Kama bado unakaa kwenu usitoke, Maisha yapo juu sana kila kitu kimepanda

Hili ndilo limeleta matatizo ya urithi nyumbani kwetu. Mwaka 2007 kaka yangu alikuwa ameshamaliza chuo lakini alikuwa anazagaa zagaa tu nyumbani.

Hataki kuhama japokuwa alikuwa amekwisha wezeshwa kiuchumi. Baba akatufukuza nyumbani 'kidiplomasia'. By that time baba alikuwa anajenga dispensary.

Alikuwa amekwishajenga nyumba ya dk, nurse na jengo la dispensary na majengo mengine.

Mimi baba aliniambia kuwa nisomee udaktari ili anirithishe hospital. Means alinichagua kuwa mrithi wa hospitali.

But baada ya kufukuzwa hom, kaka yangu alipewa nyumba ya daktari akakae, then mdogo wangu naye akasema naye hataki kukaa home, basi naye akapewa nyumba ya nurse akakae.

Baba alipofariki, mama akasema kuwa ile estate tumemilikishwa wote. Ila kwa kuwa baba alisha ascertain nini cha kurithi kwenye ile estate kt ya kaka na mdogo wangu; mimi nikasema, wacha for a mean time mama aendelee kuhemea hapo.

But in her absence hawa siblings vichwani mwao wameweka equal ownership. Hapa nawaza nawezaje kuwachomoa bila kuvunja undugu ili kila mtu abaki na kile alichogawiwa kwenye hii estate?
Wataalam hapa mnisaidie...
 
Chuo gani hiki Kinafundisha Uandishi huu! Mnatukera sana baba zenu humu Hamjui tu...
 
Reactions: EEX
Hujaeleweka bado, kama hao ndugu zako wanaona wana equal share kwenye Mali alizoacha baba yenu kwa nini usiungane nao? Hata Kama baba ako alikusomesha u Dr kwa nini wewe ufikirie ndio una haki ya ku own hiyo Mali?
 
Hujaeleweka bado,Kama hao ndugu zako wanaona wana equal share kwenye Mali alizoacha baba yenu kwa nini usiungane nao? Hata Kama baba ako alikusomesha u Dr kwa nini wewe ufikirie ndio una haki ya ku own iyo Mali?
Huyu kaka alishapewa nyumba ya dk. But in the end, atataka na majengo mengine ambayo hakupewa.
Na huyu dogo alishapewa nyumba ya nesi. But in the end mama akidondoka naye atadai majengo mengine ambayo hakupewa.
Sasa hapa nataka kaka aridhike na nyumba ya dk ambayo alipewa akaishi na kuijengea fensi asidai majengo/ eneo jingine. Vile vile huyu dogo aridhike na nyumba ya nurse asidai eneo/ majengo mengine ambayo ni mengi na yanadondokea kwangu.

====
By the way, sikusoma udaktari. Nilienda kusoma vitu vingine kabisa.
 

Naomba niseme una wivu kama sio tamaa wewe pia ile sio mali yako ni mali ya baba yenu. Kwa nini unataka kuwaondoa ili ujimilikishe hiyo dispensary kisa mzee wako alikuomba usomee udaktari. Kwa nini usiwaachie hapo ukaenda kujenga yako wewe isiyokuwa na migogoro.
 
Hawa ndugu kila mmoja alishapewa mali zingine ambazo kwa thamani zinalingana na hii estate. Yaani ni kama wao wamenivamia kwenye mali yangu. Sina tamaa na mali ya urithi ila kuikana sehemu inayoniangukia ni kama kuwakana wazazi walionileta Duniani.

Pia kuwaruhusu ndugu wachukue mali yangu ni sawa na kuchezea urithi wa wanangu.
Mwanzo nilipanga kujitoa mazima. But on a second thought nikaona kuwa nafanya kitu kibaya.

Pia kuanza mwanzo sio mchezo. Kupata hilo eneo kwa sasa inabidi uwe na milioni mia plus!
Sisi tulipewa bure na serikali mwaka 2,000.
Enzi hizo yalikuwa ni mapori ambapo majambazi walikuwa wanajificha.
Nilikuwa nikienda mimi na baba kwa kutumia usafiri wa baiskeli ya Phoenix huku tukiwa tumejihami kwa kubeba mapanga makali!

Miaka 22 imepita tangu tupate hilo eneo. Kwa sasa kupata eneo kama hilo mjini ni ndoto
 

Sasa tutaondoka lini kama tunaogopa maisha kila siku
 
Familia nyingine unabebwa tu ukiwa hauna kazi ukipata unalipia chumba au kama vipi uhame na hakuna kuolea hapo ukitaka kuoa kapange huko! Hao wanaokaa bure hongera yao but wasibweteke!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…