John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Abiria huyo anapaswa kunyang'anywa mbegu hizo alizobeba, wala siyo kumkamata na kumuweka kizuizini na kufungwa jela.Kuingiza ya kutoa mbegu nchini bila kibali ni kosa kisheria. Rejea Sheria ya mbegu ya mwaka 2003. Ni sio Tanzania tu nchi nyingi Dunia zinakataza kuingiza au kutoa mbegu bila kibali kulinda mimea yake dhidi ya magonjwa na issue nyingine. Usichukulie kirahisi hivyo.
Maelezo yangu yako very clear, aidha, maelezo hayo ni kutokana na uzoefu wangu binafsi katika maisha halisi kuhusiana na suala hili.
Je, Sheria hiyo ya Mbegu uliyonukuu au Kanuni zake zinaainisha kuwa kubeba mbegu za mazao bila kibali ni kosa la aina gani? Ni jinai?? Na, Je, Sheria hiyo imetaja adhabu gani? Adhabu ya Kifungo gerezani???
Rudia tena kusoma vizuri hiyo comment yangu kama haujaelewa vizuri suala hili.
Suala la kubeba mbegu za mazao kwenye ndege za abiria siyo kosa linaloangukia kwenye katazo la "Strictly Prohibited Items," hivyo abiria yuko subjected kupata adhabu mbadala ya kunyang'anywa mbegu hizo alizobeba na Kisha zikateketezwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Uwanja wa ndege, wala siyo kufungwa jela/ gerezani.
Aidha, usiwe unajikita kwenye nadharia (theories only) zilizopo kwenye vitabu vya Sheria, jaribu kupata uzoefu halisi kwa vitendo ili uelewe vizuri zaidi kuhusiana na Hoja husika.