- Thread starter
- #41
Upi sahihi migodi mipya mikataba yake iwe ya magao wa mali kwa mali ya vitofali vya dhahabu
MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI 🇬🇭
Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.
Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.
Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.
Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.
Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.
Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.
View: https://m.youtube.com/watch?v=idU-ZxmfIMU
Source : JoyNews
Ni Kweli kabisa ndugu bagamoyo,
Serikali Haina uwezo wa kuwalipa pesa nyingi zaidi ya wanayopata huko wanakopeleka sasa,
Wakijaribu njia hiyo, Yale ya korosho yanaweza Kutokea.