Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Utasemaje walighushi bila kuona barua zilizowasilishwa NEC na Bunge? Kama kuna kughushi hizo taasisi ndio zinazopaswa kuchukua hatua, sio lazima Chadema.
Mambo ya sheria tuwaachie wana sheria. Ni beyond uelewa wako na wangu.

Amandla...

Nadhani bado haujanisaidia.
 
Kwanini NEC nao hawajatoa uthibitisho wa barua kutoka CDM kuwa iliwateua hao 19?
CDM ilijuaje kuwa Nusrat Hanje ataachiwa gerezani usiku,siku Moja kabla ya kuapishwa hadi wakamteua kwenye hao 19?
Kuna foul play na Iko so obvious!
Nafikiri NEC wangekuwa washtakiwa wa kwanza kwakuwa zoezi la kutuma majina kwa Spika lazima walihusika.
 
Kwanini NEC nao hawajatoa uthibitisho wa barua kutoka CDM kuwa iliwateua hao 19?
CDM ilijuaje kuwa Nusrat Hanje ataachiwa gerezani usiku,siku Moja kabla ya kuapishwa hadi wakamteua kwenye hao 19?
Kuna foul play na Iko so obvious!
Its obvious wanatufanya ss wajinga,atleast tungewafahamisha we ar not stupid that much, CHADEMA, CCM wote wale wale,magenge ya wahuni wanaocheza na maisha ya Watanzania
 
Siku ile ya kuapishwa Halima aliposema anamshukuru Mwenyekiti kwa kuwaruhusu kwenda bungeni, nilijua Mbowe ana mkono wake pale.

Dalili zote zinaonyesha Mbowe anajua hatua kadhaa za kina Mdee kwenda bungeni, na kuna viashiria vyote kuwa ana uhusika kwenye hilo. Japo suala la kumtoa Nusrat Hanje gerezani usiku na namna wabunge hao walivyoapishwa linaacha alama ya mshangao. Kwa vyovyote serikali ina mkono wake kwa uwepo wa kina Mdee huko bungeni, na Mbowe anajua jambo fulani la uwepo wao huko bungeni kwa faida yake binafsi.
 
Nadhani bado haujanisaidia.
Hata wewe unaweza kwenda kuwashitaki tu. Si na wewe ni Mtanzania?

Kama wewe ni CHADEMA, jitahidi upeleke taarifa polisi ili wakamatwe na uende kuwa shahidi wa Jamhuri kesho huko mahakamani!

Unaandika tu kana kwamba hujui siasa na justice system ya Tanzania ilivyo very compromised hususani mara tu Jiwe alipoingiaga madarakani mpaka leo na baada ya kufa kwake ndiyo mdogo mdogo healing imeanza kutokea...

Na kumbuka hili mazee;

Siasa za Bongo ni lazima uende kwa mkakakati na siyo kwenda kichwa kichwa tu. CHADEMA wanajua wafanyavyo. Kwa muda tusiodhania, wahusika watajinyonga wenyewe bila hata kupelekwa mahakamani. Wenzako hawaendi kichwa kichwa tu kwa kelele zenu...

Na pia kumbuka, hakuna jinai inayoozaga. Kama kuna kughushi, obvious litajulikana tu kwa wakati wake na wahusika popote watakapokuwa watawajibika kwa makosa yao...
 
Heshima sana wanajamvi,

Ikiwa Mdee na genge lake waligushi nyaraka na hatimaye wakafanikiwa kuwa wabunge !.

Ni kwanini mpaka leo chadema hawajawafunguliwa Mdee na wenzake kesi ya kugushi !.

Ikiwa Wakili Msomi Kibatala na wenzake walijua kama mapingamizi yao yangesababisha kesi ya Mdee kutupwa lakini hapo hapo walikuwa na nafasi ya kufanya marekebisho na kesi kuanza upya. Hawakuona walikuwa wanatoa nafasi ya kesi kuchukua muda mrefu zaidi ?.

Nadhani kuna shida hapa lakini hatuambiwi ukweli.

Ngongo kwasasa Kigali.
Chadema siyo Serikali ya JMT

Baada ya Mnyika kuzikana zile fomu ilibidi police ndio wamkamate na kumuhoji
 
Hata wewe unaweza kwenda kuwashitaki tu. Si na wewe ni Mtanzania?

Kama wewe ni CHADEMA, jitahidi upeleke taarifa polisi ili wakamatwe na uende kuwa shahidi wa Jamhuri kesho huko mahakamani!

Unaandika tu kana kwamba hujui siasa na justice system ya Tanzania ilivyo very compromised hususani mara tu Jiwe alipoingiaga madarakani mpaka leo na baada ya kufa kwake ndiyo mdogo mdogo healing imeanza kutokea...

Na kumbuka hili mazee;

Siasa za Bongo ni lazima uende kwa mkakakati na siyo kwenda kichwa kichwa tu. CHADEMA wanajua wafanyavyo. Kwa muda tusiodhania, wahusika watajinyonga wenyewe bila hata kupelekwa mahakamani. Wenzako hawaendi kichwa kichwa tu kwa kelele zenu...

Na pia kumbuka, hakuna jinai inayoozaga. Kama kuna kughushi, obvious litajulikana tu kwa wakati wake na wahusika popote watakapokuwa watawajibika kwa makosa yao...

Mimi ni mwanaCCM kindaki ndaki.
 
Utasemaje walighushi bila kuona barua zilizowasilishwa NEC na Bunge? Kama kuna kughushi hizo taasisi ndio zinazopaswa kuchukua hatua, sio lazima Chadema.
Mambo ya sheria tuwaachie wana sheria. Ni beyond uelewa wako na wangu.

Amandla...
Mahakamani ndio sehemu nzuri ya kujua kila kitu. Kina Halima walijua vizuri mgogoro utaishia mahakamani na watapata nafasi ya kuwasilisha utetezi wao bila mihemko ya mashabiki nnya wa Chadema
 
Kwanini NEC nao hawajatoa uthibitisho wa barua kutoka CDM kuwa iliwateua hao 19?
CDM ilijuaje kuwa Nusrat Hanje ataachiwa gerezani usiku,siku Moja kabla ya kuapishwa hadi wakamteua kwenye hao 19?
Kuna foul play na Iko so obvious!
Ukijibiwa hii unitag.
 
Dalili zote zinaonyesha Mbowe anajua hatua kadhaa za kina Mdee kwenda bungeni, na kuna viashiria vyote kuwa ana uhusika kwenye hilo. Japo suala la kumtoa Nusrat Hanje gerezani usiku na namna wabunge hao walivyoapishwa linaacha alama ya mshangao. Kwa vyovyote serikali ina mkono wake kwa uwepo wa kina Mdee huko bungeni, na Mbowe anajua jambo fulani la uwepo wao huko bungeni kwa faida yake binafsi.
Ina maana Mbowe amekula njama na Serikali tena enzi za Magufuli kuwapeleka kina Halima bungeni? Hadi leo Serikali inamlinda Mbowe siri hiyo isibainike? Serikali hii hii iliyomuweka ndani miezi kadhaa kwa tuhuma za ugaidi mbali na madhila mbali mbali aliyotendewa na dola?

Basi uhusiano wa Mbowe na Serikali lazima utakuwa wa kushangaza sana. Kwa upande mmoja amejenga chama cha siasa kinachotikisa na kutishia mustakabali wa “establishment”. Kwa upande mwingine Mbowe ni mshirika wa Serikali anaisaidia kuhujumu upinzani! A bizarre paradox!
 
Mahakamani ndio sehemu nzuri ya kujua kila kitu. Kina Halima walijua vizuri mgogoro utaishia mahakamani na watapata nafasi ya kuwasilisha utetezi wao bila mihemko ya mashabiki nnya wa Chadema
Kesi yao ni kuhusu kuvuliwa uanachama na si suala ubunge wao. Sitegemei kama watawasilisha chochote kipya kuhusu wao kuingia bungeni. Kingekuwepo, kingeisha wasilishwa zamani na Bunge/NEC ili kuwaumbua Chadema. Hizi ni delaying tactics za kuwaongezea muda wa kukaa Bungeni na pengine kwa mtazamo wao kuwakomoa Chadema. Siamini kama wana nia ya dhati ya kubakia Chadema baada ya yote haya.

Amandla...
 
Wewe nae maswali yako mepesiii,Sasa kwanini Ccm wamteue Nusrat Hanje na yuko gerezani hakukuwa na wengine wenye akili kwenye hicho Chama?
Yaani wewe ndio mbuzimawe kweli kweli. Hukujua kuwa ccm inatafuta legitimacy kwa namna yoyote? Kwanini sasa hata mahakama kuu ilipotupilia mbali madai yao hadi sasa bado wapo bungeni. Ile hukumu haikutosha kuwaondoa bungeni?
 
Heshima sana wanajamvi,

Ikiwa Mdee na genge lake waligushi nyaraka na hatimaye wakafanikiwa kuwa wabunge !.

Ni kwanini mpaka leo chadema hawajawafunguliwa Mdee na wenzake kesi ya kugushi !.

Ikiwa Wakili Msomi Kibatala na wenzake walijua kama mapingamizi yao yangesababisha kesi ya Mdee kutupwa lakini hapo hapo walikuwa na nafasi ya kufanya marekebisho na kesi kuanza upya. Hawakuona walikuwa wanatoa nafasi ya kesi kuchukua muda mrefu zaidi ?.

Nadhani kuna shida hapa lakini hatuambiwi ukweli.

Ngongo kwasasa Kigali.

..inawezekana wameteuliwa kwa MAAGIZO tu na hakuna nyaraka zozote za uteuzi wao.

..wangekuwa wameteuliwa na Cdm basi tume na bunge wangekuwa wameshatoa ushahidi wa kuthibitisha hilo.
 
Back
Top Bottom