Mbunge wa Geita na Katibu Mwenezi wa TANU alimkosoa Nyerere mwaka wa 67 kuhusu Azimio la Arusha.
Lakini hakuuliwa. Alifukuzwa chama na ubunge. Na wakawaambia waajiri wote, mpaka Kenya, wasimpe kazi. Akakaa kijijini anafuga ng'ombe. Alisoma Tabora School na shahada ya Uandishi Marekani.
Walikuwa hawauliwi. Angalau hakuuliwa.
Japo unaweza kusema Nyerere ndio alipanda mbegu za kumfanya mtu adui wa utawala anapokuwa na mawazo tofauti na mfumo.
Lakini pia na kuvunja nguvu ya utawala wa sheria. Alidhoofisha utawala wa sheria ili atawale kwa fikra na emotions zake yeye. Mtu hajaibia mwajiri, huna kesi nae yeyote kisheria, lakini unam punish kwa kuamuri asiajiliwe popote East Africa. Kisa, Mwenezi kakataa kueneza Azimio la Arusha. Liko wapi leo hilo Azimio ?