Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Ukweli mchungu lakini ndivyo ulivyo, Ili dawa iingie wakati mwingine sindano kwanza. Moja kwa moja kwenye hoja ni kwamba kwamba kama hakuna huduma au bidhaa unayoizalisha na kuitoa kwa jamii kama mbadilishano kutafuta utajiri bila njia hiyo ni kujighilibu akili.
Mahitaji ya jamii yako ndiyo utajiri wako, utajiri mwingi upo kwenye changamoto na matatizo ya jamii. Huduma au bidhaa unazozizalisha na kuzisambaza Ili kutatua kero mbalimbali katika jamii yako ndiyo suri ya mafanikio yako.
Kuna matatizo kila mahali hivyo kuna utajiri kila mahali amka Anza kufumbua macho ya akili yako uone. Pesa ni njia tu ya kubadilishana huduma au bidhaa weka kipaumbele katika kuiona huduma au bidhaa yako Kwa jamii.
Mtu anaweza kukupa pesa na zisikusaidie chochote Kwa sababu pesa ni njia tu ya kubadilishana, tafuta cha kubadilisha kwanza Kwa kuangalia jamii yako inahitaji nini.