Nimesoma mitandao ya jamii yote maarufu katika mambo ya kitaifa na kisiasa jana. Ni Jaji mmoja tu Biswalo Mganga aliyelalamikiwa kuwa siyo uteuzi "safi" na wanasema Mama "kakosea". Biswalo ana tuhuma nyingi za kubamnikiza watu makosa ya uhujumu uchumi na kujipatia fedha yeye binafsi kupitia kichochoro cha "plea bargain".
Rais Samia Suluhu assan ashauriwe kuunda Tribunal Maalum kwa ajili ya kumchunguza Biswalo Mganga kwa vitendo vyake kama DPP kuanzia mwaka 2016 hadi 2021.
Sheria ya National Prosecution Services Namba 27 ya 2008, kifungu 3-8, imetoa mwongozo wa namna ya kumuondoa DPP