Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Mwenye matatizo ni wewe, umeshindwa kumshauri, atafute mwanaume mwenye mtoto mechi ianze me 1- 1 ke, kama baba wa mtoto anamke wake tayari kwa nini hakumuoa mdogo wako? Au ndo ile unaenda sokoni unabonyeza maparachichi alafu huchukui unaenda kununua maembe.
 
Hivi hili swala singo faza huwa haliwahusu eeh

mtoto sikuzote ni wa mama yan hata awe mkubwa vip[emoji16][emoji16] yani anaeteseka from dusk till dawn ni mama.... baba labda ayakubali majukumu hapo ndo utaona mahangaiko ya baba ila akiamua kukimbia mzigo ni wa mwanamke mpaka atakapokufa[emoji2356][emoji2356]
 
Mwanamke; Kama unataka kuolewa, peleka mtoto kwa baba yake (miaka mitano si mbaya), kama hamtaki kata mawasiliano nae kabisa mpambanie mtoto wako.

Katika mahusiano mapya usitoe historia yako ya mahusiano ya nyuma kwa bwana mpya, au sema kwa ufupi sio unamwambia kuwa mpaka hapo yeye ni mwanaume wa 7 kwako ndani ya mwaka mmoja!

Kuwa makini, epuka kutapeliwa
Hizo body counts hamnaga mwanaume hataki kujua iko wazi atadanganya kwa kusema watatu au wawili ila akili kumkichwa watu ni FIAT za Magereza
 
Mdogo wako aluchumbiwa na mvulana na ametoswa kisa kazaa.

Mwambie tu mdogo wako aache kufukuzia wavulana maana hawana moyo wa kuishi na mwanamke aliyezaa.

Mwambie afukuzie wanaume watu wazima wenye akili hao huwa hawamkatai mwanamke eti kisa ana mtoto.

asikimbize wanaume kabisa kama bahati yake ipo ipo tuu hana haja ya kuhangaika yani.. Wote tunamwomba MUNGU mmoja sio kila mtuu hawapendi singo maza kikubwa ajipende na kujikubali tuu afu awe bize na maisha yake[emoji4][emoji4] ampende mwanae basi


NB: dear ladies wanaume hawatafutwi wao ndo wanatafuta tujipe furaha tu afu tutafute hela[emoji4][emoji4]
 
Na wew utalea mtoto asie wako ndani ya ndoa Kuna fala atamjaza mimba mkeo na utalea vilevile Nyie mmeumbiwa hivo pia
Kuna mabint wawili are so good, wanalea watoto wadogo sasa hivi, mmoja analea wa kwangu, mwingine analea wa jamaa. Kama una kaka yako unaweza ukani PM nimuunganishe na mmoja wao ili aoe, ni wasichana fulani amazing na ni wife materials.

Hizo za kugongewa endelea ku wish hivyohivyo, wengine sisi tunaishi kwa makusudi.
 
Kwa wanaume hali ni tofauti, ila kama mnataka na hili mjiringanishe karibuni. Kwani sisi tuna noma basi? Sisi hatutaacha kuzalisha.
Sisi mkikaa sawa tunawapiga mimba tunateleza, kuna mafala ndiyo wameumbwa kwa ajili ya kutulelea watoto wakati sisi tunaishi.
Kwenye maisha haya hakuna mkamilifu huenda ndio kubwa kulifanya msipende kuhukumu watu Kwa mapito Yao kheri wao wamepata watoto hawakupata ukimwi
 
Kwenye maisha haya hakuna mkamilifu huenda ndio kubwa kulifanya msipende kuhukumu watu Kwa mapito Yao kheri wao wamepata watoto hawakupata ukimwi
Standards ni muhimu sana zizingatiwe. Kufeli shule siyo kufeli maisha.
Ila si sahihi, na ni kituko kwa aliyefeli shule kulazimisha kazi zinazohitaji wenye shule/elimu. Akubaliane na hali yake, mbona tunawaheshimu sana waliokubaliana na matokeo?
 
Huwa nawafikiria single father's kwakweli na mm natak nione makaburi ya wanawake mlozaa nao [emoji3]
Upo sahihi kabisa. Hili tatizo si la upnde mmoja tu. Hivi vijogoo vinavyozalisha ovyo ovyo hivi tabu sana. Unamkuta binti ana 20 yrs ila tayari ni single mother. Aisee inaumiza sana.

Na wanawake anzeni kukataa kuolewa na single fathers.

Mm ni Me
 
Kwa wanaume hali ni tofauti, ila kama mnataka na hili mjiringanishe karibuni. Kwani sisi tuna noma basi? Sisi hatutaacha kuzalisha.
Sisi mkikaa sawa tunawapiga mimba tunateleza, kuna mafala ndiyo wameumbwa kwa ajili ya kutulelea watoto wakati sisi tunaishi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aiseeee kuna watu wana mitazamo ya kiwaki kinoma[emoji1787][emoji174][emoji174] aloooh make sure ukizaa mtoto wa kike asiwe fala ambae ameumbwa kuja kuwaletea watu watoto wakati hao watu wanaishi[emoji6][emoji6]
 
NB: dear ladies wanaume hawatafutwi wao ndo wanatafuta tujipe furaha tu afu tutafute hela
emoji4.png
emoji4.png
Ni kweli tunatafuta na sio kutafutwa, umeongea point kabisa.
 
Back
Top Bottom