Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa!

Rushwa ndani ya CCM inasababishwa hasa na dhana kuwa ukipitishwa kuwa mgombea basi unakuwa umeshinda uchaguzi hata kwa kuwezeshwa!
Kumbuka 2015 Ndugai alishindwa kura za maoni, akampiga rungu mpinzani wake, hapa sisi majaji tunasubiri akiacha uspika afunguliwe kesi ya jinai
 
CCM ni ukoo wa panya ni itaendelea kuwa hivyo hadi Yesu atakaporudi. Kwa CCM kila mtu ni mwizi, kianzia kwa babu, baba, mtoto, mjukuu, kilembwe hadi kining'ina. CCM hata iongozwe na malaika, haina jipya kwenye suala la.rushwa na ufisadi.
 
Mkuu;
Chama kuvaa koti la serikali hakijaanza katika utawala huu lakini bado kilikuwa kinashindwa katika chaguzi!

Mbinu inayotumika kwa sasa ni kujenga mazingira ya kudhoofisha morally ya kundi jingine ili lisijitokeze kupiga kura na kufanya mabadiliko. Baadhi ya viongozi wa upinzani wameishtukia mbinu hii ya kuua morally ndio maana wamehamasisha watu waende kujiandikisha na kupiga kura.

Kwenye uchaguzi wowote ukiona watu wengi wanajitokeza kwenda kupiga kura basi lazima uelewe kuwa hicho ni kielelzo cha mabadiliko na walioko madarakani kukosa kura.

Ukiona watu wengi hawajitokezi kwenda kujiandikisha na kupiga kura, hicho ni kielelezo kuonyesha walioko madarakani wataendelea kuongoza kwa sababu watu hawana msukumo wa kufanya mabadiliko.

Hakuna anayeweza kuishinda nguvu ya umma kama imeamua kufanya mabadiliko.

Una utetezi mzuri, ila tulisema toka mwanzo rais aliyepo hana uwezo wa urais bali ni mjenga miundombinu. Anachofanya ni matumizi mabovu ya madaraka, kibaya zaidi analazimisha chama chake kishinde kupitia madaraka yake, matokeo yake hata nyie wenye chama mnaona fika viongozi watakaopatikana na chama ni tatizo. Hapa naona unaoongelea nguvu ya umma, nguvu ya umma maana yake unataka machafuko. Je sisi tunaosema kila siku kwamba rais huyu anataka kuleta machafuko kwakuwa hana uwezo wa siasa za ushindani tunakosea?
 
Mkuu mbona una generalize kuwa zoezi lirudiwe nchi nzima wakati mimi niliko huku Tanga mambo ni shwari tu? Huoni kurudia nchi nzima ni kuwa sumbua wanachama bure hata ambao wamechagua bila mizengwe? Au mkuu umeshindwa kura za maoni ndiyo maana unapiga kelele?
Huyo kashindwa mkuu sasa anataka uchaguzi urudiwe nchi nzima
 
Zoezi la kuchagua wagombea kwenye serikali za mitaa kupitia tiketi ya CCM limekuwa ni mizengwe na vurugu za kujitakia ambazo zimesababishwa na kanuni za uchaguzi zisizoendana na mazingira ya sasa.

Mipango waliyobuni ya kuchuja majina ya wagombea na kuyatangaza siku ambayo ndiyo zoezi la uchaguzi linafanyika yamekuwa ni kituko na chanzo cha vurugu kwa sababu kinachofanyika ni baadhi ya wagombea kuenguliwa kimizengwe na vikao vya kata na wilaya kwa lengo la kuweka wagombea ambao wengi wao hawakubaliwi kwa wana CCM wengi.

Wana CCM wanapoingia kwenye chumba cha kupigia kura husomewa majina ya wagombea ambao hawakubaliwi na kuanza kulazimishwa kuwapigia kura!

Kwa akili za kawaida, CCM ya Dkt. Bashiru kama mtendaji mkuu ilitakiwa ijue matatizo kama haya yangetokea kwa sababu rushwa na upendeleo ndani ya CCM bado upo hasa katika ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata na Wilaya.

Dkt. Bashiru Ally na sekretalieti yake walitakiwa wajue ili kupunguza rushwa na upendeleo, majina ya walioomba kuchaguliwa kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM yangerudishwa yote kwa wanaCCM ili wayapigie kura na sio vikao vya kata na wilaya viwaamulie nani wa kupigiwa kura. Hii kanuni ya uchaguzi haifai kwa mazingira ya sasa.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ‘’uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’. Kwa maamuzi haya mabovu ya Dkt. Bashiru na sekretalieti yake yamekaribisha mafisi na mainzi kugombea uongozi wa serikali za mitaaa kwa tiketi ya CCM.

Dhana inayojengwa kwa sasa kuwa ukichaguliwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM basi utakuwa umeishashinda uchaguzi inachochea rushwa na mizengwe ndani ya CCM.

Kwa mazingira haya hata ahadi namba 4 ya mwanachama wa CCM inayosema, ‘Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’ imebaki kwenye makaratasi!

Vyama vya upinzani walijua kitakachotokea ndani ya CCM ndio maana havijateua wagombea wake vikisubiri zoezi la CCM limalizike ili vianze kuvuna/kupokea wanaCCM ambao hawakutendewa haki kutokana na ubovu wa zoezi la uchaguzi ndani ya CCM.

Viongozi wakuu wa CCM wanatakiwa kujua hili zoezi limeharibika sana na linatakiwa kurudiwa upya nchi nzima!

Kama viongozi wakuu wa CCM watashupaza shingo kuhusu zoezi hili basi wategemee CCM kuvunjika ghafla, wala haitapata dawa!

Majizi Yanaibiana yenyewe kwa yenyewe yanakuja JF kulia lia
Tukusaidieje sisi sasa kwa Mfano ???
 
Tuliwaonya mapema kuwa mkiuuwa upinzani, mtabaki kuumizana na kukanyagana. Ona sasa kiburi cha kubaki peke yenu, hakuna hofu tena.
 
Naunga mkono Hoja.

Mfano Kuna malalamiko mengi hapa Dar, Maeneo kama Kinondoni, Temeke na Ilala hususani Meeneo ya pugu, Tabata, Kinyerezi, huko ndipo rafu zilikua nyingi mno na % kubwa ya waliongoza kura za maoni hawakubaliki katika jamii.
Chama Cha Mapinduzi kinahitaji kufuta kura za maoni nchi nzima na kuweka utaratibu sahihi wa kuwapata wagombea wake.
 
Watashindwa na nani wakati mlikuwa mnashinda humu mnawashawishi wanachama na wafuasi wasijiandikishe kupiga kura? Pia ujue angalau CCM ilikuwa na utararibu. Na kasoro hazihepukiki na zinazorekebishika, CCM wameishaanza kuzifanyia kazi. Vipi kuhusu Chadema, CUF, ACT na wengineo. Walikuwa na utaratibu hani "mzuri" wa kuchagua wagombea wao?

Tena sio kushinda kusema watu wasiojiandikisha, bali tunasema hata kura wasipige, kuliko kwenda kupiga kura ambazo rais anatumia madaraka yake kuhakikisha chama chake kinatangazwa washindi, kwa gharama za kutia vilema wapinzani na hujuma za wazi. Kama Ccm wameanza kurekebisha kasoro, huyu mwenzako huu uzi kauleta hapa wa nini?
 
Nakushukuru kwa kuiogopa CCM.
 
Nakushukuru kwa kuiogopa CCM.

Hakuna anayeiogopa ccm maana ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya kidola. Hivyo hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushiriki siasa za kishamba. Ingekuwa hoja ndio muamuzi wa siasa za sasa hapo sawa, ila mabavu toka kwa jiwe ndio yamegeuzwa siasa. Sisi tulishatoka enzi za madisko ya kizamani kuondoka na mwanamme kitemi, siku hizi unaenda disko unachukua mwanamme kwa ushawishi au pesa yako. Hayo madisko ya ubabe wa kishamba tumewaachia washamba wa chattle.
 
Kabisa ni ukweli usiopingika kuwa CCM wanatengeneza tatizo la ndani litakalo wagharimu kukosa kura na kuwagawa wapiga kura kwenda upande wa pili.
Mfano:
Katika mji wa kibaha kuna mtaa mmoja ambao Wana CCM wamegawanyika kwa Udini waislamu na wa wakristo wa catholic hilo limepelekea mka catholic kushinda kwa sababu wa kristo wamama wamempigia kura lakini ni mama mzee wa miaka 65.
Kwa hili tu wamegawanyika makundi mawili CCM catholic na CCM Islam lakini vijana wote hawapo tayari kumpigia bibi kura wanadhani hafai kuwaongoza walimtaka mwana CCM kijana ambaye ameangushwa kwasababu ya uislamu.

Mtaa wenyewe ni mtaa wenye changamoto kubwa ukiangalia 60% ni vijana kuanzia 15-30 ni ngumu kumuweka mstaafu mwanamke kuongoza hili kundi lenye ushawishi na mambo mbalimbali.

CCM katika wanakosea sana.
Mkuu;
Bila viongozi wa juu wa CCM kufanya tathmini na kurudia zoezi zima basi wategemee kupoteza viti vingi kwenye uchaguzi.

Matatizo ni mengi sana sehemu mbali mbali na kibaya zaidi, yanasababishwa na viongozi ambao walitakiwa wawe ndio watafuta ufumbuzi!
 
Hakuna anayeiogopa ccm maana ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya kidola. Hivyo hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushiriki siasa za kishamba. Ingekuwa hoja ndio muamuzi wa siasa za sasa hapo sawa, ila mabavu toka kwa jiwe ndio yamegeuzwa siasa. Sisi tulishatoka enzi za madisko ya kizamani kuondoka na mwanamme kitemi, siku hizi unaenda disko unachukua mwanamme kwa ushawishi au pesa yako. Hayo madisko ya ubabe wa kishamba tumewaachia washamba wa chattle.
Na hakuna chama cha siasa Tanzania kinachoweza kujenga hoja zaidi ya CCM.
 
Na hakuna chama cha siasa Tanzania kinachoweza kujenga hoja zaidi ya CCM.

Ukiona mtu yoyote anayetumia nguvu nyingi na akili kidogo jua hana uwezo wa kujenga hoja. Usisime ccm, sema jiwe maana yeye anawaburuza tu wanaccm, lakini yeye haswa ndio kaua uwezo mdogo uliokuwa umebakia wa kujenga hoja wa ccm. Pata picha kwenye mdahalo wa urais 2020 jiwe aingie kwenye mdahalo baina yake na Lissu, tena sio wa kiingereza uone kama atakubali. Sasa hivi haiba ya ccm haiko kwenye kujenga hoja, ila kwenye taswira ya chama cha mabavu zaidi kuliko uwezo wa ushawishi.
 
mkuu hata usijisikie vibaya kuitwa mbwiga, ni lugha ya kizaramo hiyo, kiswahili chake ni Rafiki.
Mkuu;
Samahani kama maana yake ni hiyo! Unajua tena taifa letu ni kubwa na lina makabila mengi na utamaduni tofauti!
 
Moderators ,tunaomba kama inawezekana muboreshe kwa kiasi kinachowezekana wakati wa kuunganisha mada,jaribuni kuweka alichoweka mleta mada wa kwanza na mnaunganisha na wa pili ili mtu akiingia anajua hii mada imeunganishwa na aliyeleta mada fulani, lakini kwa sasa unaingia unakuta mada imeanzia katikati yaani hata kuendelea unashindwa
 
Wewe tutolee kelele Hapa kapambaneni na Hali zenu mijitu inahujumiana yenyewe kwanini yenyewe. Tukisema mnaiba kura mnasema uongo Mbona sasa mnaibiana wenyewe CCM Ukoo wa panyaaaa
 
Back
Top Bottom