Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Kwenye hii mada yako kuna sehemu umeeleza kitu cha msingi Sana.
"Dhana ya wanaccm wengi ni kuwa ukichaguliwa Tu kupeperusha bendera ya CCM basi umeshinda uchaguzi"
Huku mtaani vita iliyopo ni ccm Kwa ccm na Hilo ni Jambo Baya Sana Kwa mustakabali wa chama chenu cha kishamba.
Vita vya CCM kwa CCM ni vibaya sana kwa sababu vinakifanya chama kidhoofika lakini kikubwa zaidi kutoa viongozi ambao ni wapenda rushwa na wasiokuwa wanaCCM kamilifu.
 
Hakuna kitu kama hicho!

Hii dhana unayosema hata mwaka 2014/2015 tulikuwa tunaambiwa lakini kilichotokea wapinzani walipata viti vingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Mkuu wangu zama unayozungumza ilishapita na vitabu vyake hii ni zama nyingine kabisa
 
Hivi ndivyo itakavyokua;

MKURUGENZI:
Mgombea Y wa tawala kapata kura 50,
Mgombea X wa pinzani kapata kura 100.

Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Y wa tawala ndiye mshindi.

WASIKILIZAJI:
Aaaaaaaaaaa...! Kivipiiiii...

POLISI (wanaingia):

Jamhuri ya Muungano ya Watu. Mnaamuriwa kutawanyika mara moja...
Kisha mabomu yanarindima kila kona kama mvua...

CHAMA OYEEE!
 
Zoezi la kuchagua wagombea kwenye serikali za mitaa kupitia tiketi ya CCM limekuwa ni mizengwe na vurugu za kujitakia ambazo zimesababishwa na Kanuni za Uchaguzi zisizoendana na mzingira ya sasa.

Mipango waliyobuni ya kuchuja majina ya wagombea na kuyatangaza siku ambayo ndiyo zoezi la uchaguzi linafanyika yamekuwa ni kituko na chanzo cha vurugu kwa sababu kinachofanyika ni baadhi ya wagombea kuenguliwa kimizengwe na vikao vya Kata na wilaya kwa lengo la kuweka wagombea ambao wengi wao hawakubaliwi kwa wanaCCM wengi.

WanaCCM wanapoingia kwenye chumba cha kupigia kura husomewa majina ya wagombea ambao hawakubaliwi na kuanza kulazimishwa kuwapigia kura!

Kwa akili za kawaida, CCM ya Dkt. Bashiru kama mtendaji Mkuu ilitakiwa ijue matatizo kama haya yangetokea kwa sababu rushwa na upendeleo ndani ya CCM bado upo hasa katika ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata na Wilaya.

Dkt. Bashiru Ally na sekretalieti yake walitakiwa wajue ili kupunguza rushwa na upendeleo, majina ya walioomba kuchaguliwa kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM yangerudishwa yote kwa wanaCCM ili wayapigie kura na sio vikao vya kata na wilaya viwaamulie nani wa kupigiwa kura. Hii Kanuni ya Uchaguzi haifai kwa mazingira ya sasa.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ‘’uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’. Kwa maamuzi haya mabovu ya Dkt. Bashiru na sekretalieti yake yamekaribisha mafisi na mainzi kugombea uongozi wa serikali za mitaaa kwa tiketi ya CCM.

Dhana inayojengwa kwa sasa kuwa ukichaguliwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM basi utakuwa umeishashinda uchaguzi inachochea rushwa na mizengwe ndani ya CCM.

Kwa mazingira haya hata ahadi namba 4 ya mwanachama wa CCM inayosema, ‘Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’ imebaki kwenye makaratasi!

Vyama vya upinzani walijua kitakachotokea ndani ya CCM ndio maana havijateua wagombea wake vikisubiri zoezi la CCM limalizike ili vianze kuvuna/kupokea wanaCCM ambao hawakutendewa haki kutokana na ubovu wa zoezi la uchaguzi ndani ya CCM.

Viongozi wakuu wa CCM wanatakiwa kujua hili zoezi limeharibika sana na linatakiwa kurudiwa upya nchi nzima!

Kama Viongozi Wakuu wa CCM watashupaza shingo kuhusu zoezi hili basi wategemee CCM kuvunjika ghafula, wala haitapata dawa!
CCM maana yake ni RUSHWA, songombingo, adakaadabr na mengine kama hayo, usitegemee jema lolote kama wao wanaiba kura za wapinzani tangu 1995
 
Mkuu;
Hii uliyoandika hapa ni nadharia tu na mbinu za kisiasa ili kuua morally ya kundi jingine lisiende kupiga kura!

Hakuna kitu kama hicho mbele ya nguvu za umma!
 
Watashindwa na nani wakati mlikuwa mnashinda humu mnawashawishi wanachama na wafuasi wasijiandikishe kupiga kura? Pia ujue angalau CCM ilikuwa na utararibu. Na kasoro hazihepukiki na zinazorekebishika, CCM wameishaanza kuzifanyia kazi. Vipi kuhusu Chadema, CUF, ACT na wengineo. Walikuwa na utaratibu hani "mzuri" wa kuchagua wagombea wao?
 
Naitabiria ACT WAZALENDO kuibuka kidedea kila kona ya nchi...Kwa wanasiasa wangesoma upepo na kujiunga na Zitto kwasasa.
Namtabiria Nabii Tito kuwa Naibu Spika wa Bunge lijalo.
tapatalk_1571921669725.jpeg
 
Watashindwa na nani wakati mlikuwa mnashinda humu mnawashawishi wanachama na wafuasi wasijiandikishe kupiga kura? Pia ujue angalau CCM ilikuwa na utararibu. Na kasoro hazihepukiki na zinazorekebishika, CCM wameishaanza kuzifanyia kazi. Vipi kuhusu Chadema, CUF, ACT na wengineo. Walikuwa na utaratibu hani "mzuri" wa kuchagua wagombea wao?
Chadema tumeshamaliza chaguzi za wagombea tunasubiria mpambano. Hata tusipotangazwa washindi lakini tumetimiza wajibu wetu na vigezo na masharti tuliyojiwekea vilizingatiwa.
 
Sidhani kama ccm watapoteza mitaa wakati chama kimevaa koti la serikali.

Rais ameifanya ccm ijisahau kuhusu ushindani, wanaccm sasa hivi wanahofu uchaguzi wa ndani kuliko uchuguzi wa nje..

Wana ccm wanaaamini ukipita ndani ya ccm umepita jumla (baba kasema) hivyo kuminya vyma vya upinzani madhara yake ndio haya ccm kupata wagombea wa hovyo hovyo na Taifa kuongozwa hovyo hovyo.

Rais kupata wasaidizi wa ovyo, ambao hawawezi hata kutatua mgogoro wa kiwanja cha hatua mbili mpaka Rais aje ndio wananchi watoe malalamiko yao.

Na hili linaenda hadi kwenye wabunge, watu wanaanda fedha nyingi za rushwa ndani chama sababu wanaamini ukipita ndani ccm umepita Kitaifa NEC yetu na Polis ni wetu (baba kasema)

Hili swala lipo mikononi mwa Rais akiamua mfumo wa baba kasema ufanye kazi ni yeye akiamua demokrasia ifanye kazi ni yeye.

Wananchi tupo pembeni tunamwangalia yeye na chama chake wanavyofanya, ndio maana hata kwenye kujiandikisha wengi tulikaa pembeni tuangalie mnavyofanya maana kila kitu kipo ndani ya uwezo wenu.

Hakuna la kuwashinda.!
Umechambua kama. Tangu nianze kusoma michango yako hapa jukwaani, nadhani huu ndo mchango best
 
Naitabiria ACT WAZALENDO kuibuka kidedea kila kona ya nchi...Kwa wanasiasa wangesoma upepo na kujiunga na Zitto kwasasa.
Sikubaliani na angalizo lako.

ACT-Wazalendo ina makelele kwenye mitandao ya kijamii lakini kwenye uwanja hasa wa mapambano hawapo.

Ukiishi kwenye mitandao ya kijamii unaweza kudhani ACT-Wazalendo ndio chama kikuu cha upinzani lakini ukienda kwenye uwanja wa mapambano ya kisiasa kuna maeneo mengi hawajui kama kuna chama kinaitwa ACT-Wazalendo!

CHADEMA bado kitaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani hata kwenye serikali za mitaa baada ya uchaguzi ujao.
 
CCM maana yake ni RUSHWA, songombingo, adakaadabr na mengine kama hayo, usitegemee jema lolote kama wao wanaiba kura za wapinzani tangu 1995
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa!

Rushwa ndani ya CCM inasababishwa hasa na dhana kuwa ukipitishwa kuwa mgombea basi unakuwa umeshinda uchaguzi hata kwa kuwezeshwa!
 
Zoezi la kuchagua wagombea kwenye serikali za mitaa kupitia tiketi ya CCM limekuwa ni mizengwe na vurugu za kujitakia ambazo zimesababishwa na Kanuni za Uchaguzi zisizoendana na mzingira ya sasa.

Mipango waliyobuni ya kuchuja majina ya wagombea na kuyatangaza siku ambayo ndiyo zoezi la uchaguzi linafanyika yamekuwa ni kituko na chanzo cha vurugu kwa sababu kinachofanyika ni baadhi ya wagombea kuenguliwa kimizengwe na vikao vya Kata na wilaya kwa lengo la kuweka wagombea ambao wengi wao hawakubaliwi kwa wanaCCM wengi.

WanaCCM wanapoingia kwenye chumba cha kupigia kura husomewa majina ya wagombea ambao hawakubaliwi na kuanza kulazimishwa kuwapigia kura!

Kwa akili za kawaida, CCM ya Dkt. Bashiru kama mtendaji Mkuu ilitakiwa ijue matatizo kama haya yangetokea kwa sababu rushwa na upendeleo ndani ya CCM bado upo hasa katika ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata na Wilaya.

Dkt. Bashiru Ally na sekretalieti yake walitakiwa wajue ili kupunguza rushwa na upendeleo, majina ya walioomba kuchaguliwa kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM yangerudishwa yote kwa wanaCCM ili wayapigie kura na sio vikao vya kata na wilaya viwaamulie nani wa kupigiwa kura. Hii Kanuni ya Uchaguzi haifai kwa mazingira ya sasa.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ‘’uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’. Kwa maamuzi haya mabovu ya Dkt. Bashiru na sekretalieti yake yamekaribisha mafisi na mainzi kugombea uongozi wa serikali za mitaaa kwa tiketi ya CCM.

Dhana inayojengwa kwa sasa kuwa ukichaguliwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM basi utakuwa umeishashinda uchaguzi inachochea rushwa na mizengwe ndani ya CCM.

Kwa mazingira haya hata ahadi namba 4 ya mwanachama wa CCM inayosema, ‘Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’ imebaki kwenye makaratasi!

Vyama vya upinzani walijua kitakachotokea ndani ya CCM ndio maana havijateua wagombea wake vikisubiri zoezi la CCM limalizike ili vianze kuvuna/kupokea wanaCCM ambao hawakutendewa haki kutokana na ubovu wa zoezi la uchaguzi ndani ya CCM.

Viongozi wakuu wa CCM wanatakiwa kujua hili zoezi limeharibika sana na linatakiwa kurudiwa upya nchi nzima!

Kama Viongozi Wakuu wa CCM watashupaza shingo kuhusu zoezi hili basi wategemee CCM kuvunjika ghafula, wala haitapata dawa!
Kabisa ni ukweli usiopingika kuwa CCM wanatengeneza tatizo la ndani litakalo wagharimu kukosa kura na kuwagawa wapiga kura kwenda upande wa pili.
Mfano:
Katika mji wa kibaha kuna mtaa mmoja ambao Wana CCM wamegawanyika kwa Udini waislamu na wa wakristo wa catholic hilo limepelekea mka catholic kushinda kwa sababu wa kristo wamama wamempigia kura lakini ni mama mzee wa miaka 65.
Kwa hili tu wamegawanyika makundi mawili CCM catholic na CCM Islam lakini vijana wote hawapo tayari kumpigia bibi kura wanadhani hafai kuwaongoza walimtaka mwana CCM kijana ambaye ameangushwa kwasababu ya uislamu.

Mtaa wenyewe ni mtaa wenye changamoto kubwa ukiangalia 60% ni vijana kuanzia 15-30 ni ngumu kumuweka mstaafu mwanamke kuongoza hili kundi lenye ushawishi na mambo mbalimbali.

CCM katika wanakosea sana.
 
Back
Top Bottom