Kama chanzo cha uhai kinaweza kubadilika basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti hadi sasa. Je, ni upi msingi wa uhai?

Dhana nzima ya chanzo inahitaji muktadha. Kutumia neno chanzo bila muktadha, hata wa kukubali tu kuwa kauli hiyo ina uthabiti kiasi gani na margin of error gani, na imetoka katika epistemology gani, ni kujiwekea uhakika usiokuwepo.

Kwa mfano, katika epistemology ya dini ya Kijristo chanzo cha maisha ni Mungu.

Lakini, katika epistemology ya kisayansi kauli hii haina mashiko.
 
Mada nzuri na fikirishi,... ila tatizo ni kwamba inajadili vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa Binadamu kuweza kuthibitisha uhalisia wake maana kwa mfano tukisema upo sahihi ulivyosema kwamba Mungu sio msingi wa uhai,. tutakuomba uthibitisho kuhusu hilo,. kisha tutakuomba utuambie kama Mungu sio msingi wa uhai, Je msingi wa uhai ni nini? na uthibitisho wa huo msingi wa uhai upo wapi au tutaufahamu vipi? .......

Hivyo kimsingi kadri tunavyochimba mada hii,. tutajikuta tunapata maswali mengi zaidi kuliko majibu.
 
Usichanganye ukweli kwamba, on the one hand, elimu kuhusu chanzo cha uhai inaweza kubadilika na on the other hand, chanzo cha uhai kuweza kubadilika.

Hayo ni mambo mawili tofauti.

Unaweza kuishi mpaka ukafikisha miaka 50 bila ya kumjua baba yako wa kibaiolojia ni nani, ukafikiri baba yako mlezi ndiye baba yako wa kibaiolojia.

Halafu kwenye birthday yako ya kufikisha miaka 50, ukajua kuwa huyu baba yako mlezi si baba wako wa kibaiolojia, una baba mwingine wa kibaiolojia.

Badiliko hili katika ujuzi wako halimaanishi baba yako wa kibaiol9jia amebadilika, linamaanisha kuwa ujuzi wako kuhusu nani ni baba yako wa kibaiolojia ndio umebadilika.

Usichanganye mawili hayo.
 
Nijibu swali la Msingi wa Uhai wako.....

Kwa Ufupi kwa mujibu na macho ya nature (Uhai wako ni wewe kutumia nishati unenepe, ili uwe chakula cha Specie nyingine) in short wewe ni part ya recycle ya Nishati, Kufa kwako au kuondoka kwako (hata specie kwa ujumla wake) kutakuwa hakuna massive effect ya viumbe vingine; Ukizingatia wewe Binadamu ni Kama Kirusi tu kwa viumbe wengine (The most destructive Specie) Case in Point kipindi cha lock down kuna viumbe vilishangilia sana na kujinafasi...


View: https://youtu.be/1E_vdNiTlgg?si=vUUUyvQtojs-wWlM
 
Nasubii kwa hamu na shauku kubwa mleta mada kurudi kutula msingi wa maisha au uhai.

Ukweli ni mada uliyo ileta ambayo inaacha tafakari kubwa sana ndani mwetu juu haswa ya nini maana ya maisha , msingi wake na chanzo na mantiki.

Vitu kama hivi huwezi kuvipata katika sehemu zetu za imani maana huko tunefungiwa kwenye boksi la imani hatupaswi kuhoji wala kudadisi ila kusadiki tu.

Hii imetulemaza sana na kutuweka sehemu kiasi cha kujiita watumwa au tusio kuwa huru wala tusio jua mantiki ya maisha na jinsi gani tufanye maisha yawe bora.

Natanguliza shukrani kwa mada hii.
 
Hili andiko nimeliandika baada ya kuona hilo neno chanzo limetumika kwenye maandiko almost yote badala ya neno msingi na ndio maana ukilisoma hili andiko utaona limekaa sana kwenye muktadha wa kidini kuliko wa kisayansi ila pia dhima hii hii tukiirudisha upande huo wa kisayansi lazima kuna pahala tutafika na kustack.

Kwahiyo ili tuweze kuchanganya mawazo labda tungeweza kulijibu hili swali kwa mtindo wa kukosoana kwa hoja ili pande zote mbili ziingie labda ndani ya hoja hizo tunaweza kupata pahala pa kuanzia kwenda kuujua ukweli halisi wa jambo hili.
 
Na hapo kwenye maswali mengi ndio kutakua na uelekeo mzuri wa kuivunja vunja hii puzzle iweze kua kwenye vyanzo mbalimbali vya msingi ambavyo labda kama tukiendelea kuvichambua tunaweza kupata msingi
 
Ni kweli mkuu, ila tujadilini wote ili tuweze kuisolve hii equation πŸ˜…πŸ˜…
 
Mkuu samahan je wewe ni dini gani
Mkuu Mimi naamini uwepo wa mamlaka yenye nguvu kuliko sisi, kwahiyo mtu yeyote ambae anaamini uwepo wa hiyo mamlaka bila kujali yuko upande gani Mimi nafungamana nae, iwe wa msikitini, wa kanisani, kilingeni na kadhalikaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…