Kama CCM ni chama cha watu wajinga, imetokeaje watutawale zaidi ya miaka 60?

Kama CCM ni chama cha watu wajinga, imetokeaje watutawale zaidi ya miaka 60?

Utawasikia CHADEMA wanakuambia ccm ni chama cha WATU wajinga Ila inawezekana vipi wajinga waitawale nchi hii miaka 60s?
Ni kweli ni chama cha wajinga na tanzania bado kuna kundi kubwa la wajinga ndio maana inakuwa rahisi kuongoza miaka 60s .

Mfano hapo kweny unaona viongozi wao wanateseka kwa sababu kuna kundi kubwa la wasomi wanaweza kuchambua mambo
 
Utawasikia CHADEMA wanakuambia ccm ni chama cha WATU wajinga Ila inawezekana vipi wajinga waitawale nchi hii miaka 60s?
Adolf Hitler, Bokasa, Idi amin,Sani, Abacha, Sadam Hussein, Hafez al asssad, Bashar Al Assad, hao, wote walikuwa viongozi wabovu lakini waliweza kukaa madarakani! Kasome historia! Hata apartheid ya SA hujuhi, iliwezaje kukaa, kwa muda mrefu,
Ccm ni waking, waulize, Uchaguzi mkuu uliopita Maghu na Samia walipata kura ngapi? Kila, Jimbo, weka link hapa, haipo!
 
Utawasikia CHADEMA wanakuambia ccm ni chama cha WATU wajinga Ila inawezekana vipi wajinga waitawale nchi hii miaka 60s?
Kwasababu sisi ni wajinga zaidi, tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuto kuhoji linaanzia kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukihoji kwenye ngazi hiyo utaambiwa kama umekua uondoke tabia hii ya kukataa kuhojiwa kwasasa imebebwa kwenye ngazi zote za maisha iwe mashuleni , kanisani , vyuoni kwenye vyama vya siasa na kwingineko

Tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo wengi wao hawawezi kuchakata fikra chanya na hasi jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

CCM wanaongoza nchi kwa mfumo wa unyumbu wa kisiasa ambao unawezesha wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi kwa tabia mbaya kama vile kujipendekeza ama kwa uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a. K.a kujizima data tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Wanyama nyumbu hufanya jambo fulani kwa kutumia akili za pamoja, (the same mind set), lakini huwa hawana mpango mkakati wa kukabiliana na majanga huko mbeleni wanako elekea, (no SMART goals setting), huongozana kwenye msululu kwa kupita mabonde na mito bila kuangalia hatari itakayo jitokeza mbeleni

Nyumbu hukutana na mamba wenye njaa wao huenda tu huku wengine wakinyofolewa ama kuuawa lakini wao hawajali hupita hapo hapo kwenye hatari mradi wafike wanako elekea hata kama wengine wakifa njia

Swali je nasisi ni kama nyumbu tukitekwa tuna nyamaza

Tukibambikiziwa makesi tuna nyamaza

Tukinyimwa haki tuna nyamaza
 
Sasa kama ndani ya chama anateuliwq baba levo kugombea ubunge unategemea chama kiwe na wenye akili kweli?. Mtu ambaye hajui hata KAZI ZA BUNGE.
Jibu swali kwanini nyie wenye akili mtawaliwe nawajinga kama ccm tangu 1960s acha ubabaishaji hapa
 
Utawasikia CHADEMA wanakuambia ccm ni chama cha WATU wajinga Ila inawezekana vipi wajinga waitawale nchi hii miaka 60s?
Ccm ipo kwasababu imejiungamanisha na vyombo vya dora.Ni ngumu kutenganisha ccm na vyombo vya doraWote wanafanya kazi kwa maslahi ya ccm.Wanakula kiapo kuilinda serikali ambayo ni ccm kwenye koti la serikali.Bila hivyo ccm wangekuwa wahenga.
 
Back
Top Bottom