Kama CCM wataendelea na Urasimu huu, wategemee kupoteza mitaa na vijiji vingi!

Vita vya CCM kwa CCM ni vibaya sana kwa sababu vinakifanya chama kidhoofika lakini kikubwa zaidi kutoa viongozi ambao ni wapenda rushwa na wasiokuwa wanaCCM kamilifu.
 
Hakuna kitu kama hicho!

Hii dhana unayosema hata mwaka 2014/2015 tulikuwa tunaambiwa lakini kilichotokea wapinzani walipata viti vingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Mkuu wangu zama unayozungumza ilishapita na vitabu vyake hii ni zama nyingine kabisa
 
Hivi ndivyo itakavyokua;

MKURUGENZI:
Mgombea Y wa tawala kapata kura 50,
Mgombea X wa pinzani kapata kura 100.

Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Y wa tawala ndiye mshindi.

WASIKILIZAJI:
Aaaaaaaaaaa...! Kivipiiiii...

POLISI (wanaingia):

Jamhuri ya Muungano ya Watu. Mnaamuriwa kutawanyika mara moja...
Kisha mabomu yanarindima kila kona kama mvua...

CHAMA OYEEE!
 
CCM maana yake ni RUSHWA, songombingo, adakaadabr na mengine kama hayo, usitegemee jema lolote kama wao wanaiba kura za wapinzani tangu 1995
 
Mkuu;
Hii uliyoandika hapa ni nadharia tu na mbinu za kisiasa ili kuua morally ya kundi jingine lisiende kupiga kura!

Hakuna kitu kama hicho mbele ya nguvu za umma!
 
Watashindwa na nani wakati mlikuwa mnashinda humu mnawashawishi wanachama na wafuasi wasijiandikishe kupiga kura? Pia ujue angalau CCM ilikuwa na utararibu. Na kasoro hazihepukiki na zinazorekebishika, CCM wameishaanza kuzifanyia kazi. Vipi kuhusu Chadema, CUF, ACT na wengineo. Walikuwa na utaratibu hani "mzuri" wa kuchagua wagombea wao?
 
Chadema tumeshamaliza chaguzi za wagombea tunasubiria mpambano. Hata tusipotangazwa washindi lakini tumetimiza wajibu wetu na vigezo na masharti tuliyojiwekea vilizingatiwa.
 
Umechambua kama. Tangu nianze kusoma michango yako hapa jukwaani, nadhani huu ndo mchango best
 
Naitabiria ACT WAZALENDO kuibuka kidedea kila kona ya nchi...Kwa wanasiasa wangesoma upepo na kujiunga na Zitto kwasasa.
Sikubaliani na angalizo lako.

ACT-Wazalendo ina makelele kwenye mitandao ya kijamii lakini kwenye uwanja hasa wa mapambano hawapo.

Ukiishi kwenye mitandao ya kijamii unaweza kudhani ACT-Wazalendo ndio chama kikuu cha upinzani lakini ukienda kwenye uwanja wa mapambano ya kisiasa kuna maeneo mengi hawajui kama kuna chama kinaitwa ACT-Wazalendo!

CHADEMA bado kitaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani hata kwenye serikali za mitaa baada ya uchaguzi ujao.
 
CCM maana yake ni RUSHWA, songombingo, adakaadabr na mengine kama hayo, usitegemee jema lolote kama wao wanaiba kura za wapinzani tangu 1995
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa!

Rushwa ndani ya CCM inasababishwa hasa na dhana kuwa ukipitishwa kuwa mgombea basi unakuwa umeshinda uchaguzi hata kwa kuwezeshwa!
 
Kabisa ni ukweli usiopingika kuwa CCM wanatengeneza tatizo la ndani litakalo wagharimu kukosa kura na kuwagawa wapiga kura kwenda upande wa pili.
Mfano:
Katika mji wa kibaha kuna mtaa mmoja ambao Wana CCM wamegawanyika kwa Udini waislamu na wa wakristo wa catholic hilo limepelekea mka catholic kushinda kwa sababu wa kristo wamama wamempigia kura lakini ni mama mzee wa miaka 65.
Kwa hili tu wamegawanyika makundi mawili CCM catholic na CCM Islam lakini vijana wote hawapo tayari kumpigia bibi kura wanadhani hafai kuwaongoza walimtaka mwana CCM kijana ambaye ameangushwa kwasababu ya uislamu.

Mtaa wenyewe ni mtaa wenye changamoto kubwa ukiangalia 60% ni vijana kuanzia 15-30 ni ngumu kumuweka mstaafu mwanamke kuongoza hili kundi lenye ushawishi na mambo mbalimbali.

CCM katika wanakosea sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…