Kama Dangote kafunga mitungi ya gesi kwenye malori yake, Mimi ni nani hata nisibadili mfumo wa nishati ya gari yangu?

Kama Dangote kafunga mitungi ya gesi kwenye malori yake, Mimi ni nani hata nisibadili mfumo wa nishati ya gari yangu?

Kapicha plz
Jione mwenyewe mkuu

Ova

Screenshot_20210708-143858_YouTube.jpg

Screenshot_20210708-143907_YouTube.jpg
 
Ujinga wa hii kitu inamaliza nafasi kwenye buti ukishaweka utakuwa ukitoka Chunya au Tukuyu kuja Dar unaacha kubeba Mchele na maparachichi na mikungu ya ndizi...Na kingine huwa siamini kama Technology hiyo ni salama hasa pale gari linapopata ajali na kupinduka huwa nahisi kama mlipuko utkaotokea hapo si wa kitoto
Sawa malafyale
 
Mafuta yanapanda Bei Kila kukicha, kipato kinapungua kila kukicha.

Nimepita Ubungo, kituo cha kujaza natural kwenye magari (sheli, tuite hivyo ili nieleweke) nimekuta kg 1 ni shilling 1550.
Gharama za kubadili mfumo ni kama milioni moja na kidogo.

Jumamosi naipeleka gari ikabadilishwe mfumo, sitaki ujinga mimi
Halafu mkoani unaendaje??

Au inakuwa na mifumo miwili??
 
Mafuta yanapanda Bei Kila kukicha, kipato kinapungua kila kukicha.

Nimepita Ubungo, kituo cha kujaza natural kwenye magari (sheli, tuite hivyo ili nieleweke) nimekuta kg 1 ni shilling 1550.
Gharama za kubadili mfumo ni kama milioni moja na kidogo.

Jumamosi naipeleka gari ikabadilishwe mfumo, sitaki ujinga mimi
Shida yake ni moja tu...hiyo gari itakuwa ya Dar Es Salaam tu
 
Mkisha badilisha mifumo ya mafuta kwenye vibebi woka (Magari Ya Mtumba) vyenu na mkaweka mifumo ya gas. Mtuambie, ili sisi kama serikali ya chama pendwa ya CCM tutapandisha kodi maradufu za gas kutoka "KG 1 KWA 1550/Tsh" na kufikia "KG 1 KWA 3,500/Tshs".

Itakua fursa nzuri kwetu kuongeza makusanyo ya kodi ili kuendeleza miradi ya kimkakati, tuweze kufika uchumi wa juu kabisa kuliko ulaya. Kama tulivyoongeza kodi kwenye "KILIMO CHA UMWAGILIAJI".

CCM Hoyee!!! CCM Hoyeeeeeeeee!!! Makofi!!!
Hatari sana
 
Back
Top Bottom