Kama Barua yenu kwa Spika Ndugai imeitwa 'Kipeperushi' mkienda kukutana na Rais Samia angalieni tu asiwaite 'Wapuuzi' pia

Kama Barua yenu kwa Spika Ndugai imeitwa 'Kipeperushi' mkienda kukutana na Rais Samia angalieni tu asiwaite 'Wapuuzi' pia

Genta bwana una superioty complex sijui huko unakoishi unakaa na vilaza then wewe ndio unajiona una akili sana.😅😅
" Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer " GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE.
 
..tatizo sio viongozi wa Cdm.

..tatizo ni kwamba wako baadhi ya watu wako juu ya sheria.

..sheria nchi hii ina-apply kwa baadhi, wakati wengine hawaguswi.
Mkuu Joka, kuna sehemu tatu za suala la Spika na Team Halima

1. Kwa wenye kumbu kumbu, Spika Mkwawa, Msekwa, Mang'enya, Sitta walikuwa na kauli za kiutu uzima

Kwa miaka ya karibuni na hasa mitano iliyopita kumekuwa na kauli za indhara na karaha kutoka kwenye kiti kile kile cha akina Mkwawa na Sitta .

2. Haihitaji ujuzi wa sheria kujua kwamba anachofanya Spika ni uvunjaji wa sheria.

Akiwa mkuu wa mhimili unaotunga sheria hili nalo linakera sana.

Mbunge akifukuzwa na chama chake kama ilivyokuwa kwa Sophia Simba automatic anapoteza Ubunge.
Ndivyo ilivyotokea siku zote, leo kwanini kwa Team Halima sheria ivurugwe na Spika?

3. Chadema kuna tatizo la kushughulikia Halima na Wenzake.
Siyo kazi ya Chadema kuamuru au kutaka wafukuzwe Bungeni.

Sheria ndiyo inayotaka hivyo na wala si wajibu wa Chadema kuiongelea , ni hisani tu.

Wanachotakiwa Chadema ni kumtaka Spika, na kwavile kuna barua na ushahidi , basi kupitia Mwanasheria wao amwandikie Spika akimtaka asitise kutumia jina la Chadema kwa wabunge hao, na kwamba wasihusishwe kwa jina au chochote kile. Na kwamba, ikitokea hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwemo kutafuta tafsiri ya mahakama

Chadema wanaweza kwenda mahakamani, si kutaka wafukuzwe Bungeni bali kuwataka Wabunge hao, Spika na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutohusisha, jina au shughuli zozote zile za chama na hao Wabunge. Hilo tu !

4. Si suala la Chadema kupinga uwepo wa Wabunge, bali ni suala la Walipa kodi kumtaka Spika asitishe malipo kwavile kufanya hivyo ni malipo yasiyo halali kama findings zingine katika audit.

Hili jamani si suala la Chadema, ni suala la wananchi kuhakikisha sheria zinafuatwa na kwamba hakuna abuse ya sheria zinazotuongoza wala hakuna aliye juu yake na kwamba, kodi zetu zinatumika kwa mujibu wa sheria zilizopo na si mtu au watu.

Hapa ndipo Watanzania wanatakiwa waamke, kodi zinazowalipa hao Wabunge si za Chadema ni za kwako wewe, mimi na yule.

Pascal Mayalla Ngongo
 
Wamegomea katiba mpya, wamegomea tume huru ya uchaguzi, huko mbeleni naona kutaibuka makundi ya kigaidi, yataanza mdogo mdogo, Kama vikundi vya kidini, lakini vikibeba madai ya kisiasa.
CCM haitoki madarakani kilaini
CHADEMA mkiwa madarakani mtatuletea Katiba au mnaongeongea tu
 
Kwa aina ya Uzungumzaji ule wa Spika Ndugai na ukiiangalia na 'body language' yake ( tena huku akijiamini kabisa ) tusifichane hapa ni lazima tu kutakuwa na Shida Kubwa ya 'Kiutendaji' kwa CHADEMA ila 'inafichwa' ama 'inafunikwa' tu kwa Mgongo wa Mapungufu ya Serikali na Chama Tawala chake cha CCM.
Hapa ndio naona pointi muhimu.

Chukulia mfano huu.

Mdee na jirani yake Mbowe wanagombania shamba.

Mbowe amekwenda mahakamani, na mahakama imetoa hukumu kwamba mdee hana haki katika shamba huisika.

Lakini, Mdee amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Baada ya rufaa hiyo kukatwa, Mbowe hawezi kuingia katika shamba linalobishaniwa na kuanza kulima wakati rufaa haijaamuliwa.

Katika mfano huu, uanachama wa wanaoitwa covid19 ndio shamba linagombaniwa.

Wamekata rufaa.

Kitendo cha Chadema kuandika barua kwa Spika wakitaka awatimue ni sawa na kuingia kwenye shamba lililokatiwa rufaa na kuanza kulima.

Lakini, baadhi ya viongozi wa Chadema hawaoni umantiki huu.

Sio sawa.

Kwa hiyo, mpaka hapo Spika Ndugai yuko upande sahihi, Chadema wako upande wa makosa.

Nashangaa hata mshauri wa kiroho wa Mbowe, ambaye ni PhD holder haoni ukweli huu.

Meseji zake anazozisambaza katika mitandao ya whatsapp zinathibitisha hitimisho hili.

Nimeona meseji moja yenye kicha cha maneno "NENO HUJITETEA" ambayo imesindikizwa na picha ya kuku jike aliyeatamia "vifaranga wawili wenye sura ya paka."

1620159651669.png


Maelezo yake ni haya:

....Walitekwa wakapelekwa nchi ya kigeni. Wakalazimishwa kuimba nyimbo za sifa katika nchi ya kigeni.
(Zaburi 137: 1-6).

......Hakutekwa, alikwenda mwenyewe uhamishoni.
Hakulazimishwa kuimba nyimbo za sifa akiwa ugenini.
Hakuikumbuka Sayuni akiwa ugenini.
Daima alikumbuka masufuria ya nyama aliyozoea kula katika himaya ya utumwa wa Farao. Akatamani nyama za kusaza nyumbani kwa baba yake kama mwana mpotevu (Kutoka 16:3 na Luka 15:11-32).

Tuheshimu viapo.
Thamani ya msamaha ni ukweli.
Kuokoka si chanjo, si dawa, ni UJASIRI wa kupokea matokeo.
Paka wa nyumbani akilala porini anakuwa paka-shume.
Funzo kwa wote: Aliyesamehe haamini; Aliyesamehewa haamini wala kuaminika, Aliyepotea hajifunzi japo anafundishwa.

NENO linajitetea..


Meseji nyingine yenye kichwa cha maneno "SIYEJUA AENDAKO, HAPOTEI NJIA" inasindikizwa na picha ya muumini akiwa anatubu dhambi kwa kuhani.

Kosa la muumini ni "Father, yesterday I beat up a politician". Na jawabu na mwendesha kutubio ni: "Confess your sins, not the good deeds."

1620159524334.png


Maelezo yake:

Walioshindwa hesabu, tufanye hesabu. Hivi mtu akisema tuna bunge dhaifu anamaanisha nini?

1. Spika dhaifu
2. Wabunge dhaifu
3. Katibu dhaifu
4. Wananchi dhaifu
5. Yote hapo juu dhaifu.

Na huu unaitwa ugonjwa gani?

a. Rais ana nguvu kuliko urais
b. Spika ana nguvu kuliko bunge
c. Wabunge wana nguvu kuliko bunge
d. Askofu ana nguvu kuliko kanisa.
e. Jaji ana nguvu kuliko mahakama.

Tufanye nini na haya?

1. Mbwa mlinzi anayemzuia mwenye nyumba kuingia nyumbani kwake

2. Uhuru usiotoa kujitawala

3. Kujitawala bila Uhuru

4. Uchaguzi unaomaanisha uteuzi na uteuzi unaomaanisha kifungo.

5. Madaraka yasiyokuwa na mamlaka, na mamlaka yasiyokuwa na madaraka.

Asiyenunuliwa hana thamani. Asiyenunua hana cha kuuza. Rushwa ipo, kama unabishi subiri Kikosi Kazi (Task Force). Mbele ya kikosi Kazi hata risiti ya rushwa utapata.


Mitandao ya kijamii inaonyesha kwamba mwandishi wa meseji hizi ni Askofu Benson Kalikawe Lwalinda Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, mkoani Kagera.

Anachokifanya Askofu Bagonza ni kitendo cha disinformation by spinning.

Kuhusu neno spinning, namaanisha dhana hii:

"In public relations and politics, spin is a form of propaganda, achieved through knowingly providing a biased interpretation of an event or campaigning to influence public opinion about some organization or public figure."--Wikipedia.

Ushauri kwa timu Mbowe:

"Mshauri wako akikwambia jambo la kipumbavu ukalikubali na kulitekeleza, wakati anajua kwamba hilo ni jambo la kipumbavu, na akiwa anafahamu kwamba wewe unayeshauriwa unafahamu fika kwamba jambo hilo ni suala la kipumbavu, atakudharau kwa sababu ya namna unavyofikiri, kuamua na kutenda"--J.K. Nyerere.
 
Kwhy miaka 5 ya uspika wa ndugai amesimamia nn cha maana Kama sio kupoteza muda na akina Lema ..Ni kiongozi wa hovyo never ever happen under strong institution as parliament
Anachosimamia hicho hapo

 
Hata mimi sijawahi kuona duniani, ina maana hamuamini Katibu Mkuu wa Chadema? Haamini kama walikaa vikao? Ya nini kuomba viambatanisho vyoote hivyo wakati kinachotakiwa ni barua tu! Au na barua nyingine za kiofisi ni lazima kila kitu kiwe na viambatanisho kama ripoti?
Mwisho wa siku bwana ndugai ndiyo ataonekana mjinga. Mwaka jana tu hapa alikuwa anamnanga halima mdee na kumfungia mwaka mzima! Mwaka huu anaona umuhimu wa wanawake???
 
Ndugai arudi Mirembe. File lake lipo kule.

Hivi kuandika barua kwake ni lazima uweke attachments zote hizo?

Yeye kama speaker anaesimamia wabunge wa vyama vyote ndio mwenye kutakiwa kuwa na katiba za vyama vyote ili ikija barua aweze kupekua na kuona je hao walioandika barua wako sawa au la.

Suala la kusema CHADEMA waambatanishe mambo kibao kwenye barua ni ujinga na haijawahi kutokea duniani.

Hiyo sio "report" ni barua. Mwambieni ajifunze kutofautisha.
We Kamanda. Spika sio msajiri wa kukaa na katiba za vyama.

Mmeonyesha jinsi mlivyo na uwezo mdogo wa kuendesha chama. Iteni baraza kuu msikilize rufaa zao maamuzi ya mwisho ndio yafanyiwe kazi...
 
Yaonekana una hamu tu ya kujipa furaha hewa.
Ndugai sasa hivi anababaika kwani alitegemea sana uwepo wa Jiwe kulinda takataka zake kama alivyozoea na kujidekeza.
Covid 19 hawakupendekezwa na CHADEMA. Utaratibu mzima na sheria zake viko wazi na havikufuatwa kabisa.
Huko ndiko swala lenyewe linakoanzia.
Mengine hayo ni muendelezo tabia zake mbaya, ambazo ziliendana kabisa na tabia za mungu wa Burigi aliekuwa anapata furaha na usingizi mwema kwa kukomoa na kukandamiza watu kwa kusigina katiba.
Hili bunge sio mali yake kiasi cha kujivuna hadharani kuwa hapangiwi wala hatakiwi kuongozwa. Hayuko juu ya sheria za nchi.
Kama Mama atarithi na kukubali kuendeleza uvunjaji huo wa katiba atakuwa ameanza kujichafua kitu ambacho sikitegemei sana.
Ninapenda kuamini kuwa atatafuta namna ya kulitatua kabla halijamfikisha pabaya. AMEN
Unaijua katiba au unachangia kichadema? Bunge ni muhimili na hakuna ambacho Rais wala mtu yeyote anayeweza kuliamlia. Poleni sana madalali.
 
Ndugai arudi Mirembe. File lake lipo kule.

Hivi kuandika barua kwake ni lazima uweke attachments zote hizo?

Yeye kama speaker anaesimamia wabunge wa vyama vyote ndio mwenye kutakiwa kuwa na katiba za vyama vyote ili ikija barua aweze kupekua na kuona je hao walioandika barua wako sawa au la.

Suala la kusema CHADEMA waambatanishe mambo kibao kwenye barua ni ujinga na haijawahi kutokea duniani.

Hiyo sio "report" ni barua. Mwambieni ajifunze kutofautisha.
Kihalali jana kidogo ndugai nilimuelewa, Nikweli kua hawezi kuamua mtu moja au wawili kua huyu hatumtaki kwenye chama. Alicho kisema ni kua lazima waonyeshe procedures zilizofuatwa hadi kufikia uamuzi huo. Ni vikao kadhaa vilikaa kwa mujibu wa katiba yetu na viliazimia kuwafuta uanachama wanachama wetu hawa kwa kuwa wametenda makosa haya mbona ni kitu kirahisi tu?
 
Unaijua katiba au unachangia kichadema? Bunge ni muhimili na hakuna ambacho Rais wala mtu yeyote anayeweza kuliamlia. Poleni sana madalali.
Mhimili hauna uhuru wa kuvunja katiba hilo halina kisingizio. Hakuna aliye juu ya katiba na sheria za nchi.
Yaonekana ulishazoezwa kuchezea katiba na anaewania umalaika mkuu ndio maana unaendelea kuwa kichekesho.
Jitahidi tu ukiacha tuisheni ya Polepole utaweza kuielewa vizuri na huko mko wengi mliyoathirika na deko.
 
Mhimili hauna uhuru wa kuvunja katiba hilo halina kisingizio. Hakuna aliye juu ya katiba na sheria za nchi.
Yaonekana ulishazoezwa kuchezea katiba na anaewania umalaika mkuu ndio maana unaendelea kuwa kichekesho.
Jitahidi tu ukiacha tuisheni ya Polepole utaweza kuielewa vizuri na huko mko wengi mliyoathirika na deko.
Nyie saccos mmetii katiba ya kikoba chenu? Kwanini basi msiitishe baraza kuu kusikiliza rufaa? Kwanini mnalazimisha maamuzi kwa Spika bila kuitisha baraza kuu? Mnaogopa nini kuitisha baraza kuu?
 
Back
Top Bottom