Kama binadamu aliumbwa kwa 100% je, ilikuwaje mwaafrika akawa mtu mweusi?

Kama binadamu aliumbwa kwa 100% je, ilikuwaje mwaafrika akawa mtu mweusi?

Wewe ni mzungu au mwafrika...mbona km swali lako lina ubaguzi,kwa hiyo hii rangi we unaona km adhabu au?
 
Na alifikaje afrika kutoka bustani ya edeni?

Na ilikuwaje hadi mzungu mwarabu walikuja kumwambia muafrika mungu yupo wakati huo wote walitoka sehemu moja?

Na ilikuwaje mungu kila mtu anamuita kwa jina lake na wakati huo aliye waumba ni mmoja na jina lake alifahamika kwa jina moja toka alivyo waumba?
Mbona ushangai uwepo wa Wazungu, we ushangai ulaya kuwa ya Wazungu?, india kuwa ya Wahindi?
 
asili ya binadam ni moja 'ADAM na Hawa' au ADAM na EVA', waliishi katika 'bustani' hiyo kwa muda amabo waliendelea kufuata masharti ya kuishi humo, na walipo vunja masharti hayo, waliletwa duniani, namna gani walifika hapa, haina tofauti na namna gani YESU (ISSA) alipaishwa kwenda mbinguni.

Ukizitazama dini zote duniani utaona zinayo asili moja au aina fulani ya uwiano, sababu mitume mbalimbali walitumwakote duniani kwa watu wote, wa rangi, kabila na maeneo tofauti, kwenye mafunzo ya kiislam tunajifunza duniani walifika mitume takribani 125,000. Kati hao kuna mitume wanne (4) wakubwa, ambao ni, Daudi, Musa, Issa, Muhhamad (amani ya Mola iwe juu yai wote), majukumu yao hawa yalikuwa makubwa zaidi na hasa mtume wa mwisho Muhammad ambaye amekuja kwa watu wote na majini wote ulimwenguni kote. KWA MAELEZO ZAIDI TIZAMA BLOGI YA SALIMMSANGI, Posti inayotwa 'NAMTAFUTA MUNGU.'

Binadam tunatofautina kabila na lafudhi, hivyo MUNGU, kwa watu na makabila tofauti ametajwa kwa majina tofauti.
aah mku,DAUD ni mtume?
 
Bustani ya Edeni Lugha ya picha kuelezea tu kwamba Mungu aliwawekea binadamu wa kwanza mazingira kamilifu kabisa.Ni mazingira yaliyojitosheleza.Kwamba binadamu wa kwanza waliishi maisha ya upekee sana.Kwamba walikuwa na Abundant resources.Leo tuna Limited resources.
ha ha ha ha,abundant resource ya machungwa labda...so why walikuwa uchi wa mnyama?
 
Binadamu wa kwanza ni mweusi katika mabara yote walioweusi au wekundu ndo wenye asili ya mabara hayo na weupe wote ni wageni angalia Africa, Australia, Marekani na Hata Asia utakuwa Magia ni weusi ni specie ambayo inapatika dunia yote na hii ndo uzao wa binadamu wengine wote duniani hao weupe ni upungufu wa baadhi ya virutubisho ndo maana miili yao hubadili rangi na kushambiwa na magonjwa kama vimafua kirahisi sana
 
Bustani ya Edeni Lugha ya picha kuelezea tu kwamba Mungu aliwawekea binadamu wa kwanza mazingira kamilifu kabisa.Ni mazingira yaliyojitosheleza.Kwamba binadamu wa kwanza waliishi maisha ya upekee sana.Kwamba walikuwa na Abundant resources.Leo tuna Limited resources.
Kabisa
 
Wewe ni mzungu au mwafrika...mbona km swali lako lina ubaguzi,kwa hiyo hii rangi we unaona km adhabu au?
Sio ubaguzi ila inatakiwa waafrika tujitathimini upya na sio lazima tukipokee kila kitu.
Kutoka kwa watu ambao walitutawala.
 
Rangi ya binadamu hutokea kutokana na mazingira anayoishi,si tu kwa binadamu bali kwa wanyama wengi yaani adaptation.Mfano waafrika walio karibu na Msitari wa Ikweta rangi zao ni weusi zaidi ya wale walio mbali na Ikweta hii humfanya aweze kuishi kwenye mazingira
 
Kwahiyo unakubari kwamba bindamu hakuumbwa ila alitokea kutokana na mazingira?
 
Binadamu wa kwanza ni mweusi katika mabara yote walioweusi au wekundu ndo wenye asili ya mabara hayo na weupe wote ni wageni angalia Africa, Australia, Marekani na Hata Asia utakuwa Magia ni weusi ni specie ambayo inapatika dunia yote na hii ndo uzao wa binadamu wengine wote duniani hao weupe ni upungufu wa baadhi ya virutubisho ndo maana miili yao hubadili rangi na kushambiwa na magonjwa kama vimafua kirahisi sana
Kwahiyo binadamu hakuumbwa ila alitokea kutokana na mazingira?
 
Na alifikaje afrika kutoka bustani ya edeni?

Na ilikuwaje hadi mzungu mwarabu walikuja kumwambia muafrika mungu yupo wakati huo wote walitoka sehemu moja?

Na ilikuwaje mungu kila mtu anamuita kwa jina lake na wakati huo aliye waumba ni mmoja na jina lake alifahamika kwa jina moja toka alivyo waumba?
Hizo ni decorations tuu. kwani nyumba zote zina rangi moja?? Zina rangi tofauti ili kupendezesha mtaa hata uumbaji ndo ivoo. Usiwaze wala kuconfuse mambo!
 
Hivi mkuu unadhani binadamu ni jiwe hadi asitembee? Au umesahau kwamba moja ya sifa kuu ya mamalia ni kutembea (MOVEMENT) ??

Kingine unachodanganywa kwamba Mwafrika alikuwa hajui Mungu usipende kukiamini. Ukristo umeingia Egypt, Nubia, Sheba, Libya na Timbuktu hata kabla ya kufika Ulaya.

Na hapo kwenye lugha hujiulizi kwanini Kichagga cha Kibosho na Machame kinatofautiana kwenye baadhi ya vitu, japo bado kinakuwa ni Kichagga?
Umesahau kwamba hata Kiswahili kina Lahaja zake. Kuna Kipemba, Kiunguja, Kimrina na Kimtang'atwa lakini bado ni Kiswahili?

The primary Essence of Language is to facilitate communication that enables human understanding of the basic concepts of life. Aesthetic role just adds Ingredients to it.
Safi ungekuwa mtoto wakike ningekuchumbia safi umeeleweka
 
Back
Top Bottom