Kama haufanyi mambo haya hauna haki ya kumiliki pesa au mali; utaishia kutamani tu na umasikini hautakuacha

Kama haufanyi mambo haya hauna haki ya kumiliki pesa au mali; utaishia kutamani tu na umasikini hautakuacha

Weeee! Ivi searching engine like chrome, na apps like Facebook,X , tuachane navyo twende like Microsoft ni huduma au bidhaa tuaze hapo kwanza
Mimi huwa naona wanaproducts ambazo zinatoa service.
Ndio maana huwa wanazinunua kama products. Mfano Google walinunua Youtube. Facebook wakanunua Whatsapp
 
ila kweli Supply creates it's own demand ni wewe tu kuwa committed unapiga hela.
 
Mungu anao uwezo wote ila ametengeneza mfumo wa kufanya kazi na malaika Ili tujifunze kufanya mambo kimfumo. Utajiri umejikita kwenye kuweza kutengeneza mfumo wa uhitaji na usambazaji huduma au bidhaa.
 
Ukweli mchungu lakini ndivyo ulivyo, Ili dawa iingie wakati mwingine sindano kwanza. Moja kwa moja kwenye hoja ni kwamba kwamba kama hakuna huduma au bidhaa unayoizalisha na kuitoa kwa jamii kama mbadilishano kutafuta utajiri bila njia hiyo ni kujighilibu akili.

Mahitaji ya jamii yako ndiyo utajiri wako, utajiri mwingi upo kwenye changamoto na matatizo ya jamii. Huduma au bidhaa unazozizalisha na kuzisambaza Ili kutatua kero mbalimbali katika jamii yako ndiyo suri ya mafanikio yako.

Kuna matatizo kila mahali hivyo kuna utajiri kila mahali amka Anza kufumbua macho ya akili yako uone. Pesa ni njia tu ya kubadilishana huduma au bidhaa weka kipaumbele katika kuiona huduma au bidhaa yako Kwa jamii.

Mtu anaweza kukupa pesa na zisikusaidie chochote Kwa sababu pesa ni njia tu ya kubadilishana, tafuta cha kubadilisha kwanza Kwa kuangalia jamii yako inahitaji nini.
🙏🙏🙏
 
Kuna watu wanatajirikia kkoo. Kariakoo kuna kila aina ya bidhaa, ukienda kufanya bishara pale sio kwamba unaenda kutatua problem ila unaenda kuongeza chumvi kwenye maji ya bahari.

So utajiri sio lazima kutatua tatizo
 
Usitudanganye kuwa tajiri kwa hali ya vipato vya watanzania wengi wanaotuzunguka ni uongo....unaweza sema uanzishe uzoaji wa taka..hapo hapo manispaa wanataka chao..bado hao wazolewaji taka nao kulipa ni mtiti...wacha bana...wenye utajiri labda uingie kwny magendo...ukwepe kodi n.k
 
Bado naona kama umeegemea kwenye nadharia zaidi. Hebu fafanua vizuri kwa mifano halisi (practical examples) huku ukizingatia mazingira yetu haya yenye utitiri wa kodi za TRA na tozo za kila aina. Maana wengi wanapambana sana lakini wanaishia tu kupata hela ya kula na kuendesha familia zao lakini siyo kutajirika. Hawa wanakosea wapi?

Inaonekana una fomyula ya utajiri ila hujaiweka wazi kama ilivyo kawaida yenu matajiri na watia hamasa (motivational speakers). Huwa mnaishia kugusia gusia tu nadharia za juu juu na kamwe huwa hamtoi codes zote.

Hebu funguka mkuu jinsi ulivyoweza kutajirika kihalali kabisa katika mazingira haya ya Tanzania bila connections zilizokuwezesha kukwepa kodi, kuingiza bidhaa feki n.k.

Utatusaidia wengi; na Mungu Akubariki sana kwa moyo wako huu mwema [emoji1545]
Binafis naamin ili ufanikiwe/kutajirika, uishi nje ya mfumo kwamda mpaka utakapo jipata, ndio urudi kwenye sheria zao
 
Back
Top Bottom