Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Wewe tutolee kelele Hapa kapambaneni na Hali zenu mijitu inahujumiana yenyewe kwanini yenyewe. Tukisema mnaiba kura mnasema uongo Mbona sasa mnaibiana wenyewe CCM Ukoo wa panyaaaa
Mkuu;
kwani umelazimisha kuingia kwenye thread yangu na kusoma!

Wewe ndio unatakiwa uondoe kelele zako kwenye thread yangu!
 
Sidhani kama CCM watapoteza mitaa wakati chama kimevaa koti la serikali.

Rais ameifanya CCM ijisahau kuhusu ushindani, wanaccm sasa hivi wanahofu uchaguzi wa ndani kuliko uchuguzi wa nje..

Wana CCM wanaaamini ukipita ndani ya CCM umepita jumla (baba kasema) hivyo kuminya vyma vya upinzani madhara yake ndio haya CCM kupata wagombea wa hovyo hovyo na Taifa kuongozwa hovyo hovyo.

Rais kupata wasaidizi wa ovyo, ambao hawawezi hata kutatua mgogoro wa kiwanja cha hatua mbili mpaka Rais aje ndio wananchi watoe malalamiko yao.

Na hili linaenda hadi kwenye wabunge, watu wanaanda fedha nyingi za rushwa ndani chama sababu wanaamini ukipita ndani ccm umepita Kitaifa NEC yetu na Polis ni wetu (baba kasema)

Hili swala lipo mikononi mwa Rais akiamua mfumo wa baba kasema ufanye kazi ni yeye akiamua demokrasia ifanye kazi ni yeye.

Wananchi tupo pembeni tunamwangalia yeye na chama chake wanavyofanya, ndio maana hata kwenye kujiandikisha wengi tulikaa pembeni tuangalie mnavyofanya maana kila kitu kipo ndani ya uwezo wenu.

Hakuna la kuwashinda.!
Mkuu shukurani kwa uchambuzi wako. Sina nyongeza kwani umegusa kila kitu.
 
Mkuu;
Kwanza, Mimi sikugombea na sitegemei kugombea nafasi ndani ya chama chochote cha siasa nchini.

Pili, zoezi kwa ujumla limeenda vibaya sana utajua ninayosema kama ukiuuliza watu wa vyombo vya usalama ndani ya CCM!
Hapa mtaani kwangu huyu mama wa ccn mliyetuwekea hatumtaki. Tutahakikisha mpinzani anapita.

Baada ya mwenyekiti wa mtaa kufariki, huyu mama aliteuliwa kushikiria nafasi ya mwenyekiti. Mambo aliyotufanyia Ni ya hovyo Sana, yeye kazi yake Ni kukaa kilimani bar hapa kwa mzee wa TRA na kunywa pombe muda wote. Ukiwa na shida ya kiofisi, anataka umfuate bar, muda wote ofisi yake imefungwa.

sio mfuatiliaji kabisa wa Mambo ya mtaa wetu lakini tuta hakikisha hapiti. Tunajua kua amehonga hela kupitishwa.
 
Huku kwetu uswàhilini ati kashinda muhindi! Kwakweli hii ni dharau iliyopita kiasi. Huyo muhindi hata mjumbe wake tu hamjuwi, njaa mbayà sana.
Inashangaza sana kwa yanayoendelea kwenye zoezi hili!
 
Back
Top Bottom