Kama binadamu wa kwanza alikuwa mweupe, watu weusi wametoka wapi?


nikuite mama kwa avatar yako. nimetafakari hili neno la akili mara nyingi. nimejiridhisha kuwa wazungu wana akili sawasawa kabisa na ya kwetu. kitu kidogo ambacho tunatofautiana nao ni neno 'sharing.'

kwetu kuna dawa ya kansa. ukitaka kupona lazima umfuate mwenye kuujua ule mti. hakuna 'sharing' of knowledge. hiyo dawa ni siri. mzungu akigundua kitu 'anashea' kwa maandiko.

kwanini tunakuwa wagumu wa kushea? rudi kwenye cognitive development. ipo stage ya mtoto kwenye zile hatua za mwanzo anapotaka kila jambo liishie katika yeye. mtu mweusi yupo fixed kwenye hatua hii ya psychological development. hatujawa tofauti ya wanyama wa porini kwenye hili. ngoja nikuwekee picha (i can't find it lakini ipo somewhere--i just can't find it right away) ya chui kaua nguruwe. yule chui hawezi kumaliza nguruwe yule peke yake. mbweha aliyekuja pake kula aliuawa. kama sijakosea ni baada ya mtoto kugundua kuwa ipo raha nje ya maziwa ya mama, ndipo yule mtoto kwanza huanza kujinyonya kidole, baadaye anagundua ohoo kumbe kuna raha ingine sehemu za siri, baadaye hilo linaweza kuhamia kwenye hela akawa bahili sana, au fisadi. anahamisha centre ya raha binafsi.

ubinafsi ni zao la kudumaa kisaikolojia. mtu akijua kitu hataki kushea. matokeo yake knowledge inakufa. Wazungu wanashea knowledge, na hivyo kukuza knowledge. ni hapo wanapotushinda, lakini si kwenye akili. mimi kwanza! michango ya harusi watu wanachanga hadi milion 40 kwa sababu zitaliwa. kuna ubinafsi umekuwa sugar coated katika michango ile.

selfishness is our problem. siyo akili.
 

Kila kitu ni evolution theory nothing new

 

Kuna theories nyingi sana behind black race emergence but the reality and their truth are still disputed......hata neno black lenyewe haliendandani na halai halisi....has to do with dark.....kama uko gizani ni gizani tu.....hatuoni kama tuko gizani ..tumewekwa gizani ndio maana wazungu wanatufanya tuamini kila wasemalo....dini....democracy...humanrights...genocide.........exitrimism all has to do with Africa.
 


hoja yako nataka niikubali kwa sababu haijadispute wazo napendekeza kwako. haya unayoyasema yanawezekanaje? yanawezekana kwa sababu tunayo inherent weakness. nataka nipendekeze kwamba hiyo inherent weakness SI uwezo wa kufikiri. Bali kwamba tunao uwezo mkubwa wa kufikiri, isipokuwa katika maumbile yetu ipo anti-dote ya fikra endelevu, ambayo ni selfishness.

mwaka 1964 nadhani ilikuwa ile, au pengine 1963, nikiwa mdogo lakini naweza kukumbuka matukio ya wakati huo, nilikuwa naumwa. tumetoka nyumbani na mama yangu mzazi kwenda kwa tabibu. yule mzee hakuwahi kusoma mahala popote kuhusu acupuncture au mbinu nyingine wanatumia binadamu wengine. tumefika pake, mama naye alikuwa na matatizo yake. yule mzee alichukua kipande cha pembe ya ng'ombe yapata nchi nne za pembe ule upande wa juu. kule kwenye ncha ya pembe kulikuwa na nta yenye rangi nyeusi hivi. alichemsha maji, akaosha sehemu ya mgongoni kwangu palipokuwa panauma, akanikanda kidogo kwa namna ya kusafisha kwa majani fulani, kisha akachanja chale hapo. hadi hii leo chale hizo zipo hapo kiunoni kwangu. yule tabibu akachukua kitu chenye ncha kali akaweka kishimo upande wa juu wa ile pembe ya ng'ombe kupitia kwenye ile nta halaf nikaamriwa kuinama fulani hivi. baadae aliweka ile pembe hapo kwenye chale na kunyonya hadi ile pembe ikashika pale kwa kutumia nguvu ya pumzi ambayo imezuiwa kutoka baada ya yeye kuziba kile kishimo. hii ilikuwa njia ya kusafisha damu kwa kuondoa damu chafu. nilipona.

Leo hii waganga wa muhimbili na kwingineko wanakamua majibu kama kwamba sisi hatukuwahi kujua hayo. nani anakwambia hatuna akili? Wazungu wanagundua kitu, wanashea ujuzi, kizazi kinachofuata kinaboresha ujuzi ule ndo maana leo hii tuna cd players badala ya gramophone, tuna flash disc badala ya floppy. Ndiyo maana leo tuna magari badala ya matoroli. Wanashea knowledge ili kizazi cha baadae kijue pa kuanzia.

Ubinafsi unatuzuwia waafrika kuongeza ujuzi. Wazungu wanasaidia mtoto mwenye kipaji hata kama si mtoto wako. Sisi mtoto mwenye kipaji anatafutiwa sumu afe. Tatizo la mtu mweusi ni ubinafsi--siyo uwezo wa kufikiri.

nikubaliane nawe kwamba tunalo tatizo la kukubali kila kitu kimesemwa na mzungu. hata kama ni upuuzi. na ukitaka kujua hilo angali tatizo la Zimbabwe.

Mugabe hana kosa kutaka wazungu wagawe ardhi yao. labda si kuchukua yote, lakini kugawa ardhi ile equitably hapakuwa na kosa kabisa katika fikra ile. ni taifa gani la kiafrika limejitokeza kumsaidia mugape? kinyume chake hii miafrika imekubaliana na wazungu eti zimbambwe hakuna demokrasia. aliyekwambia demokrasia ndo jibu la kila tatizo nani? si kila anachosema mzungu ni sawa. Mengine wanayasema kulinda maslahi yao ya miaka hamsini ijayo.
 

Ndugu yangu uchambuzi wako ni mzuri na lazima nikiri unaweza dadavua mambo humu JF........lakini hebu tuangalie Intellectual Property Rights(IPR) Laws kaleta nani...wanavumbua, wanazuiya uendelezaji uwe ndai yao wenyewe, hata kama kitu kitavumbuliwa Africa wanataka kikawe Approved Ulaya au marekani , hawataki kusikia mwafrika kavumbua kitu.

Fikiri jinsi walivyouwa dini zetu kwa kuziassociate na ushirikina, yote ni kutufanya tuamini wao tu kwamba they are right...ukifuatilia maisha ya mtanzania kwa mfano kule kijijini kwetu, (usukumani) mtu akipita sehemu akakuta watu wanakula akikaribishwa anakaa anakula bila kujali anatoka wapi..wanashare kile walichonacho.

Kwa mzungu ni nadra sana..anamaneno mengi ya kutofautisha kila jambo, mfano twende lunch na karibu lunch yanamaana tofouti... na ukiyaparamia utaumbuka....katika selfishness hawa weupe wanaongoza, na ndio maana wakawa maracists
 
Mambo ya imani ukiyachanganya na science jibu lake lazima liwe kama hayo yanayotolewa na GT wa hapa. lakini cha muhimu lazima ujue kuna mahala ambapo science inakoma na imani inaendelea.
 
 
 
Mh ila mkuu hapa umetupeleka chaka. Ina maana watu wanaoishi nje ya Ikweta wote ni wazungu? Inakuwaje basi kwa waafrika walioenda utumwani Ulaya na Amerika miaka ya 1870 huko na wakazaana wao kwa wao weusi, je kuna waliozaa wazungu kati yao bila kuchanganya? Hakuna mwenye majibu hapa tuache kudanganyana bali tubaki na Imani zetu tu.
 
Mkuu acha hii habari, usilazimishe uongo kuwa ukweli. Ina maana hiyo evolution unayoisema iko kwa weusi tu kuelekea weupe? Weupe hawana/hawakuwa na evolution?

Na kwanini hiyo evolution ilifanyika half way? kwamba ilichukua weusi wachache ikawabadilisha kuwa wazungu/weupe (ilihali wote walikuwa same environment) na kuacha wengine waendelee kuwa weusi??? Why so selective?

Tatizo tunalazimisha majibu ya kila kitu kwa ufahamu tulionao sasa. Vitu vingine tuviache viendelee tu kwani viko nje ya ufahamu wa kibinadamu.
 


Kutokana na maelezo yako naona hukunielewa... na kwa kua hukunielewa umeleta arguments za ajabu sana.. em jaribu kurudia kusoma nlichoandika na ukifikirie vzr umenitafsiri vibaya.. Ukikaa unasema vitu vingine tuviache kwa kua viko neya uwezo ya kibinadamu huna tofauti na waafrika wavivu wa kufikiri wanaoachia kila kitu wazungu ndio wanatafuta.. Hii knowledge unayoioinga ndio inatengeneza madawa unayotumia
 

Sasa km walianza weusi alafu wakaja weupe kwa sababu walizaliwa katika wale weusi sasa ikawaje adi watengane yaani weusi africa then weupe ulaya? Au waliama?
 
mtu wa kwanza ni mweusi na sisi ndio original people
 
Wrong.......

Hakuna kitabu cha dini kinachosema adamu na hawa walikuwa weupe au weusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…