Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Ni kweli na bila shaka angalifanya hivi:Kwenye ishu ya Corona wakati dunia nzima ikijifungia na kufata njia isiyo sahihi kushughulika na janga lile.
Baba yetu Magufuli alisimama kama kiongozi akaja na njia ambayo dunia nzima sasa inaifata kwenye kukabiliana na corona.
Naamini hata kwenye hii ishu ya mafuta, Magufuli angekuja na njia sahihi ya kusaidia watu wake wasiteseke na ugumu wa maisha unaosababishwa na gharama za mafuta kuwa juu. Angetafuta njia sahihi za kumlinda mwananchi asiumizwe na kupanda kwa bei za mafuta
Magufuli alikuwa na maono sana na aliwapenda watu wake hakutaka kuona wanateseka. Angetuvusha.
1. Angejenga oil refinery kubwa ambalo lingalitosheleza mahitaji yetu na nchi jirani ambao tungaliwauzia. Hii ingalipunguza sana bei ya mafuta kwani badala ya kununua refined oil tungalinunua crude oil, including ile ya itakayotoka Uganda.
2. Mafuta ambayo yalishagunduliwa kuwepo Tanzania, kwa kushirikiana na wale watalaam wa Museveni, yangalianza kuchimbwa mara moja.
3. Katika kipindi hiki cha vita ya Russia vs Ukraine ambayo imesababisha mafuta kutoka Saudi Arabia na OPEC kupanda sana bei na yale ya kutoka Russia kushuka sana bei, tungalinunua kutoka Russia bila woga wo wote hata kama ni kwa rubles. Russia ni marafiki zetu na tungaliimarisha biashara kati yetu. China na India ambayo ni mataifa makubwa yenye watu billioni tatu, yanafanya hivyo.
4. Tungalipunguza idadi ya tozo za serikali kutoka idadi ya tozo 15 za sasa na kubaki na tatu tu za VAT, Tanroad na Tarura. Mapungufu ya bajeti ya serikali yatakayotokana na kupunguzwa kwa tozo hizi, yangalifidiwa kwa kubana sana matumizi ya serikali yasiyo ya lazima hususani safari za ndani na nje ya nchi, washa, semina na posho zisizokuwa za msingi eg seating allowance (posho ya kukaa) n.k.