Kama chanzo cha uhai kinaweza kubadilika basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti hadi sasa. Je, ni upi msingi wa uhai?

Chanzo kinaingia kwenye muktadha wowote wa kilimwengu mkuu.

Na ikiwa tunazungumzia chanzo ndani ya ulimwengu wetu wa asili, basi lazima tukubali kuwa muda na causality vina nafasi.

Ila ikiwa tunatafuta chanzo absolute kisichotegemea muda wala causality, basi tunazungumzia kitu ambacho kiko nje ya upeo wa uelewa wetu wa kawaida.

Kwa hivyo, swali la kuwa, tunajadili chanzo cha nini na ndani ya mfumo gani? Litakua mjadala mzito kama utaendelea kubaki kwenye msimamo wako ila kwa muktadha wa kilimwengu huwezi kupingana na hoja iliyopo.
 
Ujaelewa alpha na omega ili neno.
Wewe sio elimu za kundalini sana kuhusu jicho la tatu.
 
Hii hoja yako ndio uijenge kwa kuelezea kwa kina kama ambavyo Mimi nimeelezea kwenye uzi, ya kwamba kwa namna gani jambo linaweza kuwa na chanzo pasipo kuwa na msingi?

Lakini pia hauwezi kujua msingi wa msingi wa uhai ni nini wakati vilivyopo ni vyanzo, na wala tusingejadili msingi wa uhai kama vyanzo vyake visingezungumziwa.

Kwahiyo tupo hapa kwasababu tumekua tukiona vyanzo tu, na andiko limejikita hapo kwakuelezea chanzo na msingi na sababu za kwanini tujadili msingi wa uhai.
 
Unajuaje chanzo kinaingia kwenye muktadha wowote wa ulimwengu?

Katika muktadha wa ulimwengu ambao hauna chanzo, ni cyclic, there is cause A, which has effect B, but also the effect B is the cause of the cause A, hapo kati ya A na B chanzo ni nini?
 
Swali lako linagusa dhana za kina kuhusu maisha, fahamu, na ukweli wa kuwepo kwa uhai. Hebu tuchambue sehemu kuu:

1. Alpha na Omega

Hizi ni dhana za mwanzo na mwisho, zinazoashiria ukamilifu wa uwepo. Katika maandiko ya kidini na kifalsafa, “Alpha” inawakilisha chanzo, mwanzo wa kila kitu, na “Omega” ni mwisho wa kila kitu. Ikiwa tunahusisha na uhai, tunaweza kusema kuwa uhai una mwanzo (kuzaliwa) na mwisho (kufa), lakini je, kuna hali ya kudumu nje ya haya mawili?

2. Jicho la Tatu na Kundalini

• Jicho la Tatu linahusiana na fahamu ya juu, kuona ukweli wa mambo bila kutumia macho ya kawaida. Katika falsafa ya Kihindu, linahusishwa na tezi ya pineal, ambayo inadaiwa kuwa kituo cha kiroho na uwezo wa kuona zaidi ya ulimwengu wa kimwili.

• Kundalini ni nishati ya maisha inayodhaniwa kuwa inalala chini ya uti wa mgongo na inapowekwa huru kupitia mwamko wa kiroho, inaweza kuleta mabadiliko ya fahamu.

Ikiwa nishati ya kundalini ndiyo chanzo cha uhai, basi tunahoji: Je, nishati hii inaweza kubadilika? Ikiwa inawezekana kubadilika, basi inamaanisha kuwa hakuna msingi wa uhai ulio thabiti, kwani msingi wake unategemea hali zinazoweza kubadilika.

3. Je, Uhai Una Msingi Thabiti?

• Ikiwa uhai ni nishati inayobadilika, basi hauna msingi wa kudumu, lakini unategemea hali zinazobadilika.

• Ikiwa uhai una chanzo thabiti, basi tunahitaji kuelewa chanzo hicho—je, ni akili, nishati, au kitu kingine?

Katika falsafa na sayansi:

• Sayansi inasema uhai umetokana na michakato ya kibaolojia na kemikali.

• Falsafa ya Kiroho inasema uhai ni fahamu, nguvu ya kiungu, au nishati isiyokufa.
 
Hii hoja yako ndio uijenge kwa kuelezea kwa kina kama ambavyo Mimi nimeelezea kwenye uzi, ya kwamba kwa namna gani jambo linaweza kuwa na chanzo pasipo kuwa na msingi?
Kuna vitu vingi vipo, vinatokea vina chanzo lakini havina msingi.

Mfano ajali.

Ajali haina msingi wa kutokea, Bali ajali ina chanzo cha kutokea kwake. kama vile uzembe wa dereva, mwendokasi, ulevi, barabara mbovu n.k

Sasa unaona kwamba ajali ina chanzo, Lakini hakuna msingi wowote unaosababisha vyanzo mbalimbali vya ajali.
Lakini pia hauwezi kujua msingi wa msingi wa uhai ni nini wakati vilivyopo ni vyanzo, na wala tusingejadili msingi wa uhai kama vyanzo vyake visingezungumziwa.
Hakuna msingi wa kila kitu, ila kuna vyanzo mbalimbali vya kitu.

Hakuna msingi wa uhai, Kuna vyanzo vya uhai.
Kwahiyo tupo hapa kwasababu tumekua tukiona vyanzo tu, na andiko limejikita hapo kwakuelezea chanzo na msingi na sababu za kwanini tujadili msingi wa uhai.
Chanzo sio lazima kiwe na msingi.

Ndio maana hata Ajali husababishwa na vyanzo mbalimbali bila msingi wowote ule.
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho wa andiko na maoni yake.
Nafurahi kuona watu wanauelewa mkubwa
 
Unajuaje chanzo kinaingia kwenye muktadha wowote wa ulimwengu?

Katika muktadha wa ulimwengu ambao hauna chanzo, ni cyclic, there is cause A, which has effect B, but also the effect B is the cause of the cause A, hapo kati ya A na B chanzo ni nini?
Hapa wewe unazungumzia chanzo katika dhana ya cyclic causality wakati Mimi mifano mingi niliyoitoa hapo juu imejikita kwenye linear causality.

Kwenye namna hizi mbili dhana ya chanzo huwa katika namna tofauti na kwakua umekiri umejikita huko nadhani ndio maana hatubaki kwenye eneo moja.

Swala la chanzo cha uhai limekaa kilinear na si cyclic ndio maana wewe utazaa mwanao na mwanao atazaa mjukuu wako na mjukuu wako atazaa kitukuu wako na kizazi hiki kinaendelea hivyo na wala hakuna siku itatokea hii loop ikarudi ilipoanzia kwa maana ya kwamba kwenye hiko kizazi hakuna mtu atarudi kukuzaa tena wewe na wewe ukarudi kuwazaa tena wale wale watoto wako, nao wakazaa tena wajukuu zako, na ingekua hivi basi kusingekua na haja ya kujadili hili swala.

Kwasababu mambo yangekua yanaenda na kujirudia, kwahiyo labda useme je hivi ndivyo ambavyo unahisi wewe ya kwamba chanzo cha uhai ni cyclic?
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho wa andiko na maoni yake.
Nafurahi kuona watu wanauelewa mkubwa
Kuna vitu vingi vina chanzo lakini hutokea bila msingi wowote ule.

Kwa hiyo sikweli kwamba msingi ndio mwanzo wa chanzo, Kama mleta mada anavyodai.
 
Lakini si ulisema chanzo kinaingia kwenye muktadha wowote wa ulimwengu?
 
Samaleko ... Umenikumbusha Falsafa za Dkt Adolf Mihanjo.

Falsafa na usanifu na hoja!
 
Ajali haina msingi wa kutokea, Bali ajali ina chanzo cha kutokea kwake. kama vile uzembe wa dereva, mwendokasi, ulevi, barabara mbovu n.k

Umejikita zaidi kwenye dhana ila haujaja kwenye mada halisi bado, isipokua umezidi kutengeneza puzzle juu ya puzzle na kuendelea kutupatia maswali yanayoendelea kuengeza uwanda mpana wa kuendelea kujadili.
 
Sio mzuri wa kuhandika ila elimu hii labda kama unataka kuelezewa kwa sauti.
Hata sayansi uwezi kuelewa unavyo tumia mfano hii teknolojia
 
Swala la ajali limenifanya nifikirie upya ila linaonekana linaweza kuingia kwenye mafungu yote kutokana na namna utakavyolichukulia, na hii ndio hufanya hii loop iendelee kurudi nyuma kuanzia hapo ilipo au kwenda mbele kutokea hapo ilipo.

Na kutokana na sababu hii basi pengine inapaswa turudi kwenye hoja ya Kiranga na tujiulize swali kwamba chanzo ni cyclic or linear?

Lakini kwa muktadha wa uhai tunapata jibu ya kwamba chanzo ni linear na kama ndivyo basi kwa kurudi nyuma tunaweza kukutana na msingi wake, sasa ni umbali kiasi gani tunapaswa kurudi hili ndio swali ambalo hufanya watu wengi wajipe majibu mepesi ya kurahisisha mambo ili kuepuka kuumiza kichwa kuendelea kuwaza zaidi.
 
Umejikita zaidi kwenye dhana ila haujaja kwenye mada halisi bado, isipokua umezidi kutengeneza puzzle juu ya puzzle na kuendelea kutupatia maswali yanayoendelea kuengeza uwanda mpana wa kuendelea kujadili.
Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.

We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of the mysteries we are trying to solve.
 
Lakini si ulisema chanzo kinaingia kwenye muktadha wowote wa ulimwengu?
Kwenye muktadha wowote ila katika Kila muktadha kuna namna ya kukielezea kulingana na hali ya jambo lenyewe.
 
Kwenye muktadha wowote ila katika Kila muktadha kuna namna ya kukielezea kulingana na hali ya jambo lenyewe.
Ungekuwa umesoma elimu ya atomic energy physics usinge kujakusumbua watu nahisi.
 
Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.

We cannot solve the ultimate mysteries of nature because we ourselves are the part of the mysteries we are trying to solve.
Hapa unajibana mkuu na kujipa excuse ya kurudi nyuma katika kuyafikira mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…