huu unaofanywa wanapokuwa mikononi kwa polisi na ndani ya vyumba vya mahakama zetu!.

Ndani ya vyumba vya mahakama za Uingereza, India na Afrika Kusini, watuhumiwa hawaruhusiwi kupigwa picha wakiwa ndani ya vyumba vya mahakama, au mikononi mwa polisi. Kama sisi tumerithi sheria za Uingereza, kwa nini tuende kinyume cha wenzetu, unless kwa kufanya hivyo, ndio maendeleo yenyewe!.

Kitendo cha kuwapiga picha watuhumiwa ndani ya vyumba vya mahakama, huku kamera za video zikiwamulika, ni kama kuwahukumu kupitia kitu kinachoitwa "media trial", mtu akiishaonyeshwa kwenye TV ni jambazi, hata akijakukutwa hana hatia, mtaani kila apitapo, watu watanyoosheana vidole, "jambazi yule!"

Naamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni, kwa nini haya yanafanyika na tunayanyamazia wakati sheria, taratibu na kanuni zipo wazi?!.

Wanasheria mliopo jf mtatusaidia kwa hili kama tulibadilishwa kutoka kufuata the common law or English Law into American law.

Nimetokea kumfahamu Prof. Ibrahim Juma kwa karibu na sina mashaka kabisa na uadilifu wake katika kutenda haki na kutoa haki ili tuu sio haki itendeke bali pia haki kuonekana imetendeka, "Justice must not only be done but must be seen to be done".

Paskali.
Rejea
Hili sikuanza kulipigia kelele leo kwa sababu tuu ya Rugemalila na Singasinga, nimewahi kulipigia kelele.
Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji ...
Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani ...
Huu ni udhalilishaji wa Polisi kuwavisha mabango watuhumiwa ...
Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...
Tukio zima la wachawi wawili waliodondoka na ungo huko kahama ...
ITV na "Morbid Curiosity", Very Unprofessional! | JamiiForums ...
Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo | JamiiForums | The Home of Great ...
Nini hasa maana ya utu? | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great ...
Swali kuhusu ma-fumanizi, na reaction za wafumaniaji ...
Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? | Page 2 ...

TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali ...

Umenena kweli pamoja na kwamba hao jamaa siwakubali kutokana na mambo yao hayo, lakini kitendo walicho fanyiwa si haki kabisa na kinafaa kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote, na mara kadhaa tumekuwa tukiona matukio kama hayo yakifanywa na police wetu, na hakuna hatua yoyote iliyo chukuliwa dhidi yao ili mradi wanachofanya kinampendeza mtu flani basi hata kama wamevunja sheria wanaonekana wapo sawa: it's so ☹️☹️
 

hivi kweli Rugemalila na umri ule, na Singasinga na unene ule, walikuwa na tishio lolote la kutoroka chini ya ulinzi hadi kuwa chuchumalisha?!.

What if kuna wafanikishaji wa utorokaji? What if walishaattempt kutoroka kabla hawajafikishwa mahakamani? What if walionyesha resistance kubwa wakati wa kukamatwa kiasi cha kuwafanya polisi wapunguze imani juu yao? What if kulikuwa na dalili /signals za kimawasiliano zinozitia shaka baina ya watuhumiwa hao na baadhi ya watu. Kuchuchumalishwa kuna maana nyingi zaidi ya udhalilishaji unaouona wewe.
 
Mkuu ungeanzia kulisemea toka kipindi kile watu flani falni waliokuwa wakiropokwa na Bwana yule tungekuelewa kwa hili naomba Kaimu Jaji uliache kwanza mpaka zamu za woote ziishe alafu tuanze fresh!!
 
Ndugu jenga hoja ....watu wameshasahau habari za Bashite ....sana sana ukisikia hamu ya kuzijua ipo sehemu moja tu ndio utazipata kule instagram ....otherwise discussions iliyopo sasa ni Makinikia and IPTL ....usishindane na wakati ndugu watu washahama huko ....[emoji38] [emoji38] [emoji38]
Mkuu hakuna aliyesahau ila thr is nothin they can do but ukweli utabaki kiwa ukweli kuwa magufuli kuna watu anawalinda ila nachojua cku akiacha madaraka huyo kijana atafutika kwenye siasa za tanzania kma january na jerry slaa

Muda utaamua yote
 
Mara nilipoona zile picha nilisikitika sana. Niliona huruma, yule mzee sinfa akashindwa kuchuchumaa akaliga magoti. Huu ni udhalilishaji. Haukubaliki. Sielewi ni kwa nini polisi wanadhalilisha sana watu. Au wao wapo juu ya sheria? Nina uhakika kwa nchi zinazojali sheria hii haipaswi kutendeka.. Ila in Tz, unaweza uliwa hata ukiwa polisi
 
Unaleta ubishi wakati hujui hizo taratibu. Nenda kaulize Askari Magereza au wafanyakazi wa Mahakama watakupa ufumbuzi.
Ubishi gani jiulize hio picha walikua wanasubiri gari au ndo wanaingia ndani .
wacha ubishi hapo walikua wanaingia..
 
Back
Top Bottom