Kama Dhahabu ni pesa, kwanini tupokee mgao wa makaratasi Badala ya Dhahabu?

Kama Dhahabu ni pesa, kwanini tupokee mgao wa makaratasi Badala ya Dhahabu?

Niliwahi kuandika haya kuhusu dhahabu yetu:
 
Ngoja tuone Madelu anayevaa tai ya Bendera ya Taifa 🇹🇿🇹🇿🇹🇿kama Ishara ya Uzalendo ataona Uzi huu na kupeleka ushauri kwenye Cabinet ya mawaziri!!
Hivi naweza kufungua account ya gold bars?
 
Zimbabwe imetengeneza sarafu ya Dhahabu yenye thamani sawa na USD 900 baada ya pesa Yao kutoimarika.

Sie Watanzania tumebinafsisha migodi yetu, wachimbe pesa Kisha kutupa mgao wa makaratasi, tena Kwa makadirio na wakati mwingine wanatangaza HASARA na kubadili Majina Ili kukwepa Kodi mf Kutoka Barrick kwenda Acacia 😳

Ikumbukwe kuwa tangu kuumbwa Kwa Dunia, Dhahabu haijawahi tetereka katika soko la Dunia.

Kununua Dhahabu Kutoka wachimbaji WADOGO Bado uzalishaji uko chini kutokana na uwekezaji wa Serikali chini ya Mamlaka husika kuzalisha na kuongeza ubora Kwa viwango vya kidunia.

Hivyo kuwaelekeza wafanyabiashara huko kununua Dhahabu Ili waende kuuza kupata dollar za kuagizia mafuta na bidhaa adimu, ni kukosa vision.

Botswana ni Nchi IPO hapa hapa Africa, wao wamebinafsiaha Dhahabu Yao Kwa wageni Kwa kupewa hisa ya 50%.

Sie Watanzania tunapewa mrabaha wa chini ya 20%, na mbaya zaidi tunalipwa cash Dhahabu inaenda.

Ikiwa kama Nchi tunaona uelekeo sahihi ni kununua Dhahabu Kwa wachimbaji wa ndani, kwanini tusianze na makampuni tuloyabinafsishia migodi Ili yatulipe mrabaha in terms of Gold na Si pesa cash?

Pia kwanini tusirudi mezani na kuhakikisha tunapata share ya 50+1% sababu sisi ndo wamiliki wa raslimali?

Na hiyo 50+1% Inatakiwa tupewe in terms of Gold iliyozalishwa Kwa ubora wa juu katika gold bars(vitofali).

Yaani tunaweka wazalendo kwenye Kila mgodi pale jikoni vinapitengenezwa vitofali yaani gold bars, moja letu, moja lao mwanzo mwisho.

Kwa kufanya hivyo, Nchi ingepata vitofali vingapi Kwa siku? Ni Dhahabu kiasi Gani inapelekwa nje ukizingatia wanafanya KAZI day and night?

Stamico kwanini haisitishi vibali vya utafiti na uchimbaji madini yetu Kwa makampuni ya nje Ili yenyewe iunde na kusimamia migodi itayochimba Dhahabu yetu na tukapata share kubwa zaidi?

Kwanini Benki kuu isianzishe SARAFU ya Dhahabu yenye ubora wa kimataifa Ili kuimarisha currency yetu ya Tshs?

Kwani madini yetu Mungu alitupa tuwagawie majirani au tulipewa yatutajirishe?

Watoto wanakaa chini wakati Dhahabu yetu inaenda kutajirisha wageni ambao hawakujaliwa raslimali hizo!!

Wazalendo wa Nchi wapo wapi?

Karibuni🙏
Cc Faiza fox, Meneja wa makampuni, Lord Denim, Kalamu.
Mkuu,mkuu hii dunia ya Biashara ina levels za iufanya mambo,kumbuka Magufuli aliwahi sema Mabebebru walishachukua gesi,na dhahabu ni hivyo hivyo.Imagine hata hilo unalosema ilitakiwa lifanyike kwenye dhahabu.
 
1 July 2023

Under the new deal announced on Friday, Botswana gets a bigger share of rough stones from their joint venture, Debswana.

Botswana and mining company De Beers have announced a new diamond sales deal.
View attachment 2709249
The new deal, concluded on Friday, gives Botswana a bigger share of rough stones from their joint venture.

Debswana, a joint venture between Anglo American unit De Beers and Botswana's government, sells 75% of its output to De Beers, with the balance taken up by state-owned Okavango Diamond Co.

The new agreement covers a 10-year sales deal for Debswana rough diamond production through to 2033 and 25-year Debswana mining licences.

In the run-up to Friday's deal, Botswana President Mokgweetsi Masisi, who is expected to seek re-election next year, had pushed De Beers for a bigger share of Debswana's output.

In March, Botswana announced it would take a 24% stake in Belgian gem processing firm HB Antwerp in a move seen as designed to loosen De Beers' grip on the country's gems.

Botswana supplies 70% of De Beers' rough diamonds
Botswana na Tanzania ni tofauti kama mjamzito na tasa! Very very different experience!
Niliwahi kuandika haya kuhusu dhahabu yetu:
Hivi hiyo ccm yenu inayapokea haya maoni??
 
Mawazo haya unayo wewe mkuu mwenye kulitakia mema Taifa, na sio kuitakia mema mifuko yako.
 
Tumempa ushauri wa bure kwake
Niwaambie ili tufike hapo 50/50 ni lazima tukomae Tuwe nchi ya Uchumi wa kati,kiukweli Magufuli alikuwa mtu mhimu mno,in fact ukiwa uchumi wa kati kuna profile inapanda katika nyanja za uchumi,watesi wakala kichwa
 
Mkuu,mkuu hii dunia ya Biashara ina levels za iufanya mambo,kumbuka Magufuli aliwahi sema Mabebebru walishachukua gesi,na dhahabu ni hivyo hivyo.Imagine hata hilo unalosema ilitakiwa lifanyike kwenye dhahabu.
Bt Kuna migodi na maeneo mengi Bado hayajawekezwa Kwa wageni.

Ndo tunamshauri maeneo hayo wasipewe wageni Hadi tubadili Katiba na SHERIA Ili tupate 50+1%
 
Bt Kuna migodi na maeneo mengi Bado hayajawekezwa Kwa wageni.

Ndo tunamshauri maeneo hayo wasipewe wageni Hadi tubadili Katiba na SHERIA Ili tupate 50+1%

Upi sahihi migodi mipya mikataba yake iwe ya magao wa mali kwa mali ya vitofali vya dhahabu


MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI 🇬🇭

Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.


Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.

Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.

Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.

Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.

View: https://m.youtube.com/watch?v=idU-ZxmfIMU
Source : JoyNews
 
Back
Top Bottom