Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Naomba kuuliza mkuu,

Vipi kuhusu kuzaliana kwa viumbe kama binadamu na wanyama wengine, tukiangalia tu kwa upande wa binadamu tunaona population growth kila kukicha, je hii haiwezi kuongeza uzito wa dunia?

Mkuu Dreadnought, Kwa logic ile ya chembe ndogo kabisa zinazounda matter na kwa case hii tunazungumzia mwili au mwili wa kiumbe ukiangaliwa umeundwa kwa kitu gani basi tunakuta element zilizoko hapa hapa duniani. Wataalam wanakuta asilimia 99 ya mwili wa binadamu umeumbwa kwa Oxgen, Hydrogen na Carbon. Wala hatuna tofauti na mimea inagawa yenyewe mpangilio wa molecules unakuwa tofauti kidogo. Hivyo population ya watu na viumbe inatoka kwenye materials au elements za material ziliopo hapa hapa duniani. Kunakuwa na ongezeko la nishati kutoka kwenye mwanga wa jua(mostly). Kwa hiyo miili ya viumbe ni kama recyclable tu, maji yale yale yanazunguka hewa ile ile na madini kutoka kwenye udongo na tukifa yanarudi kule kule.
 
Last edited by a moderator:

Asante sana mkuu kwa maelezo mazuri.
 
Last edited by a moderator:

Naomba kuuliza tena,

Ikiwa labda uko Tanzania, Dar es salaam ukaamua kuruka juu vertically kwa kutumia chombo chochote, halafu ukakaa huko juu (stationary) kwa muda kama wa masaa 12 halafu ukaamua kushuka chini, je inawezekana ukatua sehemu nyingine kutokana na mzunguko wa dunia?

Kama ni ndio kwa nini? Na kama hapana kwa nini?
 
Last edited by a moderator:
Safi sana wataalam nipo nanyi sambamba nikitapa hii Elimu Dunia adhimu!
 

Asante Monstgala kwa maelezo mazuri....., at least niliwahi isoma hiyo theory ya Isostacy ingawa inanipa tabu kuielewa kwa undani. Maana nikiiangalia vile New York au Washington jinsi ilivyojengwa na structures nzito kama maghorofa, madaraja, n.k sijajua ni wapi kumebonyea kubalance hiyo added weight (baharini???). Nilivyoelewa hiyo theory ni kwamba hiyo molten asthenospheric layer ina constant volume, kwa hiyo ili iweze ku-keep balance basi itajisogeza hapo kwenye loss weight pasibonyee, je huko ilikotoka si lazima pabonyee?

Au tayari dunia ipo kwenye equilibrium? kama ndivyo basi inawezekana....
 

Mkuu Njaa
Asante kwa ushirikiano.Niliposema panabonyea sikumaanisha kua patakua na shimo la hasha..namaana kua ile asthinosphere inapobonyea basi husogea na kwenda sehemu ambaya uzito ule umetoka na pale palipobonyea ni kua kuna uzito uliongezeka hivyo pakawa balanced kwa asthenosphere kusogea pembeni(kubonye)...

Hivyo basi nadhani umeona jinsi inavyofanya kazi ni kua sehemu uzito ulipokuja layer inamove kuelekea uzito ulipotoka

Ndio dunia ipo katika equillibrium(kama nilivyosema mwanzo equal balance) na ndio maana halisi ya neno hilo isostacy mkuu

NAWASILISHA.
 
Last edited by a moderator:

hata mti unakua lakini haujongei.
kuzunguka kwa dunia sio tiketi ya wewe kusafirishwa kutoka sehemu moja ya dunia mpaka nyingune.

bado hujawaza kuna siku dunia itakuja kukudondosha katika sayari ingine? Fikiri tofauti.
 
Mheshimiwa Dreadnaught,

Nafurahi sana kuwepo na wakuu wakubwa wenye kufikiria kwa kutumia logic za akili kabisa, na kama tulivyo binadamu tunaweza kukosea na pia kufanikiwa. Ili muradi ni kubadilishana mawazo na busara ili kuelimishana.

Kuhusu swala lako la kuzaliana kwa viumbe kama binadamu na wanyama wengine na mimea kwa ujumla, Jee huzidisha uzito wa Ardhi? kwa hakika kuongezeka kwa viumbe hapa Ardhini haizidishi uzito wowote ule juu ya Ardhi, kwa sababu kama walivyo tujuulisha wakuu wakubwa hapo juu ya kuwa vyote hivi vimetokeana na vitu vilivyomo Ardhini hapa hapa na vinarejea tena ndani yake. Kwa hivyo hakuna kitu kipya cha kuzidisha uzito.

Lakini kama tulivyosoma pia hapo juu ya kuwa Ardhi inaongezeka uzito wa tani 40,000 kila mwaka kwa kupokea vumbi ya angani inayo vutwa na gravity ya Ardhi, pia tunaona kuwa Ardhi kila mwaka inapoteza tani 95,000 kwa muujibu wa kutoroka kwa hydrogen na tani 1600 ya helium pia katika center ya Ardhi hupetea tani 16,000 kwa sababu ya nuklia fusion, kwa hivyo ni jumla ya kadiri ya tani 50,000 ya uzito wa Ardhi yapunguka kila mwaka, nayo ni kadiri ya 0.000000000000001% ya uzito wa Ardhi yenye lengo la uzito wa tani 5,973,600,000,000,000,000,000.

Je! inatubidi tuwe na khofu kwa kupunguka kwa uzito wa Ardhi kila mwaka? hakika hapana khofu kabisa kwa kupoteza hydrojen katika hewa kila mwaka kwa kiasi hicho, kwani itahitajia miaka karibu ya trillioni kuisha kwake. Hapo ikiwa Ardhi ingali hai hata wakati huo!
 
Error.

Uzito sio mass.

Mkuu Anheuser,

Kiswahili ni sio lugha yangu, na mimi ninajitahidi sana kuchagua maneno ya kufahamika. Kwa hiyo ningefurahi ungeliweza kunisahihisha katika neno hilo, kwani niliuliza wengine hapa maana ya mass nao wakaniambia kuwa ni uzito, na kwa kuwa sikuweza kufanikiwa na neno sahihi sikuwa na budi ila kulitumia uzito wakati mimi mwenyewe sikukubaliana nalo.

NAterejea utanielimisha hapo. Nashukuru sana.
 
What will happen kama dunia ikipoteza force of gravity;je vitu vitangukia wapi
Ndo mwisho huo APOCALYPSE.
Ila mwisho wa dunia ni pale dunia itakapo iva na kupasuka. Ila binadamu tutakuwa tumeshahama duniani na kuamia kwenye sayari nyingine au ulimwengu mwingine.
 
Wakuu Anheuser na alhajry na wengine wote

kwanza ningependa "tujadili" kidogo kuhusu tungamo na uzito(mass and weight)

Kwa watu tunaoishi duniani tu hizo ni nadharia tu lakini kwa wenzetu wanaoenda kwenye anga za mbali,mwezini na kwingineko hivi vitu kwao wanavishuhudia

Mass(tungamo) ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada fulani,yaani mfano atom flani ina particles kiasi gan hiyo ni mass.Mass haibadiliki popote unapoenda ulimwenguni iwe kwenye anga au mwezini kwasababu hata ukienda huko "damu yako,ubongo na kila kitu atoms vitabaki ndani ya mwili wako tu haviwezi kutoka...

Tukija upande wa pili weight(uzito) ni kile kiasi ambacho unakua unavutwa na gravity..yaani ni kwa kiasi gani gravity inaact kwako...ndio maana hua uzito unabadilika unapotoka duniani na kwenda mwezini hipungua na unapoenda kwenye space weight inaweza kua sifuri kabisa yani huna uzito

Na hiyo ndiyo tofauti ya mass na weight

NB:inawezekana hayo maneno ya kiswahili(tungamo na uzito) nikawa nimekosea ikawa ni kinyume si mnaelewa elimu yetu wakuu ni ya "kingelesa" lakin nadhani nipo sawa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu alhajry Unapotumia neno Ardhi kama mbadala wa msamiati wa Dunia unaleta ugumu kidogo katika kufikiri. Ardhi ni sehemu ya Dunia kama yalivyo maji, hewa, mimea na vinginevyo. Mass ya Dunia ni mjumuisho wa kila kitu ikiwemo ardhi na hewa hivyo naona kwa kama msamiati huu kama umekusudiwa na wewe kumaanisha Dunia ni moja ya utata.

Ninaweza kusahihishwa maana Kiswahili ni lugha changa.
 

Asante sana mkuu, nimekusoma vizuri.
 

Mkuu Monstgala

Upo sahihi kabisa,ardhi ni sehemu ndogo sana ya dunia ambayo hutokana na kusagika kwa miamba inayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo shughuli za binadamu kama kilimo,na vinginevyo vingi sana..na ardhi ni ile sehemu inayoruhusu maisha ya viumbe kutokana na kua na vitu muhimu kwa ajili ya ukuaji wa viumbe..

Hivyo basi tunaona kua ardhi ni sehemu ndogo sana.
 
Last edited by a moderator:
What will happen kama dunia ikipoteza force of gravity;je vitu vitangukia wapi

vitaelea! walioko anga za mbali hata akiweka chungwa juu ya meza, askitoa ile meza (ambayo pia itaelea tu) chungwa litaelea, hivyo basi katika uhalisia wake hakuna kitu kitachobaki kwani kila kitu kitaelea na kuondoka into space, hata atmosphere na yenyewe itadrift off, hata dunia na yenyewe itameguka mapande na kuondoka kwani hakuna nguvu inayoiweka pale tena!
 
He who hangs the earth on nothing … and holds all things by the word of His Power.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…