Kaka zetu, hayo mabegi ni vipi kwani?

Joannah tatizo ni kwa hawa walioiga tuu bila kujua biaowang, marcello na ponasoo ni kwa ajili ya kubeba tools na equipments kwa ajili ya shughuli za hapa na pale ila hawa wa ofisini sikuizi kuna vi bag vya leather one hand vinawafaa sana muhimu ni kuchagua bag kulingana na kazi,mazingira pamoja na shuhuli husika NB:Mi nnazo zote Biaowang na hivi vi bag vya leather
 
Exactly!na hicho ndicho ninachokizungumzia hapa.... sio wasibebe mabegi Bali wabebe hivyo vya lether watapendeza kulingana na outfits walizovaa
 
Mabebi hayo bado mimi kuyaona
 
mtuache na mabegi yetu,hata kama tukipata vibyongo ,migongo yenu !!? mtuache !!!
 
Unataka tukiwa tunaenda site sie mafundi tuweke vitu kwenye mfuko wa cement? Mabegi ya pima maji, kamba ya kupimia, konobao, timanzi na MAFUTA YA MGANDO.


Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Mabag yenyewe si ndo haya??
Maisha yana mambo mengi, tangu niligundue hili siwezi kumjudge mtu kwa muonekano wake, kwa kile alichokivaa ama kukibeba.

Ingawa sio muumini wa hizi bags lakini hili halinifanyi kumchukualia niaje mbebaji.

Kumbuka ukipendacho wewe mwenzio hakipendi, akipendacho mwenzio wewe hukipendi.
 
tafadhal ukiwaona tena jarib kuwakaguw alafu uje na sisi utwambie ulikuta wamebeba nini either makarats au PC.
"(KAMBI POPTE HAO)
 
tafadhal ukiwaona tena jarib kuwakaguw alafu uje na sisi utwambie ulikuta wamebeba nini either makarats au PC.
"(KAMBI POPTE HAO)
Ha haaa!Lengo lako Nini haswa?niteguliwe nyonga?acha watueleze hapahapa
 
Mwambie huyo mmoja unaemmiliki basi inatosha
Yaani kila mwanaume awe na muonekano unaoutaka wewe kwani unataka kuwamiliki wote
 
Tuache...
Jiulize kwa wingi wa mabank hapa dsm, ushawa ona mfanyakaz wa bank kapanda daladala?? Au unahisi wote wana magari?
Ndo tunaweka humo uniform haaa haaa
 
Kuelewa nini mwanamke anataka ni kazi sana.
Wito kwa wanaume wenzangu,tuishini kama tupendavyo sisi jamani,tusipangiwe😂😂
 
Jamani najua mko poa!

Hivi siku hizi kila kaka huku mjini naona kabeba begi mgongoni,

Hata D knob anasema "Enzi za kubeba begi mgongoni na slang za Kinyamwezi"

Enzi nawabana "kete" pale Buzuruga begi nimeweka shada,matchbox,gaslighter,mikasi,sanda,mkate ,juisi, maji na mazaga shazi. Kama hunijui utahisi nasafiri kumbe nina biashara zangu,

Yaone tu hivo hayo mabegi, Yanatufichia siri sana wajuba.
 
Kama nanyi mnavyokuwa na mabegi makuubwa hayana nauri yamejaa tissue tu.
Nakazia ......na michupi yao ya jero jero mikubwaaa kama bukta ya mkude........na bado zile tight zao ni shida.....utadhani anataka kujiumba upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…