Kaka unasafilisha mali ya asili - Julius Nyerere International Airport -Yamenikuta ya ajabu na kweli

Kaka unasafilisha mali ya asili - Julius Nyerere International Airport -Yamenikuta ya ajabu na kweli

Kuingiza ya kutoa mbegu nchini bila kibali ni kosa kisheria. Rejea Sheria ya mbegu ya mwaka 2003. Ni sio Tanzania tu nchi nyingi Dunia zinakataza kuingiza au kutoa mbegu bila kibali kulinda mimea yake dhidi ya magonjwa na issue nyingine. Usichukulie kirahisi hivyo.
Abiria huyo anapaswa kunyang'anywa mbegu hizo alizobeba, wala siyo kumkamata na kumuweka kizuizini na kufungwa jela.

Maelezo yangu yako very clear, aidha, maelezo hayo ni kutokana na uzoefu wangu binafsi katika maisha halisi kuhusiana na suala hili.

Je, Sheria hiyo ya Mbegu uliyonukuu au Kanuni zake zinaainisha kuwa kubeba mbegu za mazao bila kibali ni kosa la aina gani? Ni jinai?? Na, Je, Sheria hiyo imetaja adhabu gani? Adhabu ya Kifungo gerezani???

Rudia tena kusoma vizuri hiyo comment yangu kama haujaelewa vizuri suala hili.

Suala la kubeba mbegu za mazao kwenye ndege za abiria siyo kosa linaloangukia kwenye katazo la "Strictly Prohibited Items," hivyo abiria yuko subjected kupata adhabu mbadala ya kunyang'anywa mbegu hizo alizobeba na Kisha zikateketezwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Uwanja wa ndege, wala siyo kufungwa jela/ gerezani.

Aidha, usiwe unajikita kwenye nadharia (theories only) zilizopo kwenye vitabu vya Sheria, jaribu kupata uzoefu halisi kwa vitendo ili uelewe vizuri zaidi kuhusiana na Hoja husika.
 
Abiria huyo anapaswa kunyang'anywa mbegu hizo alizobeba, wala siyo kumkamata na kumuweka kizuizini na kufungwa jela
Ignorantia juris non excusat.


Suala la kubeba mbegu za mazao kwenye ndege za abiria siyo kosa linaloangukia kwenye katazo la "Strictly Prohibited Items
Makatazo (Prohibition or strictly prohibition) kanuni, miongozo,taratibu misingi yake yote ni Sheria za nchi. Sheria ndio inayoweka kanuni, makatazo na miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa hizo Sheria.
Kisha zikateketezwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Uwanja wa ndege, wala siyo kufungwa jela/ gerezani.

Aidha, usiwe unajikita kwenye nadharia (theories only
Unazungumzia uzoefu wako wa viwanja vya ndege vya ndani ambavyo maofisa wanaokuwa pale ni uhamiaji na polisi ( mara chache). Kwa viwanja vya kimataifa hasa mataifa makubwa kunakuwa na Kila aina ya Kada na idara ambapo zipo pale kusimamia Sheria za nchi husika na hasa kwenye usafirishaji haramu wa mimea,mazao ya baharini yaliyopigwa marufuku,wanyama,bidhaa hatarishi n.k i

Usijekuwa umesafiri na ndege toka Dar kwenda Mwanza ukasema umepata uzoefu! Yes hata Mimi nakumbuka nilipita na samaki wakamuona nikaishia kuwa mlalamishi wakaniruhusu (ambapo pia ni weakness kwa walinzi wetu wa usalama) lakini pia ni domestic flight haikuwa na madhara.
Kisha zikateketezwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Uwanja wa ndege, wala siyo kufungwa jela/ gerezani
Yes baadhi ya vitu vinateketezwa kwa lengo la kuzuia madhara kwa nchi husika. Kwa upande wa mimea na mbegu nchi nyingi hazitaki kuingiza species nyingine tofauti kwa kuhofia invasive species kwa uoto wao.
 
Back
Top Bottom