Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Watuhumiwa walitakiwa wakatae, sidhani kama walilazimishwa. Labda walielekezwa tu wakakubali ili ipatikane picha nzuri kwa kumbukumbu.
 
Utafanya jaji asusiwe kutangazwa habari zake na akina Meena kwa kuwakataza waandishi kupiga picha watuhumiwa.
Na wahariri nao ni vilaza,wataruhusu vipi picha zitolewe?
 
upload_2017-6-20_19-47-45.jpeg
 
Umeongea sawa mkuu, sio haki kwa mtuhumiwa yeyote ambaye haonyeshi kutaka kukimbia kumfanya hivyo, pia la kupiga picha jamii yetu imekumbwa na ka ulimbukeni ka mapichamapicha, mf utaona mwalimu anamwadhibu mwanafunzi anarekodi na kutupia mtandaoni, polisi nao wameingia kwenye mtego huo bila kujali ethics za kazi zao, hii iko mpaka kwa viongozi wao, mf jamaa kaenda kuripoti polisi afisa wa cheo cha juu anaomba selfie kwa mtuhumiwa kwa vile ni superstar, aibu!
 
Kwa mara ya kwanza Pascal nalazimika kukuunga mkono kwa 100% tangu nianze kuziona hizo picha mtandaoni ile jana na magazetini leo nimeshindwa kuelewa ni nini Tanzania inajaribu kuonyesha ulimwengu!! Sasa kama mtuhumiwa anafanyiwa hivi ili familia yake wajionee, je mhukumiwa anafanyiwaje huko jela? Hivi mpaka miaka 5 ikiisha si hata kina Kagame, M7 na hata Iddi Amin wataonekana kama malaika. Nafikiri si muda mrefu wafungwa na watuhumiwa wataanza kusafirishwa kwa makarandinga.

Why the presumption of innocence is so important. We all know that in criminal law, every person is presumed innocent, until proven guilty beyond a reasonable doubt. ... In the context of a criminal trial, this means the starting point for the judge / jury is that the accused person is innocent.

The Universal Declaration of Human Rights, article 11, states: "Everyone charged with a penal offence has the right to be presumed innocent until proved guilty according to law in a public trial at which he has had all the guarantees necessary for his defence.".
 
Well said PASKALI. Hata mimi hii hali ya kuwafolenisha watuhumiwa ili wapigwe picha na maneno ya kifedhuli yanayotolewa na walinzi wetu wa amani, ni udhalilishaji mkubwa. Hao wazee wamekaa nao, wamewahoji, wamewaleta mahakamani; kulikuwa na haja gani kuwaamrisha wachuchumae? (Singh ndo alipiga goti kabisa). Kuna wakati mwingine askari magereza huwaleta mahabusu wakiwa wamefungwa pingu hadi ndani ya vyumba vya mahakama, na kuwafungua tu pale hakimu anapokaribia kuanza session.

Ni vema kutunza utu wa mtu hata kama ni mtuhumiwa!

Hii ya kuwafunga pingu watuhumuiwa mahakamani ipo mpaka USA. Mara nyingi inatokea kwa aina ya makosa na aina ya mtuhumiwa kama Scorpion aliyemtoboa mtu macho na yeyey ni mtu wa karate lazima ale pingu mahakamani.

South Africa, baadhi ya watuhumiwa wanakula pingu mikonono na cheni miguuni kuanzia mpaka mwisho wa kusomewa kesi mahakamani na anapandanazo kwenye gari mpaka Gerezani ndipo zinafunguliwa.
 
Paskali hawa walishaahidiwa bilioni 7 ili hukunu ziende kama inavyotakiwa na wenye nchi. Haya ya kudhalilishana madogo sana. Ukiwachokonoa watapeleka muswada bure! Kudhalilishane kubarikiwe na sheria!
 
Sasa Kama mawazo ya nchi yameshikwa Mabashite unategemea nini ? Tupo kwenye show off tukimaliza tutarudi kwenye code of conduct.
Jaña niliuliza kulikuwa na haja ya kuwachuchumalisha na kuwapigisha magoti?? Wengine wakaniita mtetezi wao!
 
Hata mimi nilishangaa kuwarusha kichura wazee kama wale bila kujali uzito wa tuhuma zinazowakabili. Hivi wale wangekimbia kwenda wapi!
 

Wanabodi,

Tanzania ni nchi yenye katiba inayoendeshwa kwa misingi ya haki, the rule of law kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni. Kwenye kila jambo linatekelezwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, mahakamani ni mahali pa kutoa haki, tunaomba usiruhusu vyumba na maeneo ya mahakama kutumika kuwa ni sehemu ya udhalilishaji wa watuhumiwa!. Status ya Watuhumiwa wowote mbele ya sheria ni innocent until proven guilt!. Kwa nini watuhumiwa wadhalilishwe tena mbele ya kamera huku wakipigwa picha na video?!.

Tanzania inafuata mfumo wa sheria wa ya Uingereza, common law, ambapo mtuhumiwa huhesabiwa not guilt until proven guilt. Mfumo huu hauruhusu kuwapiga picha watuhumiwa wowote wakiwa mikononi mwa polisi au ndani ya vyumba vya mahakama. Lengo la kuzuia ni ili kuwaepushia watuhumiwa kuhukumiwa na media, "media trial".

Kitendo walichofanyiwa watuhumiwa hawa wawili, Rugemalila na Sing kuchuchumalishwa chini mbele ya camera za waandishi, ni udhalilishaji wa hali ya juu ya haki za watuhumiwa na ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni!.

Lengo la watuhumiwa kuchuchumalishwa, ni wale watuhumiwa wanaoshikwa kwa kufanya fujo, hivyo huchuchumalishwa ili kuwazuia wasitoroke chini ya ulinzi, hivi kweli Rugemalila na umri ule, na Singasinga na unene ule, walikuwa na tishio lolote la kutoroka chini ya ulinzi hadi kuwa chuchumalisha?!.

Sio mara moja au mbili, watuhumiwa wanafolenishwa na kupigwa picha mikononi mwa polisi. Watuhumiwa wanapigwa picha ndani ya vyumba vya mahakama!. Huu ni ukiukwaji wa haki za watuhumiwa!.

Tanzania – Code of Ethical Practice for media photographers and ...

"Contravene laws or lawful orders prohibiting the taking for pictures in the precincts for courts. The law prohibits the taking of pictures of any person (Judges, jurors and witnesses) involved in a proceeding before the court, whether civil or criminal; or to publish any photograph taken in contravention of the order. It could be in the courtroom, in the precincts of the building in which the court is held, or the persons leaving or entering the precincts".

Kwa msio fahamu, hata watuhumiwa nao ni binadamu na haijalishi wamefanya kosa gani, nao wanastahili heshima na utu wa ubinaadamu wao na sio kudhalilishwa. Watuhumiwa wana haki zao ambao zinapaswa ziheshimiwe.

Hata wahalifu wanaohukumiwa kunyongwa, pia wana haki zao zinazopaswa kuheshimiwa. Mfano mtu aliyehukumiwa kunyongwa mpaka kufa, japo lengo ni afe, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa kwanza daktari ataitwa na kumpima akikutwa na ugonjwa wowote, adhabu ile haitekelezwi hadi atibiwe apone kabisa akiwa fit ndipo anyongwe hadi kufa. Kumnyonga mtu mgojwa ni kumuonea!. Kabla ya kunyongwa viongozi wa dini huitwa kumsalisha sala ya toba, kumuungamisha na kumuombea dua na kama ni Muislamu hutazamishwa kibla ndipo hunyongwa!. Lengo la kueleza haya ni kuonyesha kuwa hata wahalifu wana haki.

Hivyo ni ombi maalum kwa Kaimu Jaji Mkuu wetu, Dr. Ibrahim Juma, tunakuomba please usiruhusu maeneo ya mahakama na vyumba vya mahakama kutumika kama sehemu ya udhalilishaji utu wa watuhumiwa huu unaofanywa wanapokuwa mikononi kwa polisi na ndani ya vyumba vya mahakama zetu!.

Ndani ya vyumba vya mahakama za Uingereza, India na Afrika Kusini, watuhumiwa hawaruhusiwi kupigwa picha wakiwa ndani ya vyumba vya mahakama, au mikononi mwa polisi. Kama sisi tumerithi sheria za Uingereza, kwa nini tuende kinyume cha wenzetu, unless kwa kufanya hivyo, ndio maendeleo yenyewe!.

Kitendo cha kuwapiga picha watuhumiwa ndani ya vyumba vya mahakama, huku kamera za video zikiwamulika, ni kama kuwahukumu kupitia kitu kinachoitwa "media trial", mtu akiishaonyeshwa kwenye TV ni jambazi, hata akijakukutwa hana hatia, mtaani kila apitapo, watu watanyoosheana vidole, "jambazi yule!"

Naamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni, kwa nini haya yanafanyika na tunayanyamazia wakati sheria, taratibu na kanuni zipo wazi?!.

Wanasheria mliopo jf mtatusaidia kwa hili kama tulibadilishwa kutoka kufuata the common law or English Law into American law.

Nimetokea kumfahamu Prof. Ibrahim Juma kwa karibu na sina mashaka kabisa na uadilifu wake katika kutenda haki na kutoa haki ili tuu sio haki itendeke bali pia haki kuonekana imetendeka, "Justice must not only be done but must be seen to be done".

Paskali.
Rejea
Utetezi wa kutetea haki za binaadamu humu jf, sikuanza leo, na wala siwatetei hawa kwa sababu ni matajiri, nimepigia kelele siku nyingi na haya chini ni mabandiko yangu kutetea haki
1. Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji ...

2. Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani ...

3. Huu ni udhalilishaji wa Polisi kuwavisha mabango watuhumiwa ...

4. Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

5. Tukio zima la wachawi wawili waliodondoka na ungo huko kahama ...

6. ITV na "Morbid Curiosity", Very Unprofessional! | JamiiForums ...

7. Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo | JamiiForums | The Home of Great ...

8. Nini hasa maana ya utu? | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great ...

9. Swali kuhusu ma-fumanizi, na reaction za wafumaniaji ...

10. Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo ...

11. IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...

12. Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

13. Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? | Page 2 ...

14. TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali ...

15. Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...

16. Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..

17. Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...

18. Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .

19. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...

20. Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .

21. Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .

22. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

23. Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |

24. Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...

25. Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..

26. Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .

27. Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J

28. Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...

29. Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...

30. Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...


"Mwizi ni mwizi tu, kule kwetu Tarime, hakuna formula maalum ya kumshughulikia mwizi" "John Heche.
 
Siwezi juwa kama ni watuhumiwa ndio walio omba wapigwe picha na maofisa wa polisi au ni polisi waliotaka wapigwe picha pamoja na watumiwa, ila kwamtazamo wangu naona muonekano wa picha hizi ni kama wamedhalilishwa
448fb21c95976b61c88514ceef5df588.jpg
abcc65016be005954fd07e5918703ad2.jpg
 
Back
Top Bottom