Kama Dhahabu ni pesa, kwanini tupokee mgao wa makaratasi Badala ya Dhahabu?

Ni Kweli kabisa ndugu bagamoyo,

Serikali Haina uwezo wa kuwalipa pesa nyingi zaidi ya wanayopata huko wanakopeleka sasa,

Wakijaribu njia hiyo, Yale ya korosho yanaweza Kutokea.
 
Niwaambie ili tufike hapo 50/50 ni lazima tukomae Tuwe nchi ya Uchumi wa kati,kiukweli Magufuli alikuwa mtu mhimu mno,in fact ukiwa uchumi wa kati kuna profile inapanda katika nyanja za uchumi,watesi wakala kichwa
Ndugu Magu alitufumbua macho na kutuaminisha kuwa inawezekana kukata minyororo ya unyonyaji inayodidimiza Africa katika Umaskini.

Magu mmoja amekufa, Bado tupo watz zaidi ya 60 ml ambao tunaweza kufanya zaidi ya alivyofanya Magu.

Mungu atusaidie.
 
Faiza yuko busy na bwana zake wa Walodi sidhani kama anaweze kutinga hapa
 
Ndugu bagamoyo ametoa HOJA muhimu hapa, kwamba:

1.Serikali inazo pesa za kununua Dhahabu ya wachimbaji WADOGO?

2. Na ikiwa inazo pesa, je inaweza Kutoa Bei ya juu kuliko huko wanakopeleka sasa wafanyabiashara WADOGO?

3. Na ikiwa itaamua kununua Kutoka makampuni makubwa Kutoka nje kama GGM au Acacia ,Je makampuni hayo yatakubali kupokea pesa za madafu kubadilishana na gold bars?

4. Pia naongezea, wafanyabiashara wa mafuta ikiwa watataka kununua Dhahabu Kutoka Acaccia au GGM, Serikali imeweka Utaratibu Gani Ili jambo Hilo liwezekane?

Karibu.
 
Wazo zuri
 
Faiza yuko busy na bwana zake wa Walodi sidhani kama anaweze kutinga hapa
Swali muhimu ni kuwa, Je inawezekana wafanya biashara wakubwa wa mafuta kutinga pale Acacia au GGM kununua Dhahabu Kwa pesa za madafu na ikawezekana?

Maana Kuna thread aliandika faizafox na Meneja wa makampuni wakishauri wafanyabiashara na Serikali kununua Dhahabu ya ndani!!
 
Huwezi kufanya terms of reference na mtu hajasomea economics ....its an insult bwana
 
Biashara inatakiwa iwe "fair and square". Tusitake kuunda kanuni mpya za biashara.
 
Botswana na Tanzania ni tofauti kama mjamzito na tasa! Very very different experience!

Hivi hiyo ccm yenu inayapokea haya maoni??
Sana tena sana.

Serikali inafanyia kazi mengi sana inayoshauriwa yenye kueleweka. Asiye na macho haambiwi tazama.
 
Mabeberu wameidhibiti dhahabu ndiyo maana hatufurukuti nayo...
 
Mabeberu wameidhibiti dhahabu ndiyo maana hatufurukuti nayo...
Basi tupige MARUFUKU vibali vipya vya uchimbaji.

Kampuni zetu chini ya stamico viwezeshwe, kikope kununua mashine za kisasa,

Sirikali ipata mgao wake, pia inunue na kutunza reserve.
 
Kwa Tanzania na jinsi tulivyo tunahitaji Rais mjeuri kama botswana wameweza sisi tunaongozwa na NG'OMBE au wasomi?
 
Basi tupige MARUFUKU vibali vipya vya uchimbaji.

Kampuni zetu chini ya stamico viwezeshwe, kikope kununua mashine za kisasa,

Sirikali ipata mgao wake, pia inunue na kutunza reserve.
Kuna vibali vinahusisha mabeberu ili uweze kua kwenye soko, tutakwama...

Mashine za kisasa na vipuli vyake vinatoka kwa hao mabeberu, tutakwama...

Kwenye mgao, tunapangiwa na mabebru, sababu mambo mengi ni kutoka kwao, hata soko la dunia la dhahabu wanaliendsha wao...
 
Kwa Tanzania na jinsi tulivyo tunahitaji Rais mjeuri kama botswana wameweza sisi tunaongozwa na NG'OMBE au wasomi?
Aje mjeuri mtenda HAKI pia akifuata KATIBA.
 
Kwa wachimbaji wadogo kwa kutumia madafu inaweza hata kununua kwa bei ya zaidi ya soko. Serikali haina shida wala uhaba wa madafu.
 
Kwa wachimbaji wadogo kwa kutumia madafu inaweza hata kununua kwa bei ya zaidi ya soko. Serikali haina shida wala uhaba wa madafu.
NB:Neno madafu limetumila kumaanisha pesa ya madafu au pesa ya Tshss. Pesa ya ndani.

Na ikinunua Kwa Bei ya juu kuliko huko duniani hiyo gold itakuwa ghali hivyo kukosa wa kumuuzia.

Balance inahitajika.
 
Kwa pesa ya ndani unaweza nunua kwa bei ya juu. Huko si unapata dola. Serikali haina shida wala uhaba na Tsh. Na si mpaka uongeze bei. Unaweza kutoa kodi.
 
Kwa pesa ya ndani unaweza nunua kwa bei ya juu. Huko si unapata dola. Serikali haina shida wala uhaba na Tsh. Na si mpaka uongeze bei. Unaweza kutoa kodi.
Ndo nasema, ukinunua Kwa Bei ya juu, Dhahabu hiyo itakuwa na gharama kubwa, hivyo ukitaka kuiuza nje ukakuta unapewa Bei ya offer ndogo kuliko gharama uliyonunulia Kwa kulinganisha na thamani ya dollar itakuwa HASARA na hutapata mteja, na ukimpata atakupa dollar chache.
 
Hujaelewa. Dhahabu kwa sasa ni Tsh 150,000 kwa gram. Serikali haina uhaba wa Tsh. Inaweza kwenda kununua kwa wachimbaji wadogo kwa 160,000. Au kwa hiyo 150,000 lakini bila kodi hivyo mchimbaji anapata pesa nzuri. Yenyewe unaenda kuiuza kwa bei ya dunia kama ni dola 60 kwa gram na kupata dola inazozihitaji sana. Inaweza fanya arrangement hii na wauzaji wa dhahabu ili kupata dola inazohitaji sana. Kifupi itakubali kuingiliwa ili ipate dola. Na

Hili linafanana na wanachofanya sasa NFRA. Wanajumua mahindi kwa bei nzuri kwa kutumia Tsh. Wanataka mtu kutoka nje ananunue kwao kwa pesa za kigeni, dola.

Hili likifanyika, serikali ikanunua labda 30% ya dhahabu za wachimbaji wadogo kwa mtindo huo, litaongeza sana dola nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…