Pre GE2025 Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila...

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chadema haiokoti wagombea mitandaoni kwa kushauriwa na mamluki , inao utaratibu wake wa kila mwenye kudhani anaweza achukue fomu
 
Muulize mwendazake Nini kilimfanya apitishe wabunge, madiwani, wenyeviti vijiji mitaa vitongoji bila kupingwa tena na yeye mwenyewe kujipitisha? Kama kweli vyama upinzani havina nguvu ni kwann Kila uchaguzi serikali inaongeza magari ya kukojolea watu pilipili? Na ni kwann Kila CHADEMA wakitangaza maandamano tena ya amani lazima serikali itangaze kuwa majeshi Fulani yatakuwa yanadeki barabara
 
Gonga like kama mwandishi aliposema uchaguzi wa 2020 walijua matokeo.
Huyu bro nadhani alikuwa india kipindi cha ule uchafuzi wa mwaka 2020 .tunashukuru sana alietuulia ile mbwa ya chato.
 
Kwanza 2025 hakutakuwa na uchaguzi kutakuwa na kugawa a majengo ya Uma. Hatuwezi kuendelea na ujinga huu wa miaka yote. Kodi za watanzania kutumika kugarmia uchaguzi ambao unaamriwa na mtu mmoja. Ni aibu kwa msomi kama wewe kuandika kishabeki kwa kiwango hiki. Yaani unaandika kama vile unachambuwa mchezo. Hivi kweli unawafikiria wanao au kwa vile wewe unaona uko vizuri na system hii ya utawala unaona hamna shida. Hapa sio jambo la kuchaguwa Kati ya mwanamke na mwanaume hapa ni kuchaguwa Kati uhuru na utumwa. Au Kati ya elimu na ujinga. Sasa msomi kama wewe kuongelea suala serious kama uchaguzi kwa style ya kushabekea Chama tawala ni bahati mbaya Sana.
 
Mkuu hata wakiweka kura za uongo, Bado ukweli utakuwa unaonekana maana binadamu sio kivuli, kama hawapo hawapo tu, na ujumbe utakuwa umefika sawia kuwa watu wamewachoka.
 

Mimi napendekezza uchaguzi ufaanyike baada ya Kupatikana kwa katiba mpya.

Wakiwamaliza Kuwaondoa Wamasai kwenye ardhi yao watakuja kwa Wasukuma. Watawatumia Machawa waliojipenyeza usukumani kama Biteko kuwarubuni badala ya kuwatetea. Kama wamasai wenye silaha mkononi wamehamishwa itakuaje kwa Wasukuma ,wagogo nao kupisha madini kama Urenium n.k.
Hatukatai wawekezaji wala kuwahamisha watu tunachokataa ni kuwauzia wageni rasilimali zetu bila tija itakayobadilisha maisha ya Wazawa badala yake wanaonufaika ni watawala na machawa wao kwa pesa za kuhongwa na hao wanaowaita wawekezaji matokeo yake ni kupandishwa kwa kodi na kuongezeka kwa tozo na kikokotoo na kushuka kwa thamani ya pesa yetu na madeni makubwa na bidhaa kupanda bei mpaka zile za ndani ya nchi kama vyakula.

Ili zoezi la uwekezaji lifanyike kwa tija na kwa haki ni lazima tupate viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa haki kuanzia kule chini mpaka juu.

Haiwezeka ni nchi za kiarabu ,China , Korea , Marekani nk. ambazo kwa hulka na mikakati yao ya kibeberu na kinyonyji na hawakubali mwanamke kutawala kwenye nchi zao lakini leo wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kutusifia kuwa tupo kwenye njia sahihi kumbe ni ili watudhoofishe kimaamuzi na kiutawala na kupora rasilmali zetu kirahisi kabisa.
 
Nadhani ni vizuri tu na Yeye agombee Ubunge ili tusikose michango yake bunge lijalo,kuliko kuwa msindikizaje wa Rais atakayetoka CCM.
Michango ya Mbowe 2010-2015 ilikuwa na tija sana.
Nachoamini safari hii nadhani Tume ya Uchaguzi kwa maagizo ya Rais idadi ya Wabunge wa Vyama vya Upinzani angalau itakuwa kubwa (chini ya theruthi ya Wabunge wote)!
Kama Tume ingekuwa Huru na vyama vya upinzani vikajipanga vizuri safari hii CCM ingepoteza wabunge wengi sana mfano wa chama cha ANC huko SA ilivyopoteza.
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni maigizo tu, kama 2020 mgombea mwenza alisema " hata nchi nzima mki wapigia CHADEMA/Upinzani, CCM ndiyo itaongoza dola", na akongezea kwamba "kuwapigia kura CHADEMA ni sawa na kumwaga sukari ziwani".

Na huyo alikuwa mgombea mwenza, sasa leo yeye ndiye mgombea kutokana na sera na utaratibu wao mzuri na wa kidemokrasia wa chama chao, kwamba form ya mgombea urais huko CCM itatolewa moja na tayari ina mwenyewe ambaye ni SSH, unategemea nini kipya.

Wakiruhusu demokrasia ndani ya ccm kwenyewe hashindi hiyo nafasi, iweje agombee nchi nzima ashinde?

Nchi hii ili tutoke tulipo lazima nchi hii ivurugike, bila hivyo iko siku utasikia hata Makonda kawa rais wa JMT.
 
Kaka,Paskal
Chonde chonde,wewe unaonekana huwa una mawasiliano ya karibu na viongozi wengi wa CCM.Nakuomba uwashauri waanze kumuandaa mgombea mwingine.Hali ni mbaya mno kumsimamisha Mama.
 
Baada ya mnyama Simba kupewa jina la TL, nimeukumbuka huu uzi Wanabodi,
Leo nimelikumbuka bandiko hili kuhusu TL kukosesha mtu usingizi baada ya kuiangalia clip hii
View: https://youtu.be/UXFoyKtbEEA?si=l6IxoAUVEFFWXWSP
Usikute TL anamkosesha mtu usingizi!, halafu itokee TL ndie asimame nae 2025!, na alivyo hana break... si kuna mtu ataogeshwa .... kila uchao?.
Hapa ni ninauliza tuu!.

Ndio maana nimeshauri, kama mgombea wa urais wa chama kubwa 2025 ni mwanamke, then vyama vyote viweke wagombea urais wanawake wapambane na sio jitu dume zima lipambane ma majike!.

Hivyo nikapendekeza Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Na endapo wapinzani watakuwa hawana kabisa mwanamke ambaye ni match na mgombea wa chama kubwa hivyo ni lazima kumsimamisha mwanaume, then mgombea wa upinzani asiwe TL ili kumstahi mgombea mwanamke, maana jinsi TL asivyo na breki, hachelewi kumuogesha na mvua ya ... TL saizi yake alikuwa JPM na sio huyu Maza Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

hivyo nimeshauri mgombea wa upinzani awe Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila... sababu ya kupendekeza FM ni kufuatia kukubali maridhiano na CCM kugawana nusu mkate, TL anayabeza maridhiano Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Hili mnalionaje?.

P
 
Upo serious?
Mbowe hapana
Anajua anachokifanya ninyi hamjui hamjashtuka bado.
Perepereeee mingi action zero.
Mabadiliko yanahitajika pande zote watawala na wapinzani ni dugu moya.
Otherwise tuna miaka mingine 60 ya kuwa kama mazombie kama sasa.
 
Wanabodi!

3. Kufuatia Freeman Mbowe ku overstay kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chadema, kugombea urais kutampa Freeman Mbowe a perfect and an honorable exit.
Paskali
Kufuatia Lissu kutangaza nia kugombea Uenyekiti wa Chadema, Mbowe hana jinsi ni lazima apishe njia, kumpisha Lissu kukifufua Chadema kwa amsha amsha.

Namna ya Mbowe kuondoka kwa heshima, ni kupitia kugombea urais.

Kwenye urais nako Lissu anakutaka, kwa vile Lissu tunamjua jinsi asivyo na breki, asiruhusiwe kugombea urais, hachelewi kumuogesha mtu wetu kwa mvua za mananiliu!.
Mbowe ndie agombee
P
 
Kaka,Paskal
Chonde chonde,wewe unaonekana huwa una mawasiliano ya karibu na viongozi wengi wa CCM.
Sii kweli, ila kufuatia fani yangu ya uandishi wa habari, nawajua viongozi wa CCM na serikali akiwemo Rais Samia, nimefanya nae mahojiano mara mbili .
Nakuomba uwashauri waanze kumuandaa mgombea mwingine.
Tumeisha shauri, ushauri wa kwanza uko kwenye HII kitu.
Hali ni mbaya mno kumsimamisha Mama.
Hata hali iwe mbaya vipi, mshindi ni yule yule, chama kile kile !. Zisipo tosha, zinatosheshwa, zisipo jaa, zina jazilizwa!.
P
 
Advocate wewe upo upande wa Mwamba.
Ila Lisu ana "manifesto" nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…