Dhana nzima ya "chanzo" si ya msingi wala ukweli. Ni dhana ya kufikirika na ina maana katika muktadha fulani tu.
Kimsingi chanzo kinategemea chronology, time, cause and effect.
These things are not real. They are not absolute.
Time is relative. One has to only read Einstein's Relativity to know that.
Cause and effect are not always synchronous, one has to only read quantum physics to know that.
If you can travel at the speed of light in a vacuum, the flow of time ceases to exist. In fact, from the perspective of a ray of light in a vacuum, the flow of time does not exist.
Everything, the past, the present, the future, happens at once.
So in reality, time appears to pass because of our position in the universe, because of the fact that we do not move as fast as light in a vacuum.
So time is not absolute, it is an illusion that appears because of the increasing entropy of the universe due to the second law of thermodynamics.
So, if time is not real, chanzo, which depends on causality and time, is also not real.
We can only speak of "chanzo" in relative terms. Not in absolute terms.
Hoja kwamba muda si kitu halisi kwa sababu ya nadharia ya Uhusiano wa Einstein na hiyo Relativity theory yake pamoja na fizikia ya Quantum kwa maana ya Quantum Mechanics, ni sahihi kwa muktadha wa kisayansi, kwamba ni kweli mwanga unasafiri bila kufuata mtiririko wa muda kwa mtazamo wake, na ni kweli pia kuwa sababu na matokeo yaani cause and effect hayafuati utaratibu wa kawaida katika kiwango cha quantum.
Lakini nikuulize mkuu, je, hii hoja yako inamaanisha kwamba muda haupo kabisa kwa hali zote?
Kwasababu tukiangalia katika uhalisia wa kila siku, muda ni jambo lenye athari kwa wanadamu, na ndio maana ulivyokua miaka 20 iliyopita sivyo ulivyo leo, na hii inamaanisha kutokea kuzaliwa, hadi kuzeeka na hadi kufa ni kwamba muda umetumika, kwasababu wewe na Mimi wote ni mashahidi ya kwamba mabadiliko haya yote yana mwelekeo fulani kwa maana ya kwamba haubaki kama ulivyo (ndio maana mtoto huanza kuzalia, anajifunza kukaa chini, anatambaa, kisha kusimama na kutembea, hivi vyote hutokea baada ya muda fulani).
Kwahiyo ingawa nadharia za kisayansi zinaonyesha kuwa muda ni wa mlinganisho kwa maana ya relative, lakini hii haiwezi kuwa sababu ya kutufanya tuukane kabisa katika maisha yetu ya kawaida, hivyo basi, kwakua chanzo ni kitu kinachotegemea sana muda na uhusiano huo wa kisababishi basi si sahihi kusema eti chanzo ni kitu ambacho hakipo kabisa.
Na hapa wacha niseme hivi, ya kwamba chanzo kinaweza kuwa hakipo katika uhalisia wa juu kabisa kwa maana ya ultimate reality, lakini ni kitu ambacho kipo katika uhalisia wetu wa kawaida kwa maana ya practical reality na sidhani kama unapingana na hii hoja.
Ila kama hiyo haitoshi, basi chukulia mfano huu, tunaposema "mimi ni chanzo cha furaha yako," hatumaanishi kwamba hakuna hali nyingine inayoweza kuleta furaha ila tunamaanisha kuwa katika mazingira fulani, uhusiano wa kisababishi upo, na ndio maana chanzo kina maana katika muktadha huo lakini chanzo hiki kinaweza kubadilika baadae (naongelea juu ya muda kaka).
Na kama wewe bado utaendelea kupinga chanzo kwa misingi ya nadharia ya uhusiano au Quantum Mechanics, basi pia unapaswa kukana dhana ya maisha ya kila siku, pamoja na effect zake (na sidhani kama unaweza kufanya hivyo).
Kwa hiyo, badala ya kukana kabisa uwepo wa chanzo, ni bora tukubali kwamba ni dhana inayotegemea muktadha, iwe ni katika maisha ya kila siku, falsafa, au imani za kidini, kwahiyo rudi katika mada na tuendelee kujadili chanzo cha uhai ni nini katika muktadha ambao andiko limelenga.
Tusijibane kwenye kaeneo fulani kadogo na kujinyima uwanda mpana wa Kutafakari juu ya mambo fulani fulani, embu tujipe uhuru wa Kutafakari kwanza halafu tuone tunaweza kufikia wapi.