Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Zoezi la kuchagua wagombea kwenye serikali za mitaa kupitia tiketi ya CCM limekuwa ni mizengwe na vurugu za kujitakia ambazo zimesababishwa na kanuni za uchaguzi zisizoendana na mazingira ya sasa.

Mipango waliyobuni ya kuchuja majina ya wagombea na kuyatangaza siku ambayo ndiyo zoezi la uchaguzi linafanyika yamekuwa ni kituko na chanzo cha vurugu kwa sababu kinachofanyika ni baadhi ya wagombea kuenguliwa kimizengwe na vikao vya kata na wilaya kwa lengo la kuweka wagombea ambao wengi wao hawakubaliwi kwa wana CCM wengi.

Wana CCM wanapoingia kwenye chumba cha kupigia kura husomewa majina ya wagombea ambao hawakubaliwi na kuanza kulazimishwa kuwapigia kura!

Kwa akili za kawaida, CCM ya Dkt. Bashiru kama mtendaji mkuu ilitakiwa ijue matatizo kama haya yangetokea kwa sababu rushwa na upendeleo ndani ya CCM bado upo hasa katika ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata na Wilaya.

Dkt. Bashiru Ally na sekretalieti yake walitakiwa wajue ili kupunguza rushwa na upendeleo, majina ya walioomba kuchaguliwa kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM yangerudishwa yote kwa wanaCCM ili wayapigie kura na sio vikao vya kata na wilaya viwaamulie nani wa kupigiwa kura. Hii kanuni ya uchaguzi haifai kwa mazingira ya sasa.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ‘’uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’. Kwa maamuzi haya mabovu ya Dkt. Bashiru na sekretalieti yake yamekaribisha mafisi na mainzi kugombea uongozi wa serikali za mitaaa kwa tiketi ya CCM.

Dhana inayojengwa kwa sasa kuwa ukichaguliwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM basi utakuwa umeishashinda uchaguzi inachochea rushwa na mizengwe ndani ya CCM.

Kwa mazingira haya hata ahadi namba 4 ya mwanachama wa CCM inayosema, ‘Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’ imebaki kwenye makaratasi!

Vyama vya upinzani walijua kitakachotokea ndani ya CCM ndio maana havijateua wagombea wake vikisubiri zoezi la CCM limalizike ili vianze kuvuna/kupokea wanaCCM ambao hawakutendewa haki kutokana na ubovu wa zoezi la uchaguzi ndani ya CCM.

Viongozi wakuu wa CCM wanatakiwa kujua hili zoezi limeharibika sana na linatakiwa kurudiwa upya nchi nzima!

Kama viongozi wakuu wa CCM watashupaza shingo kuhusu zoezi hili basi wategemee CCM kuvunjika ghafla, wala haitapata dawa!
 
Sidhani kama CCM watapoteza mitaa wakati chama kimevaa koti la serikali.

Rais ameifanya CCM ijisahau kuhusu ushindani, wanaccm sasa hivi wanahofu uchaguzi wa ndani kuliko uchuguzi wa nje..

Wana CCM wanaaamini ukipita ndani ya CCM umepita jumla (baba kasema) hivyo kuminya vyma vya upinzani madhara yake ndio haya CCM kupata wagombea wa hovyo hovyo na Taifa kuongozwa hovyo hovyo.

Rais kupata wasaidizi wa ovyo, ambao hawawezi hata kutatua mgogoro wa kiwanja cha hatua mbili mpaka Rais aje ndio wananchi watoe malalamiko yao.

Na hili linaenda hadi kwenye wabunge, watu wanaanda fedha nyingi za rushwa ndani chama sababu wanaamini ukipita ndani ccm umepita Kitaifa NEC yetu na Polis ni wetu (baba kasema)

Hili swala lipo mikononi mwa Rais akiamua mfumo wa baba kasema ufanye kazi ni yeye akiamua demokrasia ifanye kazi ni yeye.

Wananchi tupo pembeni tunamwangalia yeye na chama chake wanavyofanya, ndio maana hata kwenye kujiandikisha wengi tulikaa pembeni tuangalie mnavyofanya maana kila kitu kipo ndani ya uwezo wenu.

Hakuna la kuwashinda.!
 
Sidhani kama ccm watapoteza mitaa wakati chama kimevaa koti la serikali
Mkuu;
Chama kuvaa koti la serikali hakijaanza katika utawala huu lakini bado kilikuwa kinashindwa katika chaguzi!

Mbinu inayotumika kwa sasa ni kujenga mazingira ya kudhoofisha morally ya kundi jingine ili lisijitokeze kupiga kura na kufanya mabadiliko. Baadhi ya viongozi wa upinzani wameishtukia mbinu hii ya kuua morally ndio maana wamehamasisha watu waende kujiandikisha na kupiga kura.

Kwenye uchaguzi wowote ukiona watu wengi wanajitokeza kwenda kupiga kura basi lazima uelewe kuwa hicho ni kielelzo cha mabadiliko na walioko madarakani kukosa kura.

Ukiona watu wengi hawajitokezi kwenda kujiandikisha na kupiga kura, hicho ni kielelezo kuonyesha walioko madarakani wataendelea kuongoza kwa sababu watu hawana msukumo wa kufanya mabadiliko.

Hakuna anayeweza kuishinda nguvu ya umma kama imeamua kufanya mabadiliko.
 
Mkuu mbona una generalize kuwa zoezi lirudiwe nchi nzima wakati mimi niliko huku Tanga mambo ni shwari tu? Huoni kurudia nchi nzima ni kuwa sumbua wanachama bure hata ambao wamechagua bila mizengwe? Au mkuu umeshindwa kura za maoni ndiyo maana unapiga kelele?
 
Mkuu mbona una generalize kuwa zoezi lirudiwe nchi nzima wakati mimi niliko huku Tanga mambo ni shwari tu? Huoni kurudia nchi nzima ni kuwa sumbua wanachama bure hata ambao wamechagua bila mizengwe? Au mkuu umeshindwa kura za maoni ndiyo maana unapiga kelele?
Mkuu;
Kwanza, Mimi sikugombea na sitegemei kugombea nafasi ndani ya chama chochote cha siasa nchini.

Pili, zoezi kwa ujumla limeenda vibaya sana utajua ninayosema kama ukiuuliza watu wa vyombo vya usalama ndani ya CCM!
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
Screenshot_20191025-071927-picsay.jpeg
 
Kwenye hii mada yako kuna sehemu umeeleza kitu cha msingi Sana.
"Dhana ya wanaccm wengi ni kuwa ukichaguliwa Tu kupeperusha bendera ya CCM basi umeshinda uchaguzi"
Huku mtaani vita iliyopo ni ccm Kwa ccm na Hilo ni Jambo Baya Sana Kwa mustakabali wa chama chenu cha kishamba.
 
Back
Top Bottom