Kama bado haujafanya maamuzi ya kutulia na mwanaume ulienae/anaekutongoza basi usile hela zake

Kama bado haujafanya maamuzi ya kutulia na mwanaume ulienae/anaekutongoza basi usile hela zake

Kwa Kizazi hiki cha sasa 96% ya wanawake ndio wapo hivyo na ndio hao unaowasemanga.

4% waliobaki ndio hao unaowafagilia mtoa mada. Hawa walikuwepo miaka ya kitambo sana, sasahivi wanaelekea kutoweka. Japo kidogo unaweza kuwabahatisha huko kwenye nyumba za ibada na vijijini.

Ndio maana sikuhizi Ndoa zinasambaratika sana. Kuna uhaba sana wa kupata wife material. Staili ya maisha imebadilika sana
 
Tatizo mtoa mada unazungumzia wanawake walioangamia Kwenye Vita ya Kwanza na ya pili ya Dunia.

Hawa wa siku hizi wote Ni kausha damu tu ndo maana tunagonga tu na kusepa ili kukwepa gharama
mkuu nayajua yote hayo naona kila kitu kinachoendelea mtaani. Siku hizi visa vya kufanyiana ukatili na malalamiko vimekua vingi ukiangalia sababu ni nini unaona ni wahusika wenyewe tangu mwanzo walikosea kufanya maamuzi au kukubaliana uhusiano wao utaenda vipi, kwamba ni meaningful relationahip au wanauziana tu mahaba. Unakuta kijana kapalamia slay queen baada ya kuelemewa na gharama za ku-maintain penzi anaanza kulalamika wanawake wanapenda hela, unakuta binti kajiweka kwa bad boy baada ya kuachwa singo maza anasema wanaume wote ni mbwa. Mwanamke unajua kabisa jasho la mtu haliliwi bure kivipi unakua na matarajio ya kula hela ya mtu na kupotea kirahisi rahisi tu. Ukiangalia visa vingi unaona ni matokeo ambayo yaliandaliwa na wahusika wenyewe tangu mwanzo.
 
Tafuteni mabinti wa kishua, mboga 7, hawa wengine achaneni nao kbsaa.
Hata wa kishua kama hajielewi nae anaangukia kwenye kundi la hawa hawa kausha damu, kuna wanawake wana ajira za kutosheleza mahitaji yao na bado wanataka na hela za mwanaume, Inaonekana hii trend ya kula hela za wanaume imekua kama fashion vile
 
mkuu nazungumzia wale mabinti wa madoni, eg watoto waliosoma ma feza schools huko, ivi ukipata wa aina ile ana kuelewa mtasumbuana ?, sidhani.
 
Kuanzia unapotongoza mwanamke anakubebesha gharama zote ambazo alitakiwa kuwajibika mwenyewe au kugharamiwa na baba yake sasa hapa mwanaume akisalitiwa ndio yale yale ya msukuma na penny uko goba

Imefika hatua hauwezi kutofautisha kati mke, mpenzi na kahaba maana along the way wote watataka hela kama nguzo ya hayo mahusiano, hakuna pesa hakuna mapenzi.

Dada angu unataka pesa au matunzo kutoka kwa mwanaume tambua ya kwamba unauza uhuru, uko mbeleni ukichepuka au kutaka muachane iyo lazima italeta shida.

Hakuna mwanaume atataka kukutawala ikiwa hajawahi kuingia gharama ya hata shilingi 1 kwa ajiri yako, kama bado haujafanya maamuzi ya kutulia na mwanaume uliyenae siku zote za maisha yako basi usile hela zake.

NB: Kama unajiuza weka wazi pale pale unapotongozwa mkubaliane bei then baada ya tendo hakuna kugandana wala kubebeshana gharama zozote.
Dah 😹😹
 
mkuu nazungumzia wale mabinti wa madoni, eg watoto waliosoma ma feza schools huko, ivi ukipata wa aina ile ana kuelewa mtasumbuana ?, sidhani.
Kwenye kipengele cha hela uwezekano wa kusumbuana ni mdogo sana maana izo iphone, shopping za nguo, kula KFC n.k ni mambo yapo ndani ya uwezo wake na ashayazoea tangu akiwa mdogo.
 
Kwenye kipengele cha hela uwezekano wa kusumbuana ni mdogo sana maana izo iphone, shopping za nguo, kula KFC n.k ni mambo yapo ndani ya uwezo wake na ashayazoea tangu akiwa mdogo.
bora wa hivi, ila sasa u wife material sijui.
 
bora wa hivi, ila sasa u wife material sijui.
U-wife material unategemea na malezi aliyokulia lakini kama unataka mwanamke ambaye yupo huru kifedha basi unatakiwa kupotezea kidogo suala la uyo mwanamke kuwa submissive sana kwako.

Nb: Potezea ila isifike hatua ya kukubali mwanamke akupande kichwani
 
Back
Top Bottom