Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Watuhumiwa walitakiwa wakatae, sidhani kama walilazimishwa. Labda walielekezwa tu wakakubali ili ipatikane picha nzuri kwa kumbukumbu.
 
Utafanya jaji asusiwe kutangazwa habari zake na akina Meena kwa kuwakataza waandishi kupiga picha watuhumiwa.
Na wahariri nao ni vilaza,wataruhusu vipi picha zitolewe?
 
Umeongea sawa mkuu, sio haki kwa mtuhumiwa yeyote ambaye haonyeshi kutaka kukimbia kumfanya hivyo, pia la kupiga picha jamii yetu imekumbwa na ka ulimbukeni ka mapichamapicha, mf utaona mwalimu anamwadhibu mwanafunzi anarekodi na kutupia mtandaoni, polisi nao wameingia kwenye mtego huo bila kujali ethics za kazi zao, hii iko mpaka kwa viongozi wao, mf jamaa kaenda kuripoti polisi afisa wa cheo cha juu anaomba selfie kwa mtuhumiwa kwa vile ni superstar, aibu!
 
Kwa mara ya kwanza Pascal nalazimika kukuunga mkono kwa 100% tangu nianze kuziona hizo picha mtandaoni ile jana na magazetini leo nimeshindwa kuelewa ni nini Tanzania inajaribu kuonyesha ulimwengu!! Sasa kama mtuhumiwa anafanyiwa hivi ili familia yake wajionee, je mhukumiwa anafanyiwaje huko jela? Hivi mpaka miaka 5 ikiisha si hata kina Kagame, M7 na hata Iddi Amin wataonekana kama malaika. Nafikiri si muda mrefu wafungwa na watuhumiwa wataanza kusafirishwa kwa makarandinga.

Why the presumption of innocence is so important. We all know that in criminal law, every person is presumed innocent, until proven guilty beyond a reasonable doubt. ... In the context of a criminal trial, this means the starting point for the judge / jury is that the accused person is innocent.

The Universal Declaration of Human Rights, article 11, states: "Everyone charged with a penal offence has the right to be presumed innocent until proved guilty according to law in a public trial at which he has had all the guarantees necessary for his defence.".
 

Hii ya kuwafunga pingu watuhumuiwa mahakamani ipo mpaka USA. Mara nyingi inatokea kwa aina ya makosa na aina ya mtuhumiwa kama Scorpion aliyemtoboa mtu macho na yeyey ni mtu wa karate lazima ale pingu mahakamani.

South Africa, baadhi ya watuhumiwa wanakula pingu mikonono na cheni miguuni kuanzia mpaka mwisho wa kusomewa kesi mahakamani na anapandanazo kwenye gari mpaka Gerezani ndipo zinafunguliwa.
 
Paskali hawa walishaahidiwa bilioni 7 ili hukunu ziende kama inavyotakiwa na wenye nchi. Haya ya kudhalilishana madogo sana. Ukiwachokonoa watapeleka muswada bure! Kudhalilishane kubarikiwe na sheria!
 
Sasa Kama mawazo ya nchi yameshikwa Mabashite unategemea nini ? Tupo kwenye show off tukimaliza tutarudi kwenye code of conduct.
Jaña niliuliza kulikuwa na haja ya kuwachuchumalisha na kuwapigisha magoti?? Wengine wakaniita mtetezi wao!
 
Hata mimi nilishangaa kuwarusha kichura wazee kama wale bila kujali uzito wa tuhuma zinazowakabili. Hivi wale wangekimbia kwenda wapi!
 
"Mwizi ni mwizi tu, kule kwetu Tarime, hakuna formula maalum ya kumshughulikia mwizi" "John Heche.
 
Siwezi juwa kama ni watuhumiwa ndio walio omba wapigwe picha na maofisa wa polisi au ni polisi waliotaka wapigwe picha pamoja na watumiwa, ila kwamtazamo wangu naona muonekano wa picha hizi ni kama wamedhalilishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…