Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Ukweli ulio rahisi kueleweka ni kwamba Mbowe alikuwa anajua kila kitu na aliruhusu kutumiwa kwa nyaraka original za chama.
Hizo nyingine ni porojo za kawaida za chadema.
 
Kuna mahali au tuseme hatua za kuchukua ambazo chama kilitakiwa kuzifuata ikiwemo kutoa taarifa kwa taasisi husika eg Polisi,Tume ya uchaguzi na nk.

Ninachokiona ni chama kushanbuliwa na wakosaji badala ya wakosaji kushambuliwa na chama.
Watapeleka ushahidi upi ulioghushiwa ikiwa Tume na Bunge walikataa kutoa barua zilizodaiwa kuandika na Mnyika?
 
..inawezekana wameteuliwa kwa MAAGIZO tu na hakuna nyaraka zozote za uteuzi wao.

..wangekuwa wameteuliwa na Cdm basi tume na bunge wangekuwa wameshatoa ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Ina maana Serekali inaweza kufanya uhuni wa kiwango hiki !.
 
Siku ile ya kuapishwa Halima aliposema anamshukuru Mwenyekiti kwa kuwaruhusu kwenda bungeni, nilijua Mbowe ana mkono wake pale.
Mkono upi? Utaratibu lazima Kamati kuu kipitishe maamuzi na majina anapeleka Katibu Mkuu toka lini Mwenyekiti anapeleka majina so ilipaswa NEC wayakatae!!

Kingine Baraza kuu limewatimua sasa whether Mbowe aliwatuma or not inatuhusu nini wanachama?
 
Ukweli ulio rahisi kueleweka ni kwamba Mbowe alikuwa anajua kila kitu na aliruhusu kutumiwa kwa nyaraka original za chama.
Hizo nyingine ni porojo za kawaida za chadema.
Na serikali inamfichia siri Mbowe asiadhirike. Halafu ilikubali “ombi lake” la kumteua Nusrat na kumtoa jela Singida usiku chap chap akaapishwe Dodoma asubuhi kesho yake. Ndani ya awamu ya tano na ya sita! 🤔
 
Kuna mahali au tuseme hatua za kuchukua ambazo chama kilitakiwa kuzifuata ikiwemo kutoa taarifa kwa taasisi husika eg Polisi,Tume ya uchaguzi na nk.

Ninachokiona ni chama kushanbuliwa na wakosaji badala ya wakosaji kushambuliwa na chama.
Mkongwe unadhani kipindi kile chá jiwe ni nani ambaye yupo tayar kushughika na kufungua kesi za chadema?
 
Heshima sana wanajamvi,

Ikiwa Mdee na genge lake waligushi nyaraka na hatimaye wakafanikiwa kuwa wabunge !.

Ni kwanini mpaka leo chadema hawajawafunguliwa Mdee na wenzake kesi ya kugushi !.
...

Nadhani kuna shida hapa lakini hatuambiwi ukweli.

Ngongo kwasasa Kigali.

Badala yake kila kukicha viongozi wa CHADEMA wanakimbilia kwenye vyombo vya habari kulaani. Hata jana wameongea na Wanahabari kuhusu sakata la hao Wabunge wakati kesi iko mahakamani. Msikilize Naibu Katibu Mkuu Bara.

AIBU
 
Kesi ya kughushi ni jinai inafunguliwa na Jamhuri.
Aksante kwa kujibu vizuri, inasikitisha kuona jamii kubwa ya watanzania wasio na uelewa wa vitu uongea tena kwa kujiamini kweli.

Tujifunze kuuliza kabla ya kuanika udhaifu wetu, "forgery" ni kesi ya jinai, wenye jukumu la kufungua kesi ni Jamhuri Chadema walishaeleza kuwa hawazitambui nyaraka zilizowapa uhalali hao wabunge kuwa bungeni, Jamhuri ilitakiwa kufanya uchunguzi na kufungua mashtaka.

Nakubali pia mtu binafsi wa mazingira na maombi maalum anaweza kupata kibali cha kuendesha kesi ya jinai mahakamani, lakini kwa kuangalia tu namna Jamhuri ilivyo kimya kwenye mzozo huu sidhani kama kibali kitatoka.​
 
Mahakamani ndio sehemu nzuri ya kujua kila kitu. Kina Halima walijua vizuri mgogoro utaishia mahakamani na watapata nafasi ya kuwasilisha utetezi wao bila mihemko ya mashabiki nnya wa Chadema

Kama mahakama zingekuwa na credibility hiyo, wala akina Halima wasingejiingiza kwenye zoezi la kuforge. Kwakuwa wanajua mahakama ni sehemu ya kuagizwa nini ifanye kwa utashi wa serikali, hivyo wanaweza kuitumia mahakama kwenye huo uhuni.
 
Kesi yao ni kuhusu kuvuliwa uanachama na si suala ubunge wao. Sitegemei kama watawasilisha chochote kipya kuhusu wao kuingia bungeni. Kingekuwepo, kingeisha wasilishwa zamani na Bunge/NEC ili kuwaumbua Chadema. Hizi ni delaying tactics za kuwaongezea muda wa kukaa Bungeni na pengine kwa mtazamo wao kuwakomoa Chadema. Siamini kama wana nia ya dhati ya kubakia Chadema baada ya yote haya.

Amandla...
Hao wabunge 19, hawaikomoi chadema hizo hekaheka zao zipo katika kulinda maslahi ya matumbo yao tu. Halima na wenzie wanajua kuwa wakipoteza sifa ya kuwa wanachama basi na ubunge wao utafika kikomo.

Kama ulivyosema hawa hawana mapenzi ya dhati na chama, ila naongezea kuwa wanahangaika kulinda nafasi zao tu.​
 
Badala yake kila kukicha viongozi wa CHADEMA wanakimbilia kwenye vyombo vya habari kulaani. Hata jana wameongea na Wanahabari kuhusu sakata la hao Wabunge wakati kesi iko mahakamani. Msikilize Naibu Katibu Mkuu Bara.

AIBU

Huna ujualo mzee, kesi haikuwa mahakamani kwani ilishatupiliwa mbali. Na kwa jinsi mahakama ilivyopoteza credibility yake, sioni kama kuna haja ya kuheshimu tena kuwa kesi iko mahakamani hivyo isiongelewe.
 
Kesi yao ni kuhusu kuvuliwa uanachama na si suala ubunge wao. Sitegemei kama watawasilisha chochote kipya kuhusu wao kuingia bungeni. Kingekuwepo, kingeisha wasilishwa zamani na Bunge/NEC ili kuwaumbua Chadema. Hizi ni delaying tactics za kuwaongezea muda wa kukaa Bungeni na pengine kwa mtazamo wao kuwakomoa Chadema. Siamini kama wana nia ya dhati ya kubakia Chadema baada ya yote haya.

Amandla...

Hakuna uwezekano wa wao kubaki tena CDM bila kujali kitakachotokea kwenye hii kesi. Wale wanaotegemea siasa moja kwa moja watahamia vyama vingine hasa CCM ili kuendelea kupata ulaji. Na wengine nadhani itakuwa ni mwisho wa siasa kwao, au hata kama watabaki kwenye siasa watakuwa wamepoteza ushawishi.
 
Najua mnaogopa ila kesi ya kuvuliwa uanachama inaenda sambamba na sababu ya kuvuliwa uanachama. Mdee na wenzake wataweka kila kitu wazi kuanzia barua ya kwenda bungeni alisaini nani mpaka baraka alizotoa Mbowe watazisema wamekaa kimya mmewahukumu subirini na wao waongee mtaficha sura zenu mashabiki wa Mbowe
 
Mkono upi? Utaratibu lazima Kamati kuu kipitishe maamuzi na majina anapeleka Katibu Mkuu toka lini Mwenyekiti anapeleka majina so ilipaswa NEC wayakatae!!

Kingine Baraza kuu limewatimua sasa whether Mbowe aliwatuma or not inatuhusu nini wanachama?
kuna watu wanaandika vitu mpaka unafikiri huyu ana akili timamu kweli? Yaani Mbowe kukana, Wahusika kina Mdee hawajawahi kumtaja Mbowe, Serikali wala CCM haijawahi hata kuja hadharani kumtuhumu Mbowe, Kamati Kuu na Baraza la Chama hakukuwa na hiyo hoja. Halima na washenzi wenzie walikuwa pale.
Halafu anakuja bwege anasema ana baraka za Mbowe
 
Najua mnaogopa ila kesi ya kuvuliwa uanachama inaenda sambamba na sababu ya kuvuliwa uanachama. Mdee na wenzake wataweka kila kitu wazi kuanzia barua ya kwenda bungeni alisaini nani mpaka baraka alizotoa Mbowe watazisema wamekaa kimya mmewahukumu subirini na wao waongee mtaficha sura zenu mashabiki wa Mbowe
Tuliambiwa tutaficha sura zetu ushahidi utakapowekwa wazi kuthibitisha kuwa Mbowe ni gaidi. Nani aliyeficha sura ? Hii nayo itakuwa hivyo hivyo! Yaani Ndugai awe na barua ya kuthibitisha kuwa Mnyika au Mbowe walitoa baraka zake na aifiche kwa sababu anawapenda sana Chadema!

Amandla...
 
Hakuna uwezekano wa wao kubaki tena CDM bila kujali kitakachotokea kwenye hii kesi. Wale wanaotegemea siasa moja kwa moja watahamia vyama vingine hasa CCM ili kuendelea kupata ulaji. Na wengine nadhani itakuwa ni mwisho wa siasa kwao, au hata kama watabaki kwenye siasa watakuwa wamepoteza ushawishi.
Kweli kabisa ingawa sidhani kama watahamia CCM maana huko bado watu wanawachukia. Watahamia ACT Wazalendo au vyama vingine kama hicho. Wengine watapewa vyeo vya kiutendaji kama RC, DC, wakurugenzi, wajumbe wa bodi n.k. Wengine ndio itakuwa mwisho kweli wa safari yao, wataendelea na vitega uchumi vyao watakavyokuwq wameanzisha katika wakati huu wa mavuno.

Amandla...
 
Back
Top Bottom