Kaka unasafilisha mali ya asili - Julius Nyerere International Airport -Yamenikuta ya ajabu na kweli

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Nasafiri kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport.
baada ya mabegi kupita kwenye scanner, begi moja likaonekana lina tatizo. Likaekwa pembeni, nikaitwa, mpekuzi akalifungua na kupekuwa akatoa pakiti ambayo ilikuwa na ubuyu, ule ubuyu wa rangi nyekundu ambao kwa sasa ni maarufu hapa Tanzania.

Mdada mpekuzi akautoa na kuniambia ,je hukuliwona bango pale nikasema sikuangalia kwani kila kitu ni kawaida nina vipakiti vya chipsi za muhogo, kipo kipakiti cha kolosho na vingine mastafeli mawili,yaani vijizawadi na vingine vyangu mwenyewe.

Dada akaluka na kudai hujui kuwa unasafilisha hazina ya Taifa ,nikamuuliza kwani dada shida ipo wapi ,mbona sikuelewi ?

Tumekamata hazina ya Taifa, unasafiisha mbegu za ubuyu kinyume cha sheliya ulitakiwa uwe na kibali toka mali ya asili.

Kwanza nilifurahi sana na kucheka na kumwambia kama unautaka nikuwachie ,na hivi hizo mbegu zitachukuwa miaka mingapi hadi kuleta mazao ? Na niambia kama kuna Mtanzania aliepanda mbegu za ubuyu tokea tupate uhuru ?
Na hii mibuyu mbona ipo kila sehemu na siku hizi tu ndio tumenza kusikia mtu akisema huu M'buyu wangu ,nikafoka na kubadilika rangi ,mweusi lakini niligeuka rangi na kuwa mwekundu.
baada ya watu kuanza kuuliza kuna nini dada akalifunga begi na kuniambia sawa safari njema ila usijaribu tena kupita na mali ya asili bila ya kibali.
Wengi waliosikia walisema ni dalili ya njaa hapa Tanzania.
 
Nasafiri kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport.
baada ya mabegi kupita kwenye scanner ,begi moja likaonekana lina tatizo.
Likaekwa pembeni ,nikaitwa ,mpekuzi akalifungua na kupekuwa akatoa pakiti ambayo ilikuwa na ubuyu,ule ubuyu wa rangi nyekundu ambao kwa sasa ni maarufu hapa Tanzania.

Mdada mpekuzi akautoa na kuniambia ,je hukuliwona bango pale nikasema ,sikuangalia kwani kila kitu ni kawaida nina vipakiti vya chipsi za muhogo ,kipo kipakiti cha kolosho na vingine mastafeli mawili,yaani vijizawadi na vingine vyangu mwenyewe.

Inawezekana wapo sawa.
Kwa kiasi fulani wapo sahihi kuzuia usafirishaji wa mbegu za mimea bila kibali hususani kwa safari za kimataifa. Kwa safari za ndani ya nchi sioni Kama Kuna tatizo.
Aidha, sababu ya kwamba wanazuia usafirishaji wa mbegu hizo eti kwa kuwa ni 'mali ya asili' Wala haina mashiko hata kidogo. Nchi zingine wanazuia usafirishaji wa mbegu za mazao kutokana na sababu za kiusalama, yaani ni katika kudhibiti usalama wa vyakula (Food Security and Quality Control)
 
Hizo zao ni akili za kijamaa na kishamba,
 
"nikamwambia kama unautaka nikuwachie ,na hivi hizo mbegu zitachukuwa miaka mingapi hadi kuleta mazao ? Na niambia kama kuna Mtanzania aliepanda mbegu za ubuyu tokea tupate uhuru ?
Na hii mibuyu mbona ipo kila sehemu na siku hizi tu ndio tumenza kusikia mtu akisema huu M'buyu wangu ,nikafoka na kubadilika rangi ,mweusi lakini niligeuka rangi na kuwa mwekundu."
 
Nasafiri kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport.
baada ya mabegi kupita kwenye scanner ,begi moja likaonekana lina tatizo.
Likaekwa pembeni ,nikaitwa ,mpekuzi akalifungua na kupekuwa akatoa pakiti ambayo ilikuwa na ubuyu,ule ubuyu wa rangi nyekundu ambao kwa sasa ni maarufu hapa Tanzania.

Mdada mpekuzi akautoa na kuniambia ,je hukuliwona bango pale nikasema ,sikuangalia kwani kila kitu ni kawaida nina vipakiti vya chipsi za muhogo ,kipo kipakiti cha kolosho na vingine mastafeli mawili,yaani vijizawadi na vingine vyangu mwenyewe.

Dada akaluka na kudai hujui kuwa unasafilisha hazina ya Taifa ,nikamuuliza kwani dada shida ipo wapi ,mbona sikuelewi ?

Tumekamata hazina ya Taifa, unasafiisha mbegu za ubuyu kinyume cha sheliya ulitakiwa uwe na kibali toka mali ya asili.

Kwanza nilifurahi sana na kucheka na kumwambia kama unautaka nikuwachie ,na hivi hizo mbegu zitachukuwa miaka mingapi hadi kuleta mazao ? Na niambia kama kuna Mtanzania aliepanda mbegu za ubuyu tokea tupate uhuru ?
Na hii mibuyu mbona ipo kila sehemu na siku hizi tu ndio tumenza kusikia mtu akisema huu M'buyu wangu ,nikafoka na kubadilika rangi ,mweusi lakini niligeuka rangi na kuwa mwekundu.
baada ya watu kuanza kuuliza kuna nini dada akalifunga begi na kuniambia sawa safari njema ila usijaribu tena kupita na mali ya asili bila ya kibali.
Wengi waliosikia walisema ni dalili ya njaa hapa Tanzania.
Kwa kweli wewe umejitetea kihekima sana na umempsha huyo dada.Lazima aliona haya kwa wenzake.
Ni kweli watanzania hakuna aliyewahi kupanda mbuyu.Na kama ulikuwa unakwenda Ulaya wala hizo mbegu za ubuyu hazioti huko.
Kwa kifupi sisi watanzania katika biashara na safari za kimataifa tuna vituko sana ndio maana hatuonekani sana huko nje kuliko majirani zetu.
Karibuni hivi mimi nilibeba mti mzima mzima kwenye mfuko nikaweka kwenye begi na tena huo mti huko kwao ni mali sana lakini hawakunizuia kupita nao uwanja wa ndege.
 
Kwa kiasi fulani wapo sahihi kuzuia usafirishaji wa mbegu za mimea bila kibali hususani kwa safari za kimataifa. Kwa safari za ndani ya nchi sioni Kama Kuna tatizo.
Aidha, sababu ya kwamba wanazuia usafirishaji wa mbegu hizo eti kwa kuwa ni 'mali ya asili' Wala haina mashiko hata kidogo. Nchi zingine wanazuia usafirishaji wa mbegu za mazao kutokana na sababu za kiusalama, yaani ni katika kudhibiti usalama wa vyakula (Food Security and Quality Control)
Tusiwe tunapoteza muda kwa mambo ya hovyo, kama tumeshindwa kuzuia madini ndio tuje tukomae na mbegu za mibuyu? nchi nyingi za Afrika zina mibuyu na wala haiwasadii chochote.
 
Bado niko hapa nawaza ni sheliya gani inakataza mtu kusafiri na ubuyu
Mungu ni wa wote, yaani hata l na r hujui ila upo unapaa, hongera mjukuu.

Mwambie avipeleke maabara ila ni kama kuna kitu umeficha
Kimsingi katika nchi nyingi sana usafirishaji wa vyakula au mbegu za mazao kwenye ndege za abiria bila vibali hairuhusiwi kisheria. Wanakataza kutokana na sababu za kiusalama, hata kupanda kwenye ndege ukiwa na chupa ya maji ya kunywa sometimes pia huwa hawaruhusu.
 
Kwa kweli wewe umejitetea kihekima sana na umempsha huyo dada.Lazima aliona haya kwa wenzake.
Ni kweli watanzania hakuna aliyewahi kupanda mbuyu.Na kama ulikuwa unakwenda Ulaya wala hizo mbegu za ubuyu hazioti huko.
Kwa kifupi sisi watanzania katika biashara na safari za kimataifa tuna vituko sana ndio maana hatuonekani sana huko nje kuliko majirani zetu.
Karibuni hivi mimi nilibeba mti mzima mzima kwenye mfuko nikaweka kwenye begi na tena huo mti huko kwao ni mali sana lakini hawakunizuia kupita nao uwanja wa ndege.
Wakati huohuo TWIGA walipitishwa hapo hapo JKNIA kwa kupandishwa ndege na kusafirishwa nje, ila hatusikii wakikamata wasafirishaji wa hizo nyara muhimu za serikali, nchi ina vituko sana hii.
 
Back
Top Bottom