Mtoa mada usitake kutuhamisha goli.
Binafsi natembea Sana usiku, na Mara kibao nishakamtwa na hao hao sungusungu usiku wa manane.
Ila sijawai dhurika kwa namna moja ama nyingine.
Nnachokifahamu ktk operation zao usiku hutembea na viongozi kadhaa wa mtaa.
Wakishakukamata,
Hawa viongozi wa mtaa wanakuhoji wewe Ni Nani, unaishi wapi, unafanya shughuli gan, unaelekea wapi, unatoka wapi.
(Ukiwa ni mtu mwema kwny jamii na huna historia ya uhalifu, hakuna anayehangaika na wewe)
Ayo unayosema Kwamba wamemvamia tu na ghafla kuanza kumchoma TU kibiriti hayawezekani kabisa.
Vinginevyo uyo ndugu yenu ana historia ya uhalifu hapo kabla.
Na Kama Ni suala la uhalifu,
Hapo ninyi Kama ndugu Kuna namna mmefeli kwny suala Zima la malezi[emoji4]
Nchi haiwezi kuendelea kwa kukumbatia wezi na vibaka wanaoishi kwa kutegemea utelezi wa jasho la watu.
Wezi na Vibaka wanaorudisha maendeleo ya watu nyuma, na wanapaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote.