wacha porojo za warabu lete facts!
What is the fact?
A fact is something that has really occurred or is actually the case. The usual test for a statement of fact is verifiability—that is, whether it can be demonstrated to correspond to experience. Standard reference works are often used to check facts. (according to Wikipedia)
Ukiitazama hiyo definition kuna sifa tatu za msingi za hicho kinacho itwa 'Fact'
1- something has real occurred
2- Verifiability
3-Standard reference for check it.
Je kile ambacho hakiingii kwenye hizo sifa tatu siyo 'fact?' Kama vile uwepo wa roho, uwepo wa MUNGU MMOJA. Kwenye universal yetu ni 1% tu ya vitu vyote ndivyo tunavyo weza kuvidiriki kupitia milango yetu mitano ya fahamu na 99% hatuwezi kuvidiriki, je tutasema hivyo 99% siyo fact? Nywele zako, kucha zako zinakua unazikita, lakini kwenye definitio ya fact huwezi kuestablish ni vipi, kwa namna gani, kwa kiwango cha spidi gani vitu hivyo vinakuwa, je utasema siyo fact?
Adama na Hawa waliumbwa kutokana na udongo, 'fact' yake ni mchanganyiko wa madini mbalimbali yanayo tokana na udongo yaliyopo kwenye miili yetu. 'Fact' yake ni vyote tunavyo kula kwenye aridhi hii vinaendana na kuwiana sawia na maumbile ya mwili wetu. Lakini roho haitokani na udongo, na chakula cha roho si vitu vilivyopo kwenye udongo. Roho imetoka katika ulimwengu mwingine kabisa.
Mambo ya binadam na tabia zake hizi, zinamfanya binadamu aonekane ni mgeni kwenye dunia hii kushinda wanyama wenzake. Kwanini anaamini juu ya nyota, ulimwengu ambao hata tembo wala bluu Whales baharini hautambui. Hisia zake kubwa ni zile za woga, lakini siyo ule waoga wa kibaiolojia ambao wanyama wengine huuhisi, ni woga wa kiroho. Woga wa kutokuridhika, woga wa maajabu yanayo mzunguka, woga wa ibada zake, woga wa matokeo ya vitendo vyake. Woga ulio zalisha majina ya vitu kama ‘kitukufu,’ ‘halali,’ ‘siyo halali,’ ‘haramu,’ ‘kibaya,’ ‘kizuri,’ nakadhalika. Lakini haya yote yanatoka wapi ikiwa hapa ni kwetu na ndiko asili yetu. Hapana binadamu ni kama mgeni kwenye uso huu wa dunia, ni kama anayo asili nyingine, asili ya kiroho.
Kwanini mwanadamu kisaikolojia haridhiki, pamoja na kuwa atamiliki kila kitu anacho kitaka. Kwanini pesa siyo kila kitu, atakuwa na nyumba, magari, viwanja, biashara kubwa, kubwa, familia kubwa, na mengine na mengine, lakini bado shimo lake la saikolojia halitotoshwa kujazwa na vitu hivyo? Kwa nini kujiua na magonjwa ya akili vimeongezeka kila pale, hali nzuri ya maisha ilipo ongezeka na elimu ilipo ongezeka? Kwanini maendeleo ya kivitu hayamaanishi maendeleo ya kiutu? Sababu binadam anayo asili mbili, asili ya mwili na asili ya roho ambapo wazazi wetu Adam na Hawa waliishi, na ambapo kila roho kabla ya kuja hapa duniani kupitia 'kiwiliwili' kinacho itwa mwili, inaishi huko.
Do your research na si kila ukweli wa msingi uwe umekidhi defenition ya 'fact.'
Kuna zaidi ya kile ambacho milango yako mitano ya fahamu inaweza kukidiriki hadhiri yake, lakini kuna ambavyo vipo na haviwezi kudirikiwa na milango hiyo.