..tatizo sio viongozi wa Cdm.
..tatizo ni kwamba wako baadhi ya watu wako juu ya sheria.
..sheria nchi hii ina-apply kwa baadhi, wakati wengine hawaguswi.
Mkuu Joka, kuna sehemu tatu za suala la Spika na Team Halima
1. Kwa wenye kumbu kumbu, Spika Mkwawa, Msekwa, Mang'enya, Sitta walikuwa na kauli za kiutu uzima
Kwa miaka ya karibuni na hasa mitano iliyopita kumekuwa na kauli za indhara na karaha kutoka kwenye kiti kile kile cha akina Mkwawa na Sitta .
2. Haihitaji ujuzi wa sheria kujua kwamba anachofanya Spika ni uvunjaji wa sheria.
Akiwa mkuu wa mhimili unaotunga sheria hili nalo linakera sana.
Mbunge akifukuzwa na chama chake kama ilivyokuwa kwa Sophia Simba automatic anapoteza Ubunge.
Ndivyo ilivyotokea siku zote, leo kwanini kwa Team Halima sheria ivurugwe na Spika?
3. Chadema kuna tatizo la kushughulikia Halima na Wenzake.
Siyo kazi ya Chadema kuamuru au kutaka wafukuzwe Bungeni.
Sheria ndiyo inayotaka hivyo na wala si wajibu wa Chadema kuiongelea , ni hisani tu.
Wanachotakiwa Chadema ni kumtaka Spika, na kwavile kuna barua na ushahidi , basi kupitia Mwanasheria wao amwandikie Spika akimtaka asitise kutumia jina la Chadema kwa wabunge hao, na kwamba wasihusishwe kwa jina au chochote kile. Na kwamba, ikitokea hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwemo kutafuta tafsiri ya mahakama
Chadema wanaweza kwenda mahakamani, si kutaka wafukuzwe Bungeni bali kuwataka Wabunge hao, Spika na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutohusisha, jina au shughuli zozote zile za chama na hao Wabunge. Hilo tu !
4. Si suala la Chadema kupinga uwepo wa Wabunge, bali ni suala la Walipa kodi kumtaka Spika asitishe malipo kwavile kufanya hivyo ni malipo yasiyo halali kama findings zingine katika audit.
Hili jamani si suala la Chadema, ni suala la wananchi kuhakikisha sheria zinafuatwa na kwamba hakuna abuse ya sheria zinazotuongoza wala hakuna aliye juu yake na kwamba, kodi zetu zinatumika kwa mujibu wa sheria zilizopo na si mtu au watu.
Hapa ndipo Watanzania wanatakiwa waamke, kodi zinazowalipa hao Wabunge si za Chadema ni za kwako wewe, mimi na yule.
Pascal Mayalla Ngongo