BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,527
- 3,811
Pascal ndio umegundua jana kama huo ni udhalilishaji? Au kwakuwa ni Ruge na Singa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizi sheria zingine zahovyo
Mtu kasababisha uhai wa wenzie upotee kwa ufisadi wao
Bado apelekwe kama Yai!!
Mbona huo ni utaratibu wa kawaida pale mahakamani. Mtuhumiwa akitoka ndani ya Mahakama wakati anasubiri karandinga anatakiwa kuchuchumaa ili asikimbie. Huu utaratibu umekuwepo kwa muda tu. Nashangaa leo kuna watu mnajitoa fahamu! Au kwa kuwa ni Singasinga na Ruge!? Inapelekea kuamini kwamba Bwana Pascal Mayalla umeshachukua bahasha kutoka huko kunako "Dude".
Umesahau ya kwamba Yona na Mramba nao walichutama wakati wanasubiri karandinga!?
Unaleta ubishi wakati hujui hizo taratibu. Nenda kaulize Askari Magereza au wafanyakazi wa Mahakama watakupa ufumbuzi.Hawasubiri karandinga bali huwekwa vile kwa ajili ya picha. Wakisha maliza waandishi ndio wanaondoka
Niliandika Wapenda sifa hapa JF au Waoga Wakafuta hoja! JF saa nyingine wanavuruga sana! I am really Frustrated! Jina langu lipo, na Nasemaga Nikisema kitu hapa JF nipo Tayari kushitakiwa, lakini wapo mamods wanahofu kwa niaba yangu!Paskali hajaandika vilema wale kula kipigo posta!
Inawezekana macho yako yanachagua cha kuona ila vingine huoni. Kwa kiasi gani kuna kundi inchi hii linadhalilishwa zaidi ya hao kama sio watanzania. Na haya ni madhara ya kuchua maafisa usalama wenye Zero form four.Dah! Nilifikiri ni mimi tu nimeliona, kutokana na muhemuko wa hili Jambo nikaona ngoja nikae kimya, ni kweli hao jamaa wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi lakini sikuona sababu yoyote ile ya kuwadharirisha, sasa walipiga magoti ili iweje??
Wanafiki katika ubora wenu. Wamechutama tu mnalialia na kuleta UZANDIKI hapa, Je wakipigwa mikwaju 12 wakati wanaingia na 12 wakati wa kutoka si ndio mtajitapakaza inyee mwili mzima.Nakubaliana na mtoa Mada. Jana nilimuona yule Mzee Rugemalira na Mwenzake Singh wakichuchuma kwa taabu sana. Singh alikosa nafasi ya kuchuchuma ilibidi Rugemalira asogee kidogo ili apate nafasi.Tusirudie vitendo kama hivi tena. Sisi wote ni binadamu. Leo kwako kesho kwa mwingine.