Sidhani kama CCM watapoteza mitaa wakati chama kimevaa koti la serikali.
Rais ameifanya CCM ijisahau kuhusu ushindani, wanaccm sasa hivi wanahofu uchaguzi wa ndani kuliko uchuguzi wa nje..
Wana CCM wanaaamini ukipita ndani ya CCM umepita jumla (baba kasema) hivyo kuminya vyma vya upinzani madhara yake ndio haya CCM kupata wagombea wa hovyo hovyo na Taifa kuongozwa hovyo hovyo.
Rais kupata wasaidizi wa ovyo, ambao hawawezi hata kutatua mgogoro wa kiwanja cha hatua mbili mpaka Rais aje ndio wananchi watoe malalamiko yao.
Na hili linaenda hadi kwenye wabunge, watu wanaanda fedha nyingi za rushwa ndani chama sababu wanaamini ukipita ndani ccm umepita Kitaifa NEC yetu na Polis ni wetu (baba kasema)
Hili swala lipo mikononi mwa Rais akiamua mfumo wa baba kasema ufanye kazi ni yeye akiamua demokrasia ifanye kazi ni yeye.
Wananchi tupo pembeni tunamwangalia yeye na chama chake wanavyofanya, ndio maana hata kwenye kujiandikisha wengi tulikaa pembeni tuangalie mnavyofanya maana kila kitu kipo ndani ya uwezo wenu.
Hakuna la kuwashinda.!