Kama biashara/Ajira inakunyima muda wa ibada bado ni masikini, Ongeza bidii na umaridadi wa akili yako.

Kama biashara/Ajira inakunyima muda wa ibada bado ni masikini, Ongeza bidii na umaridadi wa akili yako.

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Unatakiwa utafute pesa hadi ifikie hatua pesa ulizotafuta zenyewe zinaanza kutafuta pesa nyenzake zaidi.

Unatakiwa ufanye kazi kwa bidii na kwa kujituma bila kujionea hurumq hadi ifikie hatua huitaji bidii kubwa kupata kipato.

Kwa hiyo bidii yako lazima iwe na malengo hata kama bado unajitafuta kiuchumi. Lengo ufikie hatua ya kupata muda wa kutosha wa kumuabudu Mungu, Kushiriki mambo ya kijamii, kushare vile Mungu alivyokupa kwa jamii inayokuzunguka kwa nia njema bila kuwa na nyama kifichi ya kuwapiga.

" Fanyeni biashara hadi nitakaporudi" Yesu.


Ni hayo tu.
 
Kweli ila Mungu alisema Siku 6 fanya kazi, Siku ya Saba ni Sabato Takatifu, Pumzika usifanye kazi wewe, wala mnyama wako, wala mjakazi wako, wala mtumwa wako, maana Bwana alistarehe na kupumzika
 
Back
Top Bottom