Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Wakina Halima watabaki Bungeni kwa sababu moja tu. Kinachowalinda ni haja ya Bunge kuwa na wapinzani wa kutosha kuweza kuipa uhalali. Siku Chadema wakiwahakikishia CCM kuwa wako tayari kuteua wabunge watakaochukua nafasi yao watakuwa history. Spika atasahau mambo ya Mahakama na atawafurumusha bila huruma.
Haya ya Mahakama ni delaying tactics ili Bunge libaki na legitimacy hadi 2025 ambapo itahakikishwa kuwa kuna kambi ya wapinzani bungeni.

Amandla...
Nguruvi3 JokaKuu
 
Yaani wewe ndio mbuzimawe kweli kweli. Hukujua kuwa ccm inatafuta legitimacy kwa namna yoyote? Kwanini sasa hata mahakama kuu ilipotupilia mbali madai yao hadi sasa bado wapo bungeni. Ile hukumu haikutosha kuwaondoa bungeni?
Wew kweli ni kitimoto upo tu unafukua ila hujui unafukua nini,madai yao yalitupiliwa mbali au waliambiwa wakarekebishe makosa yao kwenye hilo jarada.
Si unaona wamerudi mahakamani na watashindwa Tena wataambiwa wakarekebishe,watarudi watakosea Tena mpaka 2025 muda wao ukiisha
 
Sijasikia zaidi ya Katibu Mkuu kushangilia ushindi wa masaa machache.

Kama utaniwekea andiko nitashukuru.
Ndugu,
Ninadhani ukiacha ushabiki nawe ukachimba, utaweza kupata ukweli zaidi ya kuridhika na kutegemea vya kusikia TU.
Nina hakika, NEC wangekuwa na barua na forms za uteuzi zilizoidhinishwa na CHADEMA wangeishaziweka hadharani.
Pia NEC wanalindwa na sheria 'mbovu' zilizopo na wamekuwa wakiombwa nakala ya hizo barua/forms wanakaa kimya.
Ila kwa kesi tunaweza kuja kumfahamu nani haswa aliyegushi ili kuwapa ubunge covid 19. Amen
 
Kwanini NEC nao hawajatoa uthibitisho wa barua kutoka CDM kuwa iliwateua hao 19?
CDM ilijuaje kuwa Nusrat Hanje ataachiwa gerezani usiku,siku Moja kabla ya kuapishwa hadi wakamteua kwenye hao 19?
Kuna foul play na Iko so obvious!
NEC si wale wale? Vipi Chadema? Mambo ya Tom & Jerry ...
 
Utasemaje walighushi bila kuona barua zilizowasilishwa NEC na Bunge? Kama kuna kughushi hizo taasisi ndio zinazopaswa kuchukua hatua, sio lazima Chadema.
Mambo ya sheria tuwaachie wana sheria. Ni beyond uelewa wako na wangu.

Amandla...
Chadema ingetaka isingekosa njia za kimahakama kulazimisha NEC wadhibitishe!
 
Heshima sana wanajamvi,

Ikiwa Mdee na genge lake waligushi nyaraka na hatimaye wakafanikiwa kuwa wabunge !.

Ni kwanini mpaka leo chadema hawajawafunguliwa Mdee na wenzake kesi ya kugushi !.

Ikiwa Wakili Msomi Kibatala na wenzake walijua kama mapingamizi yao yangesababisha kesi ya Mdee kutupwa lakini hapo hapo walikuwa na nafasi ya kufanya marekebisho na kesi kuanza upya. Hawakuona walikuwa wanatoa nafasi ya kesi kuchukua muda mrefu zaidi ?.

Nadhani kuna shida hapa lakini hatuambiwi ukweli.

Ngongo kwasasa Kigali.
Acha nikae kimya
 
Preliminary objections (POs) ambazo hazina uwezo wa kuimaliza kesi huwa ni mkenge wa kisheria wa kupoteza muda. Mara nyingi, PO ambayo huwa inakuwa ya maana ni ya jurisdiction. Kama mahakama ikikubaliana na mwenye PO kwamba haina mamlaka ya kusikiliza hilo shauri, mlalamikaji hawezi kurudi tena kwenye mahakama hiyo. Labda akate rufaa na kushinda, in which case mahakama ya chini itaamriwa kusikiliza hilo shauri.
 
Kesi yao ni kuhusu kuvuliwa uanachama na si suala ubunge wao. Sitegemei kama watawasilisha chochote kipya kuhusu wao kuingia bungeni. Kingekuwepo, kingeisha wasilishwa zamani na Bunge/NEC ili kuwaumbua Chadema. Hizi ni delaying tactics za kuwaongezea muda wa kukaa Bungeni na pengine kwa mtazamo wao kuwakomoa Chadema. Siamini kama wana nia ya dhati ya kubakia Chadema baada ya yote haya.

Amandla...
Wanaowaunga mkono akina Mdee hawana nia yoyote ya kuwatetea. Hawa ni wale AMBAO kwa kipindi kirefu wanaopigana KUPANDIKIZA chuki ili kuibomoa CHADEMA kama walivyofanikiwa kungine NCCR, CUF.
Baada ya kupita na kushinda kipindi cha giza na udhalimu, CDM sasa iko imara kabisa. Kwa kukubali kutumiwa, akina dada hawa ambao baadhi yao walikuwa wameshajenga majina, ndio wameshajiua kabisa kisiasa. NDIO mwisho wao.
 
Utasemaje walighushi bila kuona barua zilizowasilishwa NEC na Bunge? Kama kuna kughushi hizo taasisi ndio zinazopaswa kuchukua hatua, sio lazima Chadema.
Mambo ya sheria tuwaachie wana sheria. Ni beyond uelewa wako na wangu.

Amandla...

Utaziona; ni matter ya process tu. Utaanza kwa kuandika barua kwenda NEC kukanusha madai kwamba CHADEMA iliwasilisha NEC majina ya wanachama wake ili wateuliwe kuwa wabunge wa viti maalumu. NEC watajibu hiyo barua na, most likely, wataambatanisha nakala ya barua ya CHADEMA iliyowawezesha wao kuendelea na taratibu zingine za kukamilisha mchakato wa kuteua wabunge wa viti maalumu kwa mujibu wa sheria.
 
Najua mnaogopa ila kesi ya kuvuliwa uanachama inaenda sambamba na sababu ya kuvuliwa uanachama. Mdee na wenzake wataweka kila kitu wazi kuanzia barua ya kwenda bungeni alisaini nani mpaka baraka alizotoa Mbowe watazisema wamekaa kimya mmewahukumu subirini na wao waongee mtaficha sura zenu mashabiki wa Mbowe

..hata kama mbowe aliwashawishi VIKAO vimekataa kina Halima kwenda bungeni.

..wabunge wa viti maalum wa Cdm huteuliwa na kuthibitishwa na kikao cha KAMATI KUU.

..kwa msingi huo Halima na wenzake wako bungeni kinyume na utaratibu wa chama.
 
Unataka Chadema ifungue kesi ya kughushi wakati document iliyogushiwa hawana??? Vipi kama hakuna kabisa document iliyoghishiwa lakini kwa mchongo NEC aliamua kuandika barua kwa Bunge akiwatambulisha akina Mdee kama wabunge??

Usidhani Chadema ni wajinga! Unaweza tu kusema kuna ughushi kama una document inayoonesha hivo!! Inawezekana kabisa hakuna document iliyotoka Chadema - hata serikali/NEC/Bunge sio wajinga kama jambo zima likikuwa la mchongo!!
 
Utaziona; ni process tu. Utaanza kwa kuandika barua kwenda NEC kukanusha madai kwamba CHADEMA iliwasilisha NEC majina ya wanachama wake ili wateuliwe kuwa wabunge wa viti maalumu. NEC watajibu hiyo barua na, most likely, wataambatanisha nakala ya barua ya CHADEMA iliyowawezesha wao kuendelea na taratibu zingine za kukamilisha mchakato wa kuteua wabunge wa viti maalumu kwa mujibu wa sheria.

..hakuna kikao cha KAMATI KUU ya Cdm kilichoketi na kuwapitisha kina Halima kwenda bungeni.

..Kamati Kuu ndio inayotoa go ahead kwa Katibu Mkuu kutekeleza taratibu za Nec za uteuzi wa viti maalum.

..Maadam Kamati Kuu haikuketi basi uteuzi wa kina Halima sio halali na ndio maana chama kimewafukuza.

..Lakini upo uwezekano wa kina Halima kuwa wameteuliwa kwa MAAGIZO ya watu wa serikali na hakuna documentation yoyote iliyotumika mpaka kuwaapisha.

..Inawezekana hata NEC hawakuhusika bali kina Halima walikwenda moja kwa moja bungeni na kuapa.
 
Unataka Chadema ifungue kesi ya kughushi wakati document iliyogushiwa hawana??? Vipi kama hakuna kabisa document iliyoghishiwa lakini kwa mchongo NEC aliamua kuandika barua kwa Bunge akiwatambulisha akina Mdee kama wabunge??

Usidhani Chadema ni wajinga! Unaweza tu kusema kuna ughushi kama una document inayoonesha hivo!! Inawezekana kabisa hakuna document iliyotoka Chadema - hata serikali/NEC/Bunge sio wajinga kama jambo zima likikuwa la mchongo!!

..inawezekana Nec hawakushiriki ktk suala la kina Halima.

..huenda yalitoka MAAGIZO waende bungeni kuapa na wao wakafanya hivyo.

Cc Pascal Mayalla, Nguruvi3
 
Unataka Chadema ifungue kesi ya kughushi wakati document iliyogushiwa hawana??? Vipi kama hakuna kabisa document iliyoghishiwa lakini kwa mchongo NEC aliamua kuandika barua kwa Bunge akiwatambulisha akina Mdee kama wabunge??

Usidhani Chadema ni wajinga! Unaweza tu kusema kuna ughushi kama una document inayoonesha hivo!! Inawezekana kabisa hakuna document iliyotoka Chadema - hata serikali/NEC/Bunge sio wajinga kama jambo zima likikuwa la mchongo!!

CHADEMA hawajawahi kufanya mawasiliano yoyote rasmi na NEC baada ya Mdee, et al kutangazwa na NEC kuwa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA?
 
..hakuna kikao cha KAMATI KUU ya Cdm kilichoketi na kuwapitisha kina Halima kwenda bungeni.

..Kamati Kuu ndio inayotoa go ahead kwa Katibu Mkuu kutekeleza taratibu za Nec za uteuzi wa viti maalum.

..Maadam Kamati Kuu haikuketi basi uteuzi wa kina Halima sio halali na ndio maana chama kimewafukuza.

..Lakini upo uwezekano wa kina Halima kuwa wameteuliwa kwa MAAGIZO ya watu wa serikali na hakuna documentation yoyote iliyotumika mpaka kuwaapisha.

..Inawezekana hata NEC hawakuhusika bali kina Halima walikwenda moja kwa moja bungeni na kuapa.
Halima alikuwa Mwenyekiti wa Bawacha , anajua taratibu zote kama vile mamlaka za uteuzi wa Wabunge

Iwe kwa namna yoyote ile, kupitia Bunge, NEC au ushiriki wa viongozi binafsi wa Chadema hoja kuu ya kisheria ni kuwa Uteuzi haukufuata taratibu. period. Hapa ndipo Pascal Mayalla anapopotosha umma
Kwamba ingalikuwa CCM basi Shaka akiteua Wabunge anaojua yeye hao wanakuwa 'bonafide'' misleading ya ajabu sana.

Nawaelewa Chadema, hili suala linatafutiwa namna ya ku prolong sasa ukianza uchunguzi wa nani amefoji watafika 2025. Hiki ndicho akina Halima wanataka. Chadema wanataka kwenda straight to the point kwamba uteuzi ni haramu na hapo kesi inaisha asubuhi.
 
CHADEMA hawajawahi kufanya mawasiliano yoyote rasmi na NEC baada ya Mdee, et al kutangazwa na NEC kuwa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA?

..according to Mnyika Cdm wamewahi kuandika barua Nec kuomba nyaraka zilizotumika kuwateua kina Mdee.

..wanadai Nec hawajawapa ushirikiano ktk hilo.

..ninahisi kina Halima walikwenda moja kwa moja kwa Spika na kuapishwa kwa MAAGIZO tu bila kupitia Nec.
 
..hakuna kikao cha KAMATI KUU ya Cdm kilichoketi na kuwapitisha kina Halima kwenda bungeni.

..Kamati Kuu ndio inayotoa go ahead kwa Katibu Mkuu kutekeleza taratibu za Nec za uteuzi wa viti maalum.

..Maadam Kamati Kuu haikuketi basi uteuzi wa kina Halima sio halali na ndio maana chama kimewafukuza.

..Lakini upo uwezekano wa kina Halima kuwa wameteuliwa kwa MAAGIZO ya watu wa serikali na hakuna documentation yoyote iliyotumika mpaka kuwaapisha.

..Inawezekana hata NEC hawakuhusika bali kina Halima walikwenda moja kwa moja bungeni na kuapa.

Speculations zote hizi za nini? Taratibu za kuteua na kutangaza wabunge wa viti maalumu zinafahamika.

Ina maana CHADEMA hawajawahi kufanya mawasiliano yoyote rasmi na NEC baada ya Mdee na wenzake kutangazwa (au kuapishwa) kuwa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA?
 
Back
Top Bottom