Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jiulize kabla ya kufanya ufisadiHuu sio ustaarabu na ni unyama wa kiwango cha hali ya juu, wewe kama binadamu jiulize kwanza kabla kumfanyia mwenzio kitendo chochote kama uko tayari wewe kufanyiwa hivyo unavyotaka kumfanyia mwenzao.
wezi wa kuku mwenye thamani ya 10000 anavishwa tairi hawa wa mabilioni unataka tuwapetipeto?Nyie watu sijui mnaakili gani ?!!
Sisi ndugu zetu wezi wa kuku kila siku wanadhalilishwa lkn kuonekana picha hizi ndio mnajifanya mnaumia....
Hawa ni wahalifu, utaratibu uendelee kama kawaida.
Hukuona wale watuhumiwa wa mihadarati walivyozalilishwa? tena wale hadi wakina mama waliambiwa wachuchumae., rule of law inapaswa iangaliwe kwa wananchi wote regardless ni akina nani katika jamii
Sawa mkuuNinamaanisha yeyote anayefanyiwa hivi si sahihi, haijalishi amefanya kosa gani, mahali pa kutoa hukumu ni mbele ya mahakama na sio kabla ya hapo.
Una pointwezi wa kuku wakidhalillishwa sawa tu ila kwa rugemalila ni udhalilishaji nyie wabongo kwa kujipendekeza ni mabingwa
Hizi sheria zingine zahovyo
Mtu kasababisha uhai wa wenzie upotee kwa ufisadi wao
Bado apelekwe kama Yai!!
Singasinga alipiga magoti kwa ridhaa yake baada ya kushindwa kuchutama kutokana na kitambi/ubwanyenye. Kuna watu wanatokwa na povu humu, wamesahau kwamba Yona na Mramba nao walichutama pia mkuu.Double standard... gazeti lefu kisa singa singa kapigishwa magoti na bado!!!!
Wanadhalilishwa kina mnyika bungeni umenyamaza hili la jana ndo linakumiza...
Dah! Nilifikiri ni mimi tu nimeliona, kutokana na muhemuko wa hili Jambo nikaona ngoja nikae kimya, ni kweli hao jamaa wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi lakini sikuona sababu yoyote ile ya kuwadharirisha, sasa walipiga magoti ili iweje??
Paskali hajaandika vilema wale kula kipigo posta!Paskali,
Tuache unafiki. Hebu niambie ni waTanzania wangapi wanaodharirishwa tena zaidi ya hao walioambiwa kuchuchumaa and no body cares?
Tuache huu unafiki. watu wamepiga kelele jinsi wafungwa/mahabusu wanavyokuwa treated, jinsi magereza yalivyo machafu but no body cares. hata sidhani kwenye bajeti kuna mbunge anasimama kuhoji magereza yanaendeshwa vipi. Leo singa singa ameambiwa achuchumae chini unaandika thread ndeefu kwamba amedharirishwa? Human rights zinakuwa human rights for the rich and stronger but not for the poor and the wretched of the earth? Si ndiyo?
Ngoja tusubiri tuambiwe kwamba inabidi wajengewe gereza lao maana yaliyopo ni machafu.
Kaka yangu Paskali, wazungu wanasema: If the society cannot protect the weak in its midst, what makes you think that they will protect the stronger when times come?
All I can say: Tupige kelele wee..lakini Magufuli anatufundishia watoto kitu kimoja muhimu sana (it may be late for me and you) kwamba CRIME DOESNT PAY! Tufanye kazi kwa bidii tule na kuridhika na tunachopata kwa halali. Mengine ni porojo.
Masanja
Wezi wa Kuku wanadhalilishwa Mitaani na Vijilante wengi wao Wahuni wasio na maadili. Sio jukumu la Serika au mahakama kudhalilisha watu. Under the Rule of Law you are innocent Untill proven guity!Acha unafiki mbona vibaka wa kuku wanadharirishwa kila siku na hujawahi kusema au kwasababu hao mabilionea ndio povu linakutoka